Ni upi utaratibu mzuri wa kula matunda?


ng'wanankamba

ng'wanankamba

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2010
Messages
349
Points
225
ng'wanankamba

ng'wanankamba

JF-Expert Member
Joined Dec 15, 2010
349 225
Wadau, naomba mwenye uelewa juu ya utaratibu mzuri wa kula kula matunda anisaidie. Nilishawahi kuambiwa kuwa si vizuri kula matunda mara baada ya kumaliza kula chakula kwani yanasababisha fermentation. Na je nikitaka kula matunda kama mlo, nile matunda ya aina moja tu kama vile papai, n.k na mlo mwingine niletikiti maji au nile mchