Ni usahaulifu au uzembe? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni usahaulifu au uzembe?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kidudu Mtu, Nov 25, 2009.

 1. Kidudu Mtu

  Kidudu Mtu Member

  #1
  Nov 25, 2009
  Joined: Nov 7, 2009
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwanafunzi aliyesahauliwa na serikali afariki

  • Alitakiwa kwenda India tangu mwaka 2006

  FAIDA Kyando (18), mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari ya Itigi, mkoani Mbeya, aliyekuwa akisumbuliwa na tundu kwenye moyo kwa zaidi ya miaka 10 na kushindwa kutibiwa kwa msaada wa serikali tangu mwaka 2006 baada ya kukamilisha taratibu zote za kwenda India kushindikana, amefariki dunia.


  Kifo cha binti huyo aliyegunduliwa kwa mara ya kwanza akiwa na tatizo la moyo na kuanza kutibiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya na baadaye kutakiwa akatibiwe nje, kimeacha majonzi siku chache baada ya madaktari bingwa waliokuwa na mkutano wao wa sita hapa nchini kumpokea kwa ajili ya kumfanyia uchunguzi.


  Uchunguzi wa mwanafunzi huyo uliokuwa ufanywe na madaktari hao na kisha taratibu za upasuaji zifanywe katika Taasisi ya Magonjwa ya Moyo hapa nchini (THI), hawakuweza kufanikisha upasuaji huo baada ya mgonjwa huyo kukumbwa na kiharusi kilichompata muda mfupi kabla ya kufanyiwa upasuaji.


  Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Dk. Ferdinand Masau, aliiambia Tanzania Daima Jumatano jana kuwa mwanafunzi huyo alifariki dunia Jumamosi iliyopita na tayari mwili wake umesafirishwa kwa ajili ya maziko yatakayofanyika kijijini kwao Wilaya ya Makete.


  Kifo cha binti huyo aliyekuwa na matumaini ya kuishi kimeacha doa kwa serikali na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, kwani baada ya kugundua tatizo la binti huyo mkiwa, iliweza kuwapa matumaini makubwa ndugu zake waliojiandaa kwa kila kitu ili mtoto wao akatibiwe nje na kujaza taarifa zote zilizohitajika, mwisho wake ni mauti kwa mwanafunzi huyo.


  Hali ya mwanafunzi huyo ambaye sasa ni marehemu ilisababisha babu wa mtoto huyo afike kwenye ofisi za Tanzania Daima mkoani Mbeya ambako taarifa zake zilipopokewa zilimfanya, Mkurugenzi wa THI, Dk. Masau, akubali kumtibu bure kwa kushirikiana na madaktari bingwa kutoka nchi mbalimbali.
  “Huyu binti tulimpokea vizuri akiwa amedhoofu, tulianza kumfanyia uchunguzi lakini kwa bahati mbaya alipata ‘stroke’ na alifariki dunia siku ya Jumamosi, hiyo ndiyo taarifa ya huzuni tuliyoipata, tulikuwa na nia njema ya kuokoa maisha ya binti yetu, lakini Mungu amempenda zaidi,” alisema Dk. Masau.


  Tanzania Daima Jumatano ilifanikiwa kupata nakala ya barua ya mwisho iliyoandikwa na Wizara ya Afya, Januari 24 mwaka 2005, ikikiri kupokea barua ya Kyando ya Januari 5 mwaka 2005, iliyosainiwa na Dk. Sawe kwa niaba ya katibu mkuu, ikielezea matibabu ya Faida Kyando nchini India.
  Kyando alisema, Faida alipatiwa hati ya kusafiria namba AB086918 iliyotolewa Desemba 3, mwaka 2006, baada ya kukamilisha uchunguzi wa vipimo vyote na chanjo ya ugonjwa wa manjano kama alivyoagizwa na Wizara ya Afya, lakini hakuna safari ya nje ya upasuaji aliyopangiwa mwanafunzi huyo hadi alipokutwa na mauti.
   
 2. Serendipity

  Serendipity JF-Expert Member

  #2
  Nov 26, 2009
  Joined: Jan 24, 2009
  Messages: 475
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Ni uzembe wa hali ya juu kwa watendaji wa wizara ya Afya. Je kama binti huyu angekuwa na ndugu pale wizara ya Afya unafikiri haya yote yangemkuta?
  Any away, RIP Faida.
   
 3. Annina

  Annina JF-Expert Member

  #3
  Nov 26, 2009
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 437
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  So sad, watu wanaweza kucheza na maisha ya mtu kiasi hiki? halafu bado tunajisifu ni nchi ya amani na utulivu!Kuna amani kweli kwa ndugu wa binti huyu?

  RIP Faida
   
 4. M

  Msindima JF-Expert Member

  #4
  Nov 26, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mmmh hii nchi jamani sijui hata tunaelekea wapi? sasa kama taratibu zote zilifanyika nini kilizuia asipelekwe India? Anyway wafiwa poleni.
   
 5. afkombo

  afkombo Member

  #5
  Nov 26, 2009
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 93
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Lawama kwa Wizara Ya Afya kwa kuchelewesha kumpeleka Mtoto Mahali palipostahili Kwa ajili ya Matibabu Lazima iwepo lakini Pia kwa Upande mwingine Ingependeza Kama wangepatikana wachunguzi kuangalia chanzo halisi cha kifo chake maana kilitokea akiwa Hospitali akiwa ameshafikishwa kwenye mikono ya Wataalam,sasa"stroke" tena mmmh haya!!Naamini kwa kuangalia History Ya Ugonjwa wa huyo Mtoto wangeweza kum-monitor vizuri tu na hayo yote yasingetokea lkn ndiyo hivyo tena Watanzania tunaamini Mungu"Siku yake ilifika,so hakuna jinsi "Mungu amempenda zaidi" "
   
 6. a

  alibaba Senior Member

  #6
  Nov 26, 2009
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 185
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wande,
  Kwanza kabisa Mola amweke mahali pema mwanetu Faida (marehemu) na Pili awape nguvu na subira Wazazi wake na wote walio katika familia yake, bila kuwasahau jamaa na marafiki zake aliokuwa nao Shuleni. Baada ya hayo napenda nikubakiane na wewe kuwa Upo uwezekano mkubwa kama Marehemu Faida angekuwa na Mjomba au Shangazi katika Wizara husika au mwenye ngazi yeyote ya juu serekalini au CCM basi isingechukua miaka MINNE na zaidi, ufumbuzi ungepatikana sana sana ndani ya miezi sita. Nitawatetea sana Madaktari kwa kujua wanavyofanya kazi katika Mazingira Magumu, ya Upungufu wa NYENZO na VIFAA vya KAZI kabla hujaangalia MISHAHARA yao. Faida, Madaktari na Wauguzi Wote wamo katika Kapu moja la kusalitiwa na CCM na SEREKALI yake. Watanzania tunatakiwa tutafute Mbinu ya kuondokana na haya tena itafutwe haraka sana.
   
Loading...