Ni wakati sahihi CHADEMA Kujitafakari!

Ni wakati sahihi CHADEMA Kujitafakari!

Magufuli kufariki sio mpango wako wewe au mimi.
Kamwe jaribu kuheshimu baadhi ya mambo kama vile maamuzi ya Mungu.
Maana Magufuli sio wa kwanza kufa na pia sio wa mwisho kufa.
Bali wote tutaendelea kufa.

Sasa naanza kupata picha kwa nini Chadema mliumia na mbaendelea kuumia na ujio wa Makonda na Sabaya Senior kwenye siasa za CCM ilhali sio chama chenu.
Mkuu hakuna mtanzania anayeumia, ni fikra zako tu!

Wamarekani ndio walioumia hadi wakamzuia kwenda kwao, Marekani.

Yetu macho mkuu, tunasubiri muda utasema! Utasemaje hatujui!!!!
 
Ninasema hivyo kutokana na mtazamo wangu binafsi.siwakilishi chama chochote cha kisiasa nchini.

Mbinu za ufanyaji siasa za chadema kwa sasa zimepitwa na wakati au zimechokwa!

Ninaposema hivyo nina maanisha kwamba ...wananchi wanahitaji tofauti.
Wakati Chadema pia mnalo hitaji lenu tofauti.

Jaribuni kukaa na kupata watunga sera mahiri ili wawasaidie kutunga sera zinazowagusa wananchi kwa 100%.

Badala ya Sera hizi za matukio na kutafuta Sympathy kwa watanzania.
Maana hata watanzania pia wanaihitaji hiyo hiyo Sympathy toka kwenu wanasiasa.Badala yake nyinyi mnawatumia wananvhi kama ngao ya kujikingia ili mjinufaishe binafsi

Kwa Dunia hii yenye utandawazi uliokithiri,kuwa mpinzani kunahitaji uwe mkweli na muwazi.uwe kweli unaakisi uhalisia na wananchi waweze kuweka imani kwako

Maana uelewa wa wananchi ni mkubwa kwa sasa tofauti na hapo awali.Pia mawasiliano na mifumo yake imebadilika kwa kiasi kwamba wananchi kwa asilimia kubwa wanapata na kuelewa habari nyingi nchini kwa wakati husika na kusha kuzifanyia upembuzi makini.

Ila wanasiasa mmeeendelea kuwachukulia wananchi kama watu wasiojielewa elewa ki- viile!

Lakini kumbe unakuta wananchi ndio wamewapuuza wanasiasa baada ya kuchoka na ngonjera zao zisizo na ukomo wala ukweli.

Sasa siasa imegeka kuwa sehemu ya ajira na kipato cha utajiri, na sio kipawa cha uongozi na maadili mema!

Hili ni tatizo kubwa kwa wanasiasa wa Tanzania..kote kabisaa!
Sio CCM wala Chadema pekee,bali vyama vyote!

Tukisema Chadema mnapenda kick za matukio kupata Political Mileage mnasema tunakosea?
Mfano wa hili ni juzi huko Katesh.

Chadema jipimeni kwa kina maana kwa uhalisia ni kwamba mnahitaji uongozi mpya wenye kuweza kufanya mabadiliko makubwa na ubunifu wa sera na mbinu za ufanyaji siasa kuendana na wakati uliopo ili muweze kwenda sambamba na upepo halisi wa kisiasa nchini.

Viongozi waliopo kwa sasa pumzi yao inaonekana rasmi, ndio inaelekea imefikia ukomo kisiasa.
Hawana mbinu mpya za kukabiliana na CCM wanaobadilishana vijiti kila baada ya miaka kumi(10).

Kama ni riadha ya kisiasa!
Mbowe ameishazunguka uwanja mpaka amepitiliza na vijiti nje ya uwanja. na sasa anakimbia peku kwenye lami.
Msaidieni......

Kwa kuwa matusi ni sehemu ya seraza baadhi yenu!sintawashangaa mkianza kuyaporomosha hapa
Ila mimi nimemaliza kutoa langu la Moyoni.

Niwatakie SABHATHO njema!
Kuiondoa CCM madarakani hatuhitaji kuwa na chama kistaarabu, tunapaswa kuwa na chama mithili ya M23.
 
Mtoa hoja unasemea watanzania gani waliokupa uwezo wa kuwasemea?pambana mwenyewe na usitegemee watu wengine wakupiganie, uoga wako wa kizuzu, ndio kila wakati unakufanya uje kulalama humu, push back yako ipo wapi? Unalalama humu then usiku ukifika unanyatia kitanda chako!

Miaka 60 sasa Tanzania imetawaliwa na ccm,bado wale maadui wapo na wametamalaki, ujinga, umasikini, maradhi na sasa rushwa!

Mkuu mtoa hoja Shuka huko juu na uje kwenye hawa poor of the poorest ujionee uhalisi wa maisha yao, mvua za jana nimetembelea Temeke, ni shida mkuu, kila nyumba imepata swimming pool chafu ,inayonuka mbele ya nyumba zao, ukiuliza mhusika yupo wapi ,yeye anaishi Masaki!!
Wewe ni nyumbu kweli kweli!, hebu nitajie nchi ambayo ilisha waangamiza hao maadui watatu?!, hebu nitajie,ni nchi gn hapa duniani?
 
Ebu kwanza soma andiko hizi kashfa zingine ni ushamba na utovu wa "ELIMU"
Hivi unachokisema unaweza ukasimama mbele ya Mbowe na Lissu ukawaambia? Kwakua wewe ni mwanaccm basi unajiona una akili kuliko wao! CCM inachota pesa kujiendesha na si kwakificho, hawa wanaiendesha Chadema kwa maarifa yao halafu unatikea wewe kinyangarakasha na kuwafundisha! Acha ujinga huo.
 
Wewe ni nyumbu kweli kweli!, hebu nitajie nchi ambayo ilisha waangamiza hao maadui watatu?!, hebu nitajie,ni nchi gn hapa duniani?
Makelele yote hayo ni kujua nchi ambazo zinaangamiza maadui hao, ushelisheli, Mauritius, Botswana, achilia mbali nchi za baltic, soma hii,mpangaji mkuu wa magogoni anauliza swali mbona Singida kuna umasikini mkubwa!!!,mlala hoi kakamatwa ni vidoti vya vitenge border ataumizwa mno,asas kaingiza nchini 500 tankers ,mpumbavu kama wewe utaingia humu na kumsifia
 
Ukiwa na akili timamu huwezi kuwa chadema...

Mala kumi CUF na ACT kwa mbali.
 
CHADEMA ni sikio la kufa .nilishaandika sana juu ya CHADEMA kufirisika kifikira na kugota kimawazo.kwa sasa haina mawazo mbadala zaidi ya kuvizia matukio kama mafisi wa kisiasa. chama kimepoteza muelekeo na hakina tena ushawishi kwa wananchi.hii ni kwa kuwa Watanzania hawana imani tena na CHADEMA kwa sababu wanajuwa ni chama kinachobadili gia wakati wowote ule
 
Watanzania wamekata tamaa, hakuna wa kuwasemea. Huku nauli zimepanda , kule mgao wa umeme.
Waliopo hawawataki, wasiokuwepo hawawaaamini. Watanzania wafwaaaaaaaa.
 
Yaani tunamtegenea sana Mungu kwa wakati huu kisiasa.
Kuliko wakati mwingine wowite ule!
 
Ninasema hivyo kutokana na mtazamo wangu binafsi.siwakilishi chama chochote cha kisiasa nchini.

Mbinu za ufanyaji siasa za chadema kwa sasa zimepitwa na wakati au zimechokwa!

Ninaposema hivyo nina maanisha kwamba ...wananchi wanahitaji tofauti.
Wakati Chadema pia mnalo hitaji lenu tofauti.

Jaribuni kukaa na kupata watunga sera mahiri ili wawasaidie kutunga sera zinazowagusa wananchi kwa 100%.

