NI VIGUMU LAKINI INAWEZEKANA

Galacha Maestro

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
1,353
2,220
NI VIGUMU LAKINI INAWEZEKANA
Kusamehe kuna faida nyingi sana kwa anayesamehe hasa pale unapoamua kusamehe bila hata kuombwa msamaha na kusamehe yale ambayo kibinadamu hayasameheki.
Siwezi kukudanganya kuwa kusamehe ni rahisi na huja automatically, si kweli. Tena kusamehe mtu wa karibu uliyemwamini na kumpenda akakutenda ni ngumu sana kuliko kumsamehe mtu unayefahamiana naye juu juu.
Kusamehe ni uchaguzi, na ni uchaguzi wa kujitoa hasa.
Ni uchaguzi utakaokuweka huru na kukusogeza mbele za Mungu.
Ni uchaguzi utakaosababisha Mungu asikie maombi yako na kukusaidia. Ni uchaguzi ambao wewe mwenyewe ndiwe mwenye uwezo wa kuufanya.
Usikubali watu wakushawishi kutokusamehe, ni wewe unayeumia ndani na sio wao.
Amua kusamehe sasa na anza maisha mapya bila mtu yoyote ambaye hujamsaheme.
Ni ngumu ila Inawezekana!
 
Back
Top Bottom