Ni wakati Mwafaka wa kuwa na "Wabunge Wakazi"

ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,620
1,407
Nimeona dondoo za kitabu cha mweshimiwa raisi mstaafu wa awamu ya tatu, Mh Benjamin Mkapa zikieleza mapungufu ya kile tunaita "wabunge"

binafsi nakubaliana na hoja ya wabunge hawafanyi lolote, sijasema yeye kasema hivyo bali nimesema mimi nasapoti hoja hiyo.

Ukitazama madaraka na majukumu ya mbunge au wabunge kikatiba ni makubwa sana, tena wao ndio mhimili unaotakiwa kuwa juu ya mihimili mingine miwili. Lakini cha kusikitisha mfumo na utaratibu wa hawa watu tuliojiwekea hauwafanyi kutumika na kuwajibika.

Mbunge ndiye muwakilishi wa wananchi anayeisimamia serikali lakini mbunge huyu anaishi dar anawakilisha jimbo lililoko mkoa mwingine kijijini. Kazi yake ni kwenda bungeni kujadili na kurudi kwenye shughuli zake.

Tunahitaji mbunge anayekaa kwenye ofisi ya jimbo kama hayuko bungeni, bungeni wamepitisha nini basi anafuatilia katika jimbo lake utekelezaji wake, mwananchi ana shida au changamoto anakutana nazo ofisi za umma anamfuata mbunge ofisini kwake,

Summary ya yale anayokutana nayo katika utendaji wake wa kila siku jimboni iwe ndiyo mijadala yake bungeni

Chukua mfano mdogo Juzijuzi tulisikia mkoani Mwanza wilaya ya ukerewe wakituambia kumekuwa na mchezo unafanyika kwenye madawa yaliyokuwa yakitoka MSD, madawa yanaibiwa wala hayafiki katika wilaya husika.

Katika Tatizo hili mimi sitazami mifumo ya utendaji wa serikali katika hili bali natazama jinsi ambavyo mbunge kama angekuwa anafanya kazi yake angegundua tatizo hili hata kama serikali wameshindwa kubaini.

kama madawa yakiibiwa hivyo hayafiki sehemu husika maana yake wananchi wakienda hospitali watakuwa wanambiwa madawa hayapo wakanunue. Kama mbunge umefika jimboni kwako ukawaambia wananchi katika magonjwa haya na haya madawa yapo hospitali na kama kama mtu akienda hospitali akaambiwa akanunue dawa lete taarifa katika ofisi ya mbunge.

Sasa madawa yakiibiwa wananchi wataleta "feedback kwa mbunge" na mbunge ataenda kufuatilia kwa wahusika kwenye jimbo lake kwanza kuna tatizo gani wananchi wanaambiwa hakuna dawa. Jambo limeshindikana kutatuliwa ngazi ya wilaya ambayo nadhani ndio utawala wa jimbo unakosimama basi mbunge atapeleka hoja kwa waziri husika na kama shida ni kubwa ya kuhitaji attention ya watunga sera wote kulijadili basi alipeleke bungeni.

Lakini hoja za sasa ni mtu kujadili kivyepesivyepesi tu kuwa watu wanakwenda hospitali na kuambiwa hakuna madawa yaani wanaongea kwa generality tu na kufanya hata kwenye wizi na kusikokuwa na wizi kuonekana shida ni moja na inapewa majibu mepesi tu ya wizara inaweka mikakati gani n.k
mkazi
 
Point sana chama kiwe kinapitisha Wabunge wakazi

Hili lisiwe hiari kwa vyama vya siasa au wagombea bali tunahitaji kufanya marekebisho ya Katika ili kudefine upya sifa za kuwa mbunge na majukumu ya mbunge.

ingawa hili ni gumu kulifanya kwa maana unahitaji wabunge waliopo kupitisha hoja hii ambayo ni kama kuwaambia wakate matawi waliyoyakalia lakini naamini
1. Vyama vyote vina nia ya dhati ya kuwatumiakia wananchi na hivyo vingipenda kuona inakuwepo mifumo ya kuwafanya wawakilishi wa wananchi ambao ni wabunge wanawajibika ipasavyo hivyo vyama vikilipa msukumo na msimamo ukawa ni wa chama basi wabunge wake watapitisha tu

2. Serikali ikiweka nia ya dhati ya kulisukuma hili litafanikiwa maana wabunge wakiwajibika katika majimbo yao inawasaidia sana serikali katika supervision.
 
