Nimeona dondoo za kitabu cha mweshimiwa raisi mstaafu wa awamu ya tatu, Mh Benjamin Mkapa zikieleza mapungufu ya kile tunaita "wabunge"
binafsi nakubaliana na hoja ya wabunge hawafanyi lolote, sijasema yeye kasema hivyo bali nimesema mimi nasapoti hoja hiyo.
Ukitazama madaraka na majukumu ya mbunge au wabunge kikatiba ni makubwa sana, tena wao ndio mhimili unaotakiwa kuwa juu ya mihimili mingine miwili. Lakini cha kusikitisha mfumo na utaratibu wa hawa watu tuliojiwekea hauwafanyi kutumika na kuwajibika.
Mbunge ndiye muwakilishi wa wananchi anayeisimamia serikali lakini mbunge huyu anaishi dar anawakilisha jimbo lililoko mkoa mwingine kijijini. Kazi yake ni kwenda bungeni kujadili na kurudi kwenye shughuli zake.
Tunahitaji mbunge anayekaa kwenye ofisi ya jimbo kama hayuko bungeni, bungeni wamepitisha nini basi anafuatilia katika jimbo lake utekelezaji wake, mwananchi ana shida au changamoto anakutana nazo ofisi za umma anamfuata mbunge ofisini kwake,
Summary ya yale anayokutana nayo katika utendaji wake wa kila siku jimboni iwe ndiyo mijadala yake bungeni
Chukua mfano mdogo Juzijuzi tulisikia mkoani Mwanza wilaya ya ukerewe wakituambia kumekuwa na mchezo unafanyika kwenye madawa yaliyokuwa yakitoka MSD, madawa yanaibiwa wala hayafiki katika wilaya husika.
Katika Tatizo hili mimi sitazami mifumo ya utendaji wa serikali katika hili bali natazama jinsi ambavyo mbunge kama angekuwa anafanya kazi yake angegundua tatizo hili hata kama serikali wameshindwa kubaini.
kama madawa yakiibiwa hivyo hayafiki sehemu husika maana yake wananchi wakienda hospitali watakuwa wanambiwa madawa hayapo wakanunue. Kama mbunge umefika jimboni kwako ukawaambia wananchi katika magonjwa haya na haya madawa yapo hospitali na kama kama mtu akienda hospitali akaambiwa akanunue dawa lete taarifa katika ofisi ya mbunge.
Sasa madawa yakiibiwa wananchi wataleta "feedback kwa mbunge" na mbunge ataenda kufuatilia kwa wahusika kwenye jimbo lake kwanza kuna tatizo gani wananchi wanaambiwa hakuna dawa. Jambo limeshindikana kutatuliwa ngazi ya wilaya ambayo nadhani ndio utawala wa jimbo unakosimama basi mbunge atapeleka hoja kwa waziri husika na kama shida ni kubwa ya kuhitaji attention ya watunga sera wote kulijadili basi alipeleke bungeni.
Lakini hoja za sasa ni mtu kujadili kivyepesivyepesi tu kuwa watu wanakwenda hospitali na kuambiwa hakuna madawa yaani wanaongea kwa generality tu na kufanya hata kwenye wizi na kusikokuwa na wizi kuonekana shida ni moja na inapewa majibu mepesi tu ya wizara inaweka mikakati gani n.k
mkazi