Ni uwendawazimu kupandisha bei ya mafuta ya taa, maji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni uwendawazimu kupandisha bei ya mafuta ya taa, maji

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bajabiri, Jun 23, 2011.

 1. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #1
  Jun 23, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Serikali imeongeza kodi kwenye bidhaa ya mafuta ya taaa,kwakuwa ndio yanayotumika kuchakachulia mafuta......
  Hayo yalisemwa jana bungeni........mheshimiwa CHENGE aliunga mkono hoja hiyo......
  Serikali imesema imefanya hivyo ili kuongeza mapato na kufuta utaratibu wa kuchakchua......mafuta

  My take:je tumekosa njia nyingine ya kudhibiti uchakchuaji wa mafuta hadi yapandishiwe kodi????kwani mafuta ya taa nadhan ndiyo yanatumiwa na sehemu kubwa ya watanzania.....hawa watendaj wa wizara ya fedha wana nia ya dhat ya kumuondolea mzigo mtanzania????nachojua watu wa vijijin wanategemea mafuta ya taa.....mbona hivi jamani????yaani njia sahihi ya kuondoa uchakachuaji ni hiyo tuuu
   
 2. m

  marco thomas Member

  #2
  Jun 23, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Nimekulia kijijini, sikuwahi ni sijawahi kutumia nishati ya umeme kijijini kwetu. Nimekuwa nikitumia Kuni au mkaa kupikia. Hutumia mafuta ya TAA kupata mwanga wakati wa Usiku. Sasa mafuta yanapanda bei mara saba (kodi), Kipato kinapungua. Nifanye nini nipate wa kunitetea?
   
 3. MWAKIGOBE

  MWAKIGOBE Member

  #3
  Jun 23, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 65
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jamani hivi hawa walio pandisha kodi kwenue mafuta yataa kama suluhisho la tatizo la uchakachuaji wa mafuta ya petrol, hawajui wanawamaliza kabisa wananchi wa vijijini ambao tanesco yao ni mafuta ya taa? mi nadhani wangeshusha kodi kwenye petrol na disel, na sio kuwamaliza kabisa watu wa vijijini kwa kupandisha bei ya mafuta ya taa, jamani hatutadika!
   
 4. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #4
  Jun 23, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,921
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  TFDA, EWURA, SUMATRA, NGELEJA, CHENGE wajiuzuru,wawafilisiwe na wanyongwe hadi kufa...wameshiba, wamesahau watanzania wenye njaa!! Watanzania tupo zaidi ya mil 40+, wachakachuaji hata 1000 hawafiki...mamlaka za udhibiti zipo wapi??wanafanya nini??
  Ngoja nikuchallenge....hivi kuna mtanzania yoyote ambaye hajawahi kutumia mafuta ya taa?? Nishati ya umeme imefika huko vijijini?? Bei ya diesel ifike 1500 na mafuta iwe hivyo nani ataweza??wanafunzi wanatumia vibatari kujisomea watatoka kwa bei hiyo??
  Sasa Mtetezi wa wananchi mjengoni anaitwa muuza sura anataka kuonekana kwenye TV...Werema umevimbiwa!!
   
 5. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #5
  Jun 23, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Wanasiasa wetu wengi ni wabinafsi na wavivu wa kufikiri. Siamini kama kweli serikali imeshindwa kudhibiti suala la uchakachuaji kiasi cha kukimbilia kupandisha bei ya mafuta ya taa kama suluhisho.
   
 6. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #6
  Jun 23, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Sijui pale bungen watu wa kupinga kwa nguvu walishindikana??????bajet inayosemwa ya kumkomboa mtz iko wapi yailah
   
 7. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #7
  Jun 23, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hapa wanajimaliza wenyewe! Nani atawapigia kura tena 2015 kama na huko vijijini ndo wanawatendea hivi ilihali hujidai kuwa kura zao ni za masikini na wajinga?

  Kweli siku ya kufa nyani miti yote huteleza, sasa ccm wataponea wapi jamani?

