Bei ya Gesi ya kupikia juu, Mafuta taa juu, watu watapikia mkaa, miti kuisha, ukame na njaa

MPadmire

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,931
3,227
Tanzania kama nchi tumekosa mwelekeo

Tunasema Kilimo kwanza, tunategemea mvua, miti tunakata kwa ajili ya mkaa.....Sasa watu wapikie nini wakati uwezo wao ni kuni na mkaa!

Nishati mbadala ya kupikia ni Gesi na mafuta taa..

Sasa Mh. Mkuya, Mh. Mwigulu, Malima na Boss Wao JK, wameamua kupandisha bei za Nishati ili kupata vijisenti vya leo, wanasahau kesho

Mafuta taa yamepanda bei kuliko hata diesel

Watu wa vijijini wanaumia sana jamani

Hii bei ya mafuta taa ndo kete ya kuwaondoa CCM madarakani maana wanategemea kura za vijijini

Kwanza bei ya umeme ni juu sana, hata ukiwekewa umeme nyumbani bure, lakini bei ya unit za luku ni ghali sana....huwezi kupikia..... Mkaa lazima utumike maana gesi na mafuta taa bei juu.
 
Ni kitu cha kushangaza sana kuona watu tunalalamikia kupanda kwa gharama za mafuta ya vyombo vya moto ilihali tulikua tunajua kua serikali ilishatangaza kwamba kuanzia tar 01/07/2015 ambao ni mwaka mpya wa bajeti kwamba kutakua na ongezeko la bei! Kulishindwa vipi kulilalamikia hili toka mwanzo kabla ya tar 01/07?
Kwanini tulishindwa kilishikia hili mabango hata kabla halijaingia July? Yaani tunakua walalamikaji tuu hatufanyi maamuzi?
Hata baada ya Uchaguzi mkuu itakua hivi hivi tu kama kawaida yetu, Tutachagua mwenyewe na tutalalamika mwenyewe.
 
Watanzania ndo tulivyo si watu kuchukua maamuzi,yaan tunalalamika tu baasi...nnch nyingine watu wangeshaandamana zaman.hakuna nch rais kuiongoza kama tanzania dunian...kwa sababu watu wengi wanalalamika hawatake action...
 
Kama taifa tunahitaji kutunza mazingira yetu kwa vitendo. Kitendo cha kuongeza bei ya gesi na mafuta ya taa kitapelekea wanajamii kukimbilia kwenye kuni na mkaa kama nishati, hivyo kuongeza kasi ya uteketezaji wa misitu.
 
Ni utahira kuendelea kuikumbatia ccm octoba! Tanganyika itabakia kapi! Inatakiwa tuwafukuze hawa jamaa na magaga yao magumu!
 
Ni kitu cha kushangaza sana kuona watu tunalalamikia kupanda kwa gharama za mafuta ya vyombo vya moto ilihali tulikua tunajua kua serikali ilishatangaza kwamba kuanzia tar 01/07/2015 ambao ni mwaka mpya wa bajeti kwamba kutakua na ongezeko la bei! Kulishindwa vipi kulilalamikia hili toka mwanzo kabla ya tar 01/07?
Kwanini tulishindwa kilishikia hili mabango hata kabla halijaingia July? Yaani tunakua walalamikaji tuu hatufanyi maamuzi?
Hata baada ya Uchaguzi mkuu itakua hivi hivi tu kama kawaida yetu, Tutachagua mwenyewe na tutalalamika mwenyewe.

Tanzania ni kichwa cha wendawazimu nukuu Ndg Alhassan Mwinyi.
 
Serikali hai angalia afadhari kipindi hiki ndio ungefanya isha bora.ila wao wako vizuri na wanakuja sasa hivi wanatudanganya nasi tunatongozeka tunawapa kura pumbavu kweli
 
Trafic wa check point mali asili pale kibaha itabidi waongezeke kwa sababu malori na fuso usiku wa manane na magunia ya mikaa kuingia mjini. Yataongezeka
 
Hilo ndilo hitimisho la JK la "MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA!" Mwisho wa miaka yake kumi ya utawala, maisha ni magumu kwa kila Mtanzania kuliko miaka kumi iliyopita!
 
Bajeti hii , ni hukumu ya kifo kwa CCM .
Umesema kweli mkuu, bajeti hii ni kitanzi kwa CCM kwenye uchaguzi mkuu mwezi Oktoba mwaka huu.

Pia hata Katibu Mkuu wa Chama chao Abdrahman Kinana amelitamka waziwazi kwenye hotuba yake na wananchi kule Mwanza majuzi, aliposema kuwa anakerwa mno na kitendo cha wabunge wa Chama chake kupitisha jambo lolote linaloletwa bungeni na serikali hata likiwa baya la kupindukia.

Kwa tafsiri nyingine ni kama vile Kinana ametoa credit 'indirectly' kwa utendaji kazi wa wabunge wa upinzani.

Kauli hiyo ya Katibu Mkuu wa Chama tawala cha CCM itakuwa ni 'neema' kubwa sana kwa Ukawa kwa kuweza kupata ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi mkuu mwezi Oktoba mwaka huu.
 
OKoa mazingira, amka kajiandikishe upige kura.

Wao wameiba kodi zetu, hawajali wananchi.

jamani hata mafuta taaa?? Shame on them.

Hili la mafuta taa linagusa wizara 4.... Wizara ya maliasili, wizara ya mazingira/makamu wa raisi, wizara ya kilimo na wizara ya elimu. Shule za kata huko vijijini wanafunzi watajisome kweli?

Je Hawa mawaziri woote 4 na Makamu wa raisi kabisa hawakuona impact ya kupandisha bei ya mafuta taa??

Gesi nayo imependa.... Duuuu

NEMC nayo mko wapi

Wanaharakati tokeni semeni kuhusu shule za kata......
 
Miswada ya kuwauza watanzania miaka 100 ijayo..

Tukatae ukoloni Mamboleo

Tuna deni kubwa ajabu, tutalipa miaka 50 ijayo

Bado kodi zinapigwa mpaka kwenye mafuta taa... masikini mkulima wa kijijini

Shule za kata, wanafunzi watasomaje...

referrrrrr

Wafanyakazi wanasema eti mishahara ni midogo.....

Wakulima na wafugaji wamepandishiwa bei ya mafuta taa...

Maandamano Mikoa yote... Yaanzie Dodoma, yaende Dar, Mtwara na Lindi, Mwanza

Watanzania tuamke.... Tuendako ni kubaya.... Hawa Madikteta na mafisadi yatakuja kutunyang'anya hata waume ama wake zetu..

Watetezi wetu UKAWA wanatolewa Bungeni halafu tumekaa kimya wananchi..

Ndio Maaana wanafanya ufisadi mchana kweupe na wanarudia tena, Watanzania tunasahau, wanarudia tena..

EPA, Ikaja RICHMOND, IKAJA ESCROW..... na bado.....


Watanzania Tunauzwa.... Miswada ya kutuuza miaka 100 ijayo..

Deni la Taifa Tanzania limekuwa... Tutalipa miaka 50 ijayo

Kodi wanatukamua mpaka mafuta taaa, aargh

Jumatatu ASB... hakuna Dala dala kutembea, hakuna wafanyakazi kwenda kazini, Maduka yote yafungwe....

Jamani, hata kama kwa simu tumeshindwa (sheria) basi kwa Facebook jee, Kwa Twitter je.

Tunashindwa hata na Burundi...

Wakenya walipeleka Damu ya Nguruwe bungeni..... Wakenya wanatucheka....

Watanzania tujitoleee.....
 
bei ya mafuta soko la dunia ni bei chini sana....

kenya mafuta bei chini..kwa nini Tanzania bei iwe juu

Mgombea wa ccm....punguza bei ya mafuta

Wakati baraza la waziri..magufuli yupo..magufuli alikubali watanzania wapigwe bei juu

Nishati mbadala ya kupikia ni Gesi na mafuta taa..

Sasa Mh. Mkuya, Mh. Mwigulu, Malima na Boss Wao JK, wameamua kupandisha bei za Nishati ili kupata vijisenti vya leo. Baraza la mawaziri yupo pia Magufuli...

Mafuta taa yamepanda bei kuliko hata diesel
 
Back
Top Bottom