Nchi inaongozwa kutokea Dar! Kwa sasa wanapanga mikakati ya ubunge.
Anyway! Wanaweza kuwa wazawa, na wakichuma wakimbia.
Tumesikia vigogo wamechuma Bongo na kukimbilia South, ....kusimika mahekalu, huku asilia wanaishi kimachalemachale. Kikisanuka, waamshe na familia zao. Ndivyo ilivyo kwa watawala wengi wa Afrika.
Kwa maoni yangu, kuna namna TAMISEMI inaweza kuboreshwa ili transparency, check and balance vizae matunda.
 
Ipo haja kupunguza idadi wabunge.Walau 2 kila mkoa kwa njinsia.

Kweli kabisa kuna haja ya kuwa na wabunge wanaoendana na mahitaji yetu.

kwa kuongezea katika hili mimi nilitamani mbunge awe ni mwakilishi wa wilaya, Badala ya kuhangaika na Kusema sijui wakuu wa mikoa wachaguliwe na wananchi au wakuu wa wilaya basi kama fedha za serikali kuu zinatolewa ki wilaya au halmashauri na makusanyo cha chini yanafanyika katika ngazi hiyo basi wananchi wawe na mwakailishi ngazi hiyo.
 
Yeah! Ndio maana naona haja ya kuifanyia reform TAMISEMI.
Kuna nafasi, kwa maoni yangu - kama vile Katibu Tarafa - zinapaswa kuondolewa.
 
Hata akikaa jimboni kama ni mpiga makofi kwa kila kinachozungumzwa na kusema ndio kimepita ni kazi bure.
 
Hata akikaa jimboni kama ni mpiga makofi kwa kila kinachozungumzwa na kusema ndio kimepita ni kazi bure.

hii ni ibara ya 63 ambayo ndiyo iliyoweka msingi wa utendaji wa wabunge. Miaka ya 1977 wakati wanatunga sheria mazingira yaliyokuwepo yaliruhusu pengine wabunge kukutana bungeni na kujadili basi.

leo hii miaka zaidi ya 40 baadae katika hii bado inatafsiriwa kwa mazingira ya mwaka 1977. mambo mengi yamebadirika lakini hawa wawakilishi wetu ambao ibara ya 63 (2) inasema wao ndio chombo kikuu cha Jamhuri ya muungano bado wanaenda kwenye biashara zao wakitoka huko wanaenda eti kumtetea mmnyonge kwa mijadala tu.

ni lazima tuone haya ya kupiga makofi yanatokana na mtu kwenda kujadili mambo ambayo hajajiandaa.

haiwezekani mtu akae jimboni kwake, madawa yamepitishwa lakini jimboni kwake hayajafika alafu ampigie makofi waziri wa afya.

ni swala la kutengeneza sysytem inayojisimamia yenyewe basi watu watasukumana wenyewe. Imagine umepeleka tatizo lako kwa mbunge na hujapata jibu alafu mbunge wako anakwenda bungeni anapiga makofi kwa hatuba zinazosema hakuna shida kama hizo si mbunge kajia kitanzi kinachosubiri uchaguzi ufike mwananchi achomoe stuli chini basi.

mwananchi - serikali - mbunge- mwananchi ni mduara uliokamilika ambao ukianza kufanya kazi basi aliyezembea anabainika na system inamuwajibisha.