  Wamelogwa hawa na aliyewaloga kashakufa!
   
 8. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #8
  Jun 23, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Waliopandisha kodi(=bei) ya mafuta ya taa hawa hawayatumii, wananufaika na mgao wa wachakachuaji.
   
 9. Donnie Charlie

  Donnie Charlie JF-Expert Member

  #9
  Jun 23, 2011
  Joined: Sep 16, 2009
  Messages: 6,575
  Likes Received: 842
  Trophy Points: 280
  ktk maamuzi mabaya kabisa yaliyowahi kufanywa na serikaki hii ya awamu ya nne hili ni mojawapo
   
 10. Makucha

  Makucha JF-Expert Member

  #10
  Jun 23, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 255
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mafuta ya taa ni nishati muhimu sana vijijini. serikali kama Serikali itashindwaje kudhibiti uchakachuaji wa mafuta kutumia mafuta ya taa? Vituo viko wazi na shughuli inaendela wazi wazi. Wakikagua wanawabaini wazi wazi lakini kwa kuwa tuamini ndio wakubwa wenyewe wanaohusika nani achukue hatua. EWURA ipo, Serikali ipo, Police ipo, Mahakama zipo lakini matatizo haya yanendelea. Kupandisha bei ya kerosine ni kuhamisha watakachokikosa wakiacha kuchakachua wanakipata kupitia bei kubwa ya kerosine. Watumiaji tunaumia tu, wapi haki na serikali ipo wapi kutulinda. Tajiri hatumii kerosine, masikini ndiye anayetumia kerosine.

  Sheria ni hii duniani kote inafanya kazi kwa ufanisi mkubwa: Correct me:
  YEYOTE AKIJUA KWAMBA AKIVUNJA SHERIA (atachakachua mafuta) HATAJULIKANA NA HATA AKIJULIKANA HATAPA ADHABU YA KUOGOFYA, ATAVUNJA SHERIA (Hata awe binadamu mkiristu au muislamu wa namna gani).
  Kwa hili siwasamehi serikali, ninailaumu sana ila sina la kufanya tuumie tu wa vijijini ila tajiri mijini waendelee kuneemeka.
   
 11. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #11
  Jun 23, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  vipi kaka, ulikuwa unawahi lecture nini?
   
 12. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #12
  Jun 23, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  Kwa mara ya kwanza hilo wazo lilitolewa na Mwakyembe, hakuna wanachofikiri hawa zaidi ya matumbo yao, alafu siyo vijijini tu hata hapa mjini wengi wnayatumia katika kupika.
   
 13. K

  Kamura JF-Expert Member

  #13
  Jun 23, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 488
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nimesikitika kusikia kwamba Bunge linaombwa kuridhia kupandisha bei ya mafuta ya taa na maji ya kunywa ya chupa. Mafuta ya taa ndio nishati tegemezi ya kupikia na mbadala wa umeme kwa Watanzania wanaoishi vijijini, leo wanataka ipande ilingane bei na dizeli kwa sababu watu wameshindwa kufanya kazi yao ya kudhibiti uchakachuaji wa mafuta na huku wanakula mishahara minono ya wavuja jasho haohao. Maji ya chupa sasa yanaonekana anasa wakati yanasaidia kweli. Hivi wanataka watu watembee na mitungi kwenye mabasi au treni wanaposafiri au wanywe maji kwenye madimbwi ili wahare na kupata magonjwa mengine ya mlipuko? sioni mantiki ya hoja ya kupandisha bei kwenye bidhaa hizo muhimu.
   
 14. m

  mwelimishaji Member

  #14
  Jun 23, 2011
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bei za bidhaa muhimu zinapopanda mara zote inakuwa mzigo kwa mwananchi wa tabaka la kati na la chini. Walio juu hufurahia kwani wanapata furaha wanapoona mwanya mkubwa kati yao na wasionacho. Ni vizuri wananchi wanaonyonywa na tabaka la juu wajue kuwa hawakuiweka serikali madarakani ili iwatetee wanyonge bali iwanyonge kidogo kidogo mpaka watakapoamua kubadili mwelekeo.
   
 15. K

  Kamura JF-Expert Member

  #15
  Jun 23, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 488
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Huo ubinafsi utawaumiza na hukumu yake ni mbaya kwa sababu huwezi kumpandishia mwananchi bei ya mafuta ya taa wakati umemmnyima umeme na wewe umejipa umeme usio na mgao na unapikia gesi na nishati nyinginezo. Uliyemnyima maji anajaribu kutafuta ya chupa naye unataka asinywe ya chupa ili aendelee kunywa machafu!
   
 16. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #16
  Jun 23, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,060
  Likes Received: 6,508
  Trophy Points: 280
  Wanapowakamata wanapewa rushwa na wanawafungulia tena station zao na chakachua ndo linazidi.
   
 17. mkonowapaka

  mkonowapaka JF-Expert Member

  #17
  Jun 29, 2011
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 1,483
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Nimesoma kwa masikitiko makubwa mojawapo ya magazeti ya leo kuwa kodi ya mafuta ya taa itapanda toka toka sh 52 hadi kufikia sh 400 kwa lita hivyo wamachi watarajie kununua lita moja kwa wastani wa shilingi 1900 sawa na bei ya petroli,

  sababu hasa ya kupandishwa ni kuzuia uchakachuaji wa diesel unaofanywa na baadhi ya wafanyabiashara!

  my take: kweli uyu mtu wa ewura hapo ndio mwisho wake wa kufikiria namna ya kuwabana watu hao...

  Amejaribu hata kuwaza ni watanzania wangapi wanatumia mafuta hayo pengine kuliko hata watumiaji wa dieasel yenyewe? HIVI kweli ni akili hii...........nakuuliza wewe mtu wa ewura na hali hii ya uchumi kuwa ngumu,hatuna umeme tunategemea mafuta hayo umetafakari vyema kweli?

  hivi tunaelekea wapi jamani...tutaendelea kulia hivi hadi lini,....lini tutaingia barabarani....naona bado freedom ipo mbali sana!!

  nimeandika kwa uchungu nikiwaza wazazi wangu kule kijijin wanotegemea mafuta hayo kwa taa na kajiko ka mchina ....omg
   
 18. Pota

  Pota JF-Expert Member

  #18
  Jun 29, 2011
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 1,813
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  hivi ina leta mantiki kweli? kisa mfanyabiashara anachakachua petrol then unapandisha bei
  ya kerosene? hapa c kumwadhibu mkulima kijijini? je ewura wameshindwa kumuwajibisha
  huyo mfanyabiashara? shameful apon ewura
   
 19. mikonomiwili

  mikonomiwili JF-Expert Member

  #19
  Jun 29, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 274
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kwakifupi hatuna serikali inayo wajali wananchi wake . Natatizo kubwa ni hili lakuogopana hakuna anaye weza kumchukulia hatua mwezanake kwani hao watu wanao chakachua mafuta wana julikana kwani walisha wahi hata kuweka kwenye gari ya raisi na hatukisikia kilichoendelea .
  Huu ni uvivu waku solve problem wana fikiria simple solution. Na huaga hawafikirii impact yake kwenye jamii . mtu alikua ana nunua mafuta shilingi elfumoja sasa akanunue elfumbili wakati nikitu kinge faa kuthibiti kama wangekua serious.

  anyway wanajichimbia kaburi wenyewe na hili na laumeme ndilo litawaondoa. hivi najiuliza Tanzania Tumelogwa ama kunanini watu hatufikirii na hatutaki kufanya kazi kabisa .Iposiku tutaamka Mungu ibariki Tanzania ,Mungu wabariki watu watanzania ili watoke usingizini waliko
   
 20. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #20
  Jun 29, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  MHHHH %%%%zenu%%%$#JK%%#KABUNGE$$$ mimi ndo maana naishia kutukana tuuu!
   
Loading...