Ni vigezo gani hutumika kuwapata CDF na IGP?

Ni vigezo gani hutumika kuwapata CDF na IGP?

Dogo G

JF-Expert Member
Joined
Jul 6, 2018
Posts
1,052
Reaction score
440
Wadau nadhani kwema,

Nisiende mbali sana,ninajua humu kuna ambao wana ufahamu na hizi mamlaka za hawa wakuu wa vyombo vya usalama kama vile Jeshi,Polisi,magereza,uhamiaji lakini hususani Jeshi la wananchi na Police kwa kuwa vinachukua mamlaka kwa kiasi kikubwa na hata uapisho wa wakuu wake hutrend sana kijamii.

Je,wanapatikana vipi hawa?,Ili kamanda wa jeshi(senior)ateuliwe kuwa mkuu wa majeshi awe amepitia sifa zipi?,je awe amepigana vita angalau moja au awe amefuzu fani gani?.Na je,ili kamanda wa polisi(kamishna) ateuliwe kuwa IGP awe na sifa gani au amesomea mambo gani? Maana kuna kile kipindi ambacho Ernest Mangu aliteuliwa kuwa IGP nikasikia juu juu kuwa kuna kamanda ilibidi awekwe badala ya Mangu ila hakupitia CCP sijui sasa sijaelewa hapa inawezekana mtu depo akapitia nchi nyingine na kukubaliwa kuwa askari wa nchi nyingine.

Kumekucha
FB_IMG_15515883742910512.jpeg
FB_IMG_15517158908015595.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Apart from proffesional qualifications ni lazima Awe karibu sana na system (Hatuwezi kuweka mamluki) hata kama ana cheo kidogo atapandishwa fasta ili akidhi cheo cha kuwa mkubwa!!
 
Awe amefuzu mafunzo ya uongozi kijeshi (military and armed combating) na awe commissioned na Rais.
 
Wadau nadhani kwema,

Nisiende mbali sana,ninajua humu kuna ambao wana ufahamu na hizi mamlaka za hawa wakuu wa vyombo vya usalama kama vile Jeshi,Polisi,magereza,uhamiaji lakini hususani Jeshi la wananchi na Police kwa kuwa vinachukua mamlaka kwa kiasi kikubwa na hata uapisho wa wakuu wake hutrend sana kijamii.

Je,wanapatikana vipi hawa?,Ili kamanda wa jeshi(senior)ateuliwe kuwa mkuu wa majeshi awe amepitia sifa zipi?,je awe amepigana vita angalau moja au awe amefuzu fani gani?.Na je,ili kamanda wa polisi(kamishna) ateuliwe kuwa IGP awe na sifa gani au amesomea mambo gani? Maana kuna kile kipindi ambacho Ernest Mangu aliteuliwa kuwa IGP nikasikia juu juu kuwa kuna kamanda ilibidi awekwe badala ya Mangu ila hakupitia CCP sijui sasa sijaelewa hapa inawezekana mtu depo akapitia nchi nyingine na kukubaliwa kuwa askari wa nchi nyingine.

KumekuchaView attachment 1037979View attachment 1037980

Sent using Jamii Forums mobile app
Awe member Wa vyombo hivyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nafikiri kuna vigezo stahili kwa hizo nafasi za juu za utumishi katika vyombo vya Ulinzi na Usalama..

Ila kwa awamu hii, la kwanza na la muhimu kuliko yote ni wewe mwenyeji wa kanda gani..

Wa Lake Zone ni first priority.
 
Kwa U 'CDF' Nadhani cha kwanza ni lazima awe Jenerali sababu ukisema uteue chini ya majenerali Kuna makanali(Full colonel) hawajamaliza Kozi zote zinazotakiwa kusomwa lakini mameja jenerali wote wameshamaliza mafunzo yote yanayotakiwa na kwa Brigadiers ni kwamba most of them wameshamaliza mafunzo yote

Cha pili: kwa CDF akiteuliwa chini ya vyeo vya ujenerali litaleta manun'uniko kuwa mteuaji amewadharau au ameruka Seniority kwa sababu Kanali au chini yake hana hadhi sawa na mtu alie kwenye ujenerali So mteuaji akiwaruka Generals akateua mtu kutoka vyeo vya chini ya Cadre ya U'General' itakuwa kama amewaonea kwa kuruka seniority majenerali, na ndio maana nchi yetu ma'CDF' wote wametokea kwenye Ujenerali ndio wakapata U'CDF'

Jenerali Waitara ndio peke yake alitokea kwenye UBrigedia mpaka post ya U'CDF' ila wengine wote naowajua walitokea kwenye Umeja-jenerali
 
Back
Top Bottom