Ni wakati gani muafaka?

Masikini_Jeuri

JF-Expert Member
Jan 19, 2010
6,829
1,296
Wadau kuna tabia inajitokeza hivi sasa kwa baadhi ya wanandoa kutokeapo kutokuelewana ama mataiizo baina yao basi moja kwa moja upande unaoona kuonewa huamua kwenda kuyasema matatizo ama kutafuta ushauri nje.

Matatizo ya ndoa yapo mengi na kila ndoa ina matatizo yake; Je ni upi muda muafaka na baada ya kuwa hatua gani zimechukuliwa ndio ikulazimu uende nje ya mipaka ya ndoa kutoa duku duku lako iwe ni kwa wazazi, marafik,i ndugu; wazee, viongozi wa dini na kadhalika?

Je ni kweli uwaalikapo watu wa nje kumaliza tatizo lako la ndoa wankuwa na tiba ya kweli na ya kudumu ya ndo yenu ama ndio kuukuza mgogoro?

Je ni yapi pia utawashirikisha hawa watu wa nje ama kila kitu?

Tuelimishane.
 
Ni bora kwenda kwa mtu aliye neutral e.g. counselor. Kwenda kwa ndugu au marafiki hakusaidii sana. ndugu ndio wabaya zaidi ktk kutoa ushauri kwenye mambo haya. Ni vigumu sana kwa wao kuwa neutral.

Na mara nyingi kama nyinyi wenyewe wawili mmeshindwa kuyatatua matatizo yenu, sidhani kama kuna mwingine wa nje atakayeweza. Mlianza uhusiano wenu wenyewe na mtaumaliza nyinyi wenyewe.
 
Yakikutokea ya kuhitaji ushauri wa masuluhisho ya ndoa. Nakushauri ndugu yangu usiende kutafuta upatanishi kwa hawa wanaojiita watumishi wa Mungu! Hakika Watakumegea!
 
NN ikiwa ndio nimeletewa mashataka kama Big brother..............niyapige chini?
 
tatizo mpaka liwe na ukubwa wa kiasi gani ndo twende kwa washauri?

manake kuna watu wengine hata wao wenyewe hawajamaliza mbinu za kutatua tatizo unakuta keshalipigia upatu.
 
Yakikutokea ya kuhitaji ushauri wa masuluhisho ya ndoa. Nakushauri ndugu yangu usiende kutafuta upatanishi kwa hawa wanaojiita watumishi wa Mungu! Hakika Watakumegea!


B........kuna wachungaji wanawake sikuhizi..............................lol
 
VUNJA UKIMYA! ZUNGUMZA NA MWENZIO.

Ujue kila mtu ana matatizo yake tena pengine ya ko ni madogo. Hivyo jaribuni kutatua wenyewe, japo ukiona maamuzi yako ni kufa au kuua basi nenda jiulize utapata jibu kwa lolote lile.

Hata wana JF wana mawazo mazuri. Waambieni watu waje walete tuchangie. ndoa zao zitapona tu!
 
tatizo mpaka liwe na ukubwa wa kiasi gani ndo twende kwa washauri?

manake kuna watu wengine hata wao wenyewe hawajamaliza mbinu za kutatua tatizo unakuta keshalipigia upatu.

Ndo hapo shida yangu.........................mie nimeletewa mashtaka ambayo kwangu nayaona ni madogo ya kumaliza ndani wao wenyewe lakini mletaji kwake ni kero kubwa. Ndo msingi wa swali langu
 
tatizo mpaka liwe na ukubwa wa kiasi gani ndo twende kwa washauri?

manake kuna watu wengine hata wao wenyewe hawajamaliza mbinu za kutatua tatizo unakuta keshalipigia upatu.
hao wana matatizo makubwa chapa vibao!
 
Pale mambo yanapovuka mipaka na kujirudia unahitaji kuomba msaada la sivyo watu watshangaa unapata Presha unakufa taratibu kumbe ulikosa kutoa nafasi ya kusikilizwa na kusaidiwa
 
Mfano kwa hii kesi niliyoletewa naweza ingilia kwlei swala la unyumba wa Sister na shemeji?..................Kia afrika ni ngumu!
 
NN nakubaliana na wewe kabisa, ndugu hawatatui tatizo na wanaegememea upande mmoja always esp kwa mwanamme, hata kama amefumaniwa still yeye ndo anaonekana yuko right!
 
Matatizo hayana ukubwa wala udogo, hayana muda maalumu wala sababu. Yenyewe hujitokeza tu. Bahati mbaya yanakua na kusambaa kama saratani, yasipogundulika mapema na kupatiwa 'tiba.'
Binafsi nakushauri ubadili mawazo yako kwamba "tatizo lenyewe dogo!". Wao kwao tayari ni kubwa hilo.
Mfano; Ni busara na jukumu lako wewe kuwasikiliza. Inaelekea kwao (tatizo) hawana masikilizano mpaka pawepo mtu wa kati...kama referee vile!
 
Mi nadhani ukiona tatizo limefikia kwamba umelipeleka kwa third party ujue hapo na ndoa unaiweka rehani

dawa ni kuyazungumza wawili...so mkuu MJ kama inakuwa kwamba sister na shemeji...washauri warudi ulingoni wayamalize wenyewe...unless kuna issue ya jinai kama kutishiana kuuana nk
 
Pale mambo yanapovuka mipaka na kujirudia unahitaji kuomba msaada la sivyo watu watshangaa unapata Presha unakufa taratibu kumbe ulikosa kutoa nafasi ya kusikilizwa na kusaidiwa
...No!!! FL1, siamini hata tatizo likiwa kubwa kiasi gani eti kwenda kueleza wazazi, ndugu, marafiki ndio suluhu. kwa mtazamo wangu huko ni kufanya mambo kuwa mabaya zaidi. Mi huwa naamini katika nafsi zenu wewe na mtu wako. kama kuna tatizo mnatakiwa kuelezana, kuonyana, kushauriana na hatimaye kusamehana. matatizo kwenye ndoa au mahusiano yapo jambo la msingi ni wewe kuwa na kiwango (kuwa with all efforts ambazo unaamini ni za kweli) ikishindikana unabwaga manyanga unakula kona...maisha lazima yaendelee. Siamini hata kidogo katika kuwekeana vikao...
 
Back
Top Bottom