Badala ya Sera hizi za matukio na kutafuta Sympathy kwa watanzania.
Maana hata watanzania pia wanaihitaji hiyo hiyo Sympathy toka kwenu wanasiasa.Badala yake nyinyi mnawatumia wananvhi kama ngao ya kujikingia ili mjinufaishe binafsi

Kwa Dunia hii yenye utandawazi uliokithiri,kuwa mpinzani kunahitaji uwe mkweli na muwazi.uwe kweli unaakisi uhalisia na wananchi waweze kuweka imani kwako

Maana uelewa wa wananchi ni mkubwa kwa sasa tofauti na hapo awali.Pia mawasiliano na mifumo yake imebadilika kwa kiasi kwamba wananchi kwa asilimia kubwa wanapata na kuelewa habari nyingi nchini kwa wakati husika na kusha kuzifanyia upembuzi makini.

Ila wanasiasa mmeeendelea kuwachukulia wananchi kama watu wasiojielewa elewa ki- viile!

Lakini kumbe unakuta wananchi ndio wamewapuuza wanasiasa baada ya kuchoka na ngonjera zao zisizo na ukomo wala ukweli.

Sasa siasa imegeka kuwa sehemu ya ajira na kipato cha utajiri, na sio kipawa cha uongozi na maadili mema!

Hili ni tatizo kubwa kwa wanasiasa wa Tanzania..kote kabisaa!
Sio CCM wala Chadema pekee,bali vyama vyote!

Tukisema Chadema mnapenda kick za matukio kupata Political Mileage mnasema tunakosea?
Mfano wa hili ni juzi huko Katesh.

Chadema jipimeni kwa kina maana kwa uhalisia ni kwamba mnahitaji uongozi mpya wenye kuweza kufanya mabadiliko makubwa na ubunifu wa sera na mbinu za ufanyaji siasa kuendana na wakati uliopo ili muweze kwenda sambamba na upepo halisi wa kisiasa nchini.

Viongozi waliopo kwa sasa pumzi yao inaonekana rasmi, ndio inaelekea imefikia ukomo kisiasa.
Hawana mbinu mpya za kukabiliana na CCM wanaobadilishana vijiti kila baada ya miaka kumi(10).

Kama ni riadha ya kisiasa!
Mbowe ameishazunguka uwanja mpaka amepitiliza na vijiti nje ya uwanja. na sasa anakimbia peku kwenye lami.
Msaidieni......

Kwa kuwa matusi ni sehemu ya seraza baadhi yenu!sintawashangaa mkianza kuyaporomosha hapa
Ila mimi nimemaliza kutoa langu la Moyoni.

Niwatakie SABHATHO njema!
Tunarudi kule kule. Je wasomi na watanzania kwa ujumla tunalijua tatizo letu? Tatizo la Tanzania ni katiba au ni upinzani kutokuwa na sera nzuri? Jibu ni: KATIBA. Sisemi kuwa Chadema ni wakamilifu, lakini pamoja na hizi weakness ulizosema, bado CCM inaogopa kufanya free and fair election. Wewe unadhani Chadema ikifanya hayo unayosema, CCM itabadilika na kuleta katiba na uchaguzi huru? Nadhani wewe ni mmoja ya watanzania wanapoteza muda ku-address wrong cause of our failure in democracy. Bora ungesema sisi wananchi ndiyo tatizo ningekuelewa kwa sababu wananchi wakijitambua wanaweza kuifanya hata hii CCM mbovu kuwa chama kizuri.
 
CHADEMA ni sikio la kufa .nilishaandika sana juu ya CHADEMA kufirisika kifikira na kugota kimawazo.kwa sasa haina mawazo mbadala zaidi ya kuvizia matukio kama mafisi wa kisiasa. chama kimepoteza muelekeo na hakina tena ushawishi kwa wananchi.hii ni kwa kuwa Watanzania hawana imani tena na CHADEMA kwa sababu wanajuwa ni chama kinachobadili gia wakati wowote ule
Ni kweli umewahi kuandika kuhusu hili.na mimi pipa sikupingi kwa hilo!
Lakini sasa tatizo limekuwa kubwa kitaifa!
Kwa maana kwamba hata huko CCM kumekuwa Chung cha maafa ya kisiasa!

Waliostahili kuongiza ndio wako benchi.Na majizi ndio yametamalaki ulingoni.
 
Watanzania wamekata tamaa, hakuna wa kuwasemea. Huku nauli zimepanda , kule mgao wa umeme.
Waliopo hawawataki, wasiokuwepo hawawaaamini. Watanzania wafwaaaaaaaa.
Hizi sasa ni moja kati ya misemo mingi ambayo inawafanya watanzania wazidi kudidimia na viongozi kunawiri. Hivi kwa nini unadhani watanzania wanatakiwa kuwa na mtu wa kuwasemea? Huoni unajidhalilisha mwenyewe na nchi yako kwa kusema watu wazima zaidi ya milioni 30 hawawezi kusema wenyewe na wanasubiri mtu wa kuwasemea? Come on watanzania, sisi ndiyo tunatakiwa tujisemee wenyewe na siyo kusubiri watu watusemee.
 
Yaani tunamtegenea sana Mungu kwa wakati huu kisiasa.
Kuliko wakati mwingine wowite ule!
Kaa basi umtegemee Mungu uone kama kutakuwa na matokeo. Mungu ametupa akili na maarifa halafu tujifungie ndani tusubiri atufanyie. Ni taifa gani uliloona wananchi wake wamekaa kimya wakimtegemea Mungu na wakaendelea? Bila sisi wananchi kujitambua hakuna kitakachobadilika.
 
Kwa hiyo unaamini chaguzi zote Chadema wanashinda, ccm wanaiba kura dah, unahitaji msaada mkuu, akili zako haziko sawasawa.
Ni wapi nimesema chaguzi zote cdm wanashinda na ccm wanaiba? Ninaamini chaguzi zinachezewa. Ingekuwa matokeo halisi yanatangazwa, leo hii ccm isingekuwa na nguvu ya kufanya maamuzi pekee huko bungeni, na uwezakano wa wao kuwa chama Cha upinzani ungekuwa mkubwa. Hili Wala sibahatishi.
 
Ni kweli umewahi kuandika kuhusu hili.na mimi pipa sikupingi kwa hilo!
Lakini sasa tatizo limekuwa kubwa kitaifa!
Kwa maana kwamba hata huko CCM kumekuwa Chung cha maafa ya kisiasa!

Waliostahili kuongiza ndio wako benchi.Na majizi ndio yametamalaki ulingoni.
Lucas atakubishia HP kwenye majizi.
 
CHADEMA isilaumiwe sana,

Alaumiwe aliyegoma kuitenga CCM na mfumo na kugoma kuisajili kama chama Cha siasa hapo 1992.
 
Mbinu za ufanyaji siasa za chadema kwa sasa zimepitwa na wakati au zimechokwa!

Chadema jipimeni kwa kina maana kwa uhalisia ni kwamba mnahitaji uongozi mpya wenye kuweza kufanya mabadiliko makubwa na ubunifu wa sera na mbinu za ufanyaji siasa kuendana na wakati uliopo ili muweze kwenda sambamba na upepo halisi wa kisiasa nchini.

Kama ni riadha ya kisiasa!
Mbowe ameishazunguka uwanja mpaka amepitiliza na vijiti nje ya uwanja. na sasa anakimbia peku kwenye lami.
Msaidieni......
Mkuu voicer , huu ni ushauri mchungu kwa Chadema, ila ndio ukweli wenyewe, angalia akina sisi, tuliwashauri nini Chadema, lini na matokeo ya kupuuza ushauri huo!.
Ili Chadema iendelee kuwa relevant na serious opposition, it has to change from Chama harakati cha siasa za matukio na siasa za majitaka, into chama tawala in waiting kwa kufanya real politics za siasa mbadala wa CCM.

- Swali kuhusu tabia ya kususa, kugomea au kuzira: Je, si tabia za kike, si utoto?

P
 
Back
Top Bottom