Ni Wajibu wa Nani?

Spear_

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
1,603
486
TaboraPupilsdown.jpg

Kuna mikoa ukisikia wanafunzi wanakaa chini unaweza usisikitike sana.....ila kwa hili la Tabora mkoa ambao una Madini na Misitu...inasikitisha sana...eti ndo wasomi wa kesho wa nchi hii......

Kwenye mazingira kama haya, kwa nini wazazi wasitafute solution ya Tatizo hili? watakuambia wanasubiri serikali wakati watoto wao ndo wanateseka.......Tunayoweza kufanya tusisubiri Serikali!!
 
]View attachment 49637

Wazazi kwa Baadhi ya shule tunachangia MADAWATI kila mwaka na bado tatizo haliishi, japo dawati halichakai kwa Mwaka mmoja
Ukibagua miji/mikoa yenye Rasilimali nyingi ndio ipate huduma zote muhimu na kusiko na rasilimali wabaki Tu, Unaimega nchi ktk mafungu ambayo mwisho wake sijui itakuwaje

WIZARA YA ELIMU haija pata kiongozi atakaetoa vipaumbele kwa matatizo tuliyonayo
 
Kwa kweli haingii akilini kuona kuwa Tanzania tumeshindwa kabisa kutatua tatizo la madawati. Yaani tukisha jenga madarasa tu kazi imeiisha na tunategemea watoto waingie madarasani na kuendelea na masoma kwa kuchuchumaa, kupiga magoti, kukunja migongo kwa kipindi cha miaka saba. Baada ya hapo tunalalamika kuwa mwanafunzi wa darasa la saba hajui kusoma.
Inasikitisha sana na ni aibu mtu kujitambulisha kuwa ni waziri wa elimu na elimu yenyewe ndio inapatikana hivi kwa kwa mtoto kitanzania.
 
]View attachment 49637

Wazazi kwa Baadhi ya shule tunachangia MADAWATI kila mwaka na bado tatizo haliishi, japo dawati halichakai kwa Mwaka mmoja
Ukibagua miji/mikoa yenye Rasilimali nyingi ndio ipate huduma zote muhimu na kusiko na rasilimali wabaki Tu, Unaimega nchi ktk mafungu ambayo mwisho wake sijui itakuwaje

WIZARA YA ELIMU haija pata kiongozi atakaetoa vipaumbele kwa matatizo tuliyonayo

mkuu umenikumbusha kitu... mimi nilipoingia darasa la kwanza nilienda na Dawati langu....siku hizi huo utaratibu hakuna? cha ajabu nilipomaliza la saba mdogo wangu naye alienda la kwanza na Dawati lake (japo mimi niliacha langu) ....sasa kama system ndo hii na wote tulimaliza tukaacha madawati shuleni uhaba unatokea wapi? kama ni Mwalimu mkuu anatafuna fedha za madawati ina maana wazazi hawawezi kumwajibisha???
 
Back
Top Bottom