Ni vigezo gani unatakiwa uwe mavyo ili uwe mwanzilishi na mmiliki wa forum?

Pendaelli

JF-Expert Member
Feb 13, 2014
8,581
22,048
Wakuu salamu kwenu heri na Baraka ziwe juu yenu.

Nimejiwa na wazo la kuwa na forum yenye maudhui ya kitamaduni, ushirikishwaji wa mambo mbali mbali kuhusu jamii fulani,lugha mama frusa , kukutanisha walio mbali. mila, historia na mambo mbali mbali lakini yakilenga jamii fulani hapa Tanzania mf wangoni au warangi au nyasa.

Sasa nilikua naomba kuuliza huwa inagarimu kiasi gani cha fedha, vifaa gani, ujuzi wa namna gani, na sheria za nchi zitaniruhusu?

Elimu yangu ni std 7, kiingereza nakijua kwa mbali kidogo, matumizi ya internet ninayo kiasi jee kwa sifa hizi zangu nakidhi vigezo?

Ni hayo tu wakuu, mujaliwe kila lenye heri.
 
Una wazo jema sana kiongozi. Nakushauri kwanza kabisa ni kuanza.. Jaribu kuonana na wataalam wanaofanya kazi za utengenezaji na usimamizi wa tovuti.. Ili upate maelelzo mazuri.

Uzuri ndani ya JF kuna watu wanaitwa Jamii soft.. Unaweza kutembelea tovuti yao inaitwa jamiisoft.net wakupe ushauri..

Nakutakia mafanikio
Mema
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom