The only
JF-Expert Member
- May 19, 2011
- 10,435
- 13,421
huyu kijana anastahili awe mshauri wa CHADEMA yuko vizurMagazeti mengi toka jana hadi leo bado yanaipa uzito habari za kuanguka kwa Sumaye kwa kiwango kisicho cha kawaida. Kupewa uzito huko kwa habari hizo una msukumo wa kimakundi ndani ya ccm. Na mimi sijui ni kundi lipi kati ya makundi hasimu.
Leo mwananchi imekuja na habari za Lowasa kudai kwamba Monduli ni msuli wake wa kisiasa. Kauli hiyo ni dongo kwa Sumaye kwamba yeye hana Msuli wa Kisiasa Hanang na Kwamba nitakushinda 2015. Na hapa analengwa Sumaye na kundi lake aka mtandao wake.
Wote wawili Sumaye na Lowasa hakuna aliyetangaza nia ya kugombea Urais lakini inafahamika wote ama wanautaka Urais ama wanasukumwa na wapambe wao au mitandao yao ili wagombee. Wote pia wanatoka katka makundi makubwa mawili hasimu. Kwa mujibu wa magazeti kadhaa ya Leo Sumaye yuko tayari kupambana na waliomwaga fedha Hanang za kumwangusha yeye iwe ndani ya ccm au nje ya ccm ( mgombea binafsi). Taarifa zilizoenea Hanang ni kwamba Nagu alifadhiliwa na ama kundi la Lowasa au JK.
Mpambano huu sasa unazidi kunoga kufuatia habari zinazoendelea kuvuja ktk magazeti ya leo kuwa Sumaye sasa anataka kuunganisha nguvu na kundi la Sitta ktk kujipanga kwao.
Hiyo ina maanisha kwamba makundi makubwa sasa ni hilo la Lowasa lenye fedha nyingi na likiwahusisha pia wahindi wengi wenye shekeli nyingi.
Kundi la pili ni hilo la Sumaye na (sitta?) na wastaafu wengine akiwepo mkapa ( taarifa isiyo rasmi) ambao sasa wanataka kuunganisha nguvu na Samweli Sitta. Membe na Sitta wanaelewana sijui kama anaunganisha nguvu kwa sitta au anataka ajitegemee bado. Mkapa hana ugomvi na Lowasa lakini hana imani kama atashinda.
Kuna la tatu ni la Mkuu wa Nchi, ambalo linataka kutumia keti ya zamu ya wanawake ( Asha Rose Migiro). Hili ndilo kundi linaloungwa Mkono na wakuu wa wilaya, mikoa wengi na wakurugenzi wote wateule wa JK. Baadhi ya taarifa zinasema JK pia ameahidi kumsapoti Membe huku Membe akiamini kuwa JK anamuunga mkono A. Migiro.
The bottom line is kuna makundi hayo makubwa matatu Sitta/sumaye, Lowasa na Jk + makundi mengine madogo.
Kila kundi linategemea jambo Fulani.
Kundi la Lowasa linategemea sana Pesa wako vigogo kama Rais mstaafu Karume.
Kundi la Sitta linajinadi kwa maadili wapinga ufisadi ( Japo maadili yao yanahojika) Hawana pesa nyingi.
Kundi la Sumaye/sitta ( ambalo linataka kuunganisha nguvu na sitta +sumaye) linategemea majina zaidi. Hapa kuna marais wastaafu akiwepo mkapa, viongozi wa Chama wenye majina makubwa na heshima ndani ya Chama kama akina Mangula. Kuna taarifa pia kuwa Mwandosya na Mwakyembe baada ya uchaguzi huu wa ndani ya Chama wakizidiwa watajiunga na kundi hili.
Kundi kubwa la tatu la JK linategemea mamlaka. Nguvu yao kubwa ni wakuu wa wilaya na mikoa ambao ni wajumbe wa kamati ya siasa wa ngazi zao. Kundi hili pia lina fedha na linauwezo wa kupata fedha kutoka kwa wafanyabiashara wasiotaka matatizo na dola. Hata hivyo, kadri siku zinavyoenda wafanyabiashara wakisoma upepo watawagomea.
Kundi hilo ndilo linatumia vizuri mamlaka yake ndani ya Chama na Serikali na kushinikiza mabadiliko ya katiba ili kushinda. Hapa JK alilenga yafuatayo.
a) Kubadilisha katiba ili kubadili muunda wa kupata wajumbe NEC. Lengo ni kuondoa hawa waliopo ambao wengi ni kundi la Lowasa Hapa anadhibitiwa ni Lowasa zaidi.
b) Wameweka marekebisho ya kuondoa marais wastaafu ndani ya Kamati kuu kwa sababu marais wastaafu wote ( karume, Mkapa na Mwinyi) hawako katka kundi la JK.
Hitimisho.
Kwa kuwa uhasama kati ya makundi haya umefika kiwango cha juu cha kutoa kauli ya kupambana ndani na nje ya chama.(Kauli hii wakati Nyerere inatosha kumwajibisha mhusika) Na,
Kwa kuwa m/kiti wa ccm ameshindwa kabisa kuongoza Chama na kuwa sauti ya Chama kama ilivyokuwa wakati wa Nyerere. Na,
Kwa kuwa, kiwango cha kukataliwa kwa ccm kimezidi kupanda kila kukicha. Na
Kwa kuwa baadhi ya makundi yako tayari chama cha upinzani (chadema) kichukue dola kuliko kundi pinzani ndani ya Chama, Na,
Kwa kuwa, baadhi ya makundi yanafanya mazungumzo yasiyo rasmi na baadhi ya vyama vya siasa ili kuhamia huko mambo yakiwazidia Na,
Kwa kuwa kundi la Lowasa ndilo lenye nafasi kubwa kushida kwa kutegemea nguvu ya fedha huku ikiwa halikubaliki kabisa kwa umma wa watz ambao hawataweza kuwahonga (Pasco wa JF upo?).
Hivyo basi,
Naomba kuhitimisha kwamba;
kama Chadema itamaliza uchaguzi wake wa ndani vizuri mwaka kesho, na
Na kama Chadema watakuwa tayari kumuunga mkono mgombea wao mmoja bila kuvurugana wenyewe ktk kura ya maoni ya ndani mwaka 2015,
Njia ya Chadema kushinda 2015 iwepo katiba mpya au ya zamani ni nyeupe mno. Hii ni kwa sababu, hata kama hakutakuwa na kundi litakalohamia chadema kati ya makundi hasimu (Naamini wako watakaokimbia) hakuna siri itafichika ambalo haitajulikana na Chadema ikiwepo mipango ya kuchakachua kura hakuna ushindi bila uwezo wa kutunza siri.
NB; Nadhani nimepunguza sana ushabiki wa kisiasa na kuweka ukweli mtupu.