Hii bei imepanda kwa asilimia zaidi ya 100%,toka tsh 900 hadi 2100 kwa kisingizio cha kuzuia uchakachuaji wa petrol na diesel,sasa hawa wananchi wa vijijini wanaotumia kerosine kwa ajili ya vikoroboi,ndo wanaochakachua?,hivi mnajua watumiaji wakubwa wa Kerosine ni watu wa vijijini na wa kima cha chini sana?,huku mijini tunatumia Gas,Majenereta,Taa za kichina za betri na za kuchaji,Solar na Tanesco.Kwa hali hiyo,haki ya Mungu,mmewaadhibu watu wasio na hatia.Mi najua kuna mashine za kupima mafuta yaliyo chakachuliwa,kweli mmeshindwa kuandaa utaatibu wa kuyapima mafuta kila siku katika vituo vya mafuta na kutoa adhabu kwa wenye hatia?,Mbona BP juzi mmewaletea noma?,mi nadhani mmedhalia kutumaliza kabisa,mmetutafuna mjini,sasa mmehamia vijijini.wachakachuaji wakigungua kuchakachua kwa kutumia mikojo ya bia,nadhani mtapandisha kodi ya bia na tununue mara mbili ya bei ya sasa,bia moja kuanzia elfu 3000,mko juu wasomi wetu wa WEHu Ra,Wehu kasisa,hope less kabisa.