Yaani mwananchi atimize wajibu wake wa kufanya kazi na kuchangia maendeleo kupia kodi - serikali ikusanye kodi na kurudisha maendeleo kwa wananchi huku mbunge akiwepo kama kiunganishi cha serikali na wananchi. kwa sasa wananchi wamechochewa kila mmoja anaona nchi yetu kila siku TRA wanatangaza kuongezeka kwa mapato. Serikali imepata mwenyewe tunaona kasi ya miradi ya maendeleo Sekita pekee iliyobaki ni hiki kiunganishi kilichopewa nguvu ajabu kikatiba lakini hakijitambui au kilinyangangywa sijui.

Ninachojua ni kuwa kiunganishi hiki kikizinduka tutapaa kimaendeleo kwa maana kila kona system itajisimamia yenyewe na

Shida iliyokuw
1573819793344.png
 
Nchi inaongozwa kutokea Dar! Kwa sasa wanapanga mikakati ya ubunge.
Anyway! Wanaweza kuwa wazawa, na wakichuma wakimbia.
Tumesikia vigogo wamechuma Bongo na kukimbilia South, ....kusimika mahekalu, huku asilia wanaishi kimachalemachale. Kikisanuka, waamshe na familia zao. Ndivyo ilivyo kwa watawala wengi wa Afrika.
Kwa maoni yangu, kuna namna TAMISEMI inaweza kuboreshwa ili transparency, check and balance vizae matunda.
Una mawazo mazuri sana sana. Hili hata mimi nilishaliwaza siku nyingi. Wabunge wengi siyo wakazi wa maeneo wanayowakilisha. Infact kwenye nafasi ya ubunge kuna mapungufu mengi sana ambayo yanatakiwa kurekebishwa na hili la ukazi ni moja. Iwekwe sheria mbunge awe ni mwenyeji wa eneo husika na awe anaishi pale muda wote. Akisafiri basi anaenda tu kwenye vikao vya bunge. Halafu hawa wabunge wa viti (soma vitu) maalum wooote wanatakiwa kuondolewa. Hawa wamekuwa wanachaguliwa wale wanawake wajanja wajanja (wengi vimada wa viongozi) wanaishi mjini na wakiona wakati wa uchaguzi umekaribia ndiyo wanakimbilia maeneo husika. Kama ni suala la kutaka uwakilishi wa makindi fulani basi tuweke utaratibu wananchi kuwapigia kura huko majimboni. Idadi ya wabunge nayo ipunguzwe. Tuna waaunge wengi sana pasipo sababu yoyote. Kuna mengi ya kuangalia lakini ni vigumu wanasiasa kukubali kubadilisha kwani ndiko kwenye ulaji wao.
 
Tatizo lipo kwa wananchi wenyewe.
Kwa nini wamchague mtu ambaye siyo mwenzao kuwawakilisha au kuwasemea?
Anatakiwa muwakilishi wanayeshiriki naye katika mazingira wanayoishi.
Umasikini unaanzia hapo kwenye fikra za kuchagua mgeni.
 
ukiwalaumu wananchi basi hakuna haja ya kuwa na viongozi, kila mtu angeona njia sahihi na akafuata akafanikiwa, lakini kiuhalisia maisha hayako hivyo. jamii zetu nyingi mbumbu ambao wakipewa vitu wanachagua, wakichezewa ngoma wanachagua bado ni wengi. tatizo kubwa ni elimu au uelewa kwa maana wengi wetu hatuwezi kuunganisha maisha yetu na hawa tunaowachagua.

waliibuka wahuni wakabadili taswili za nafasi hizi, wapo waliozipa taswila za ngo za kutoa misaada hivyo wanatafuta misaada na kwenda kugombea. imekuwa kama kazi za mbunge ni kutoa mabati ya shule, kuchangia mifuko ya simenti n.k.

unahitajika mwongozo unaowaelekeza wananchi na kazi ya wananchi iwe ni kumalizia tu
 
Viongozi hutokana na wananchi, hivyo wananchi wa hovyo huchagua viongozi wa hovyo.
Wananchi wakiwa vizuri hawawezi kuwakubali viongozi wapuuzi hata kidogo.
Uwepo wa viongozi wa ajabu ajabu siku hizi ni uthibitisho wa hilo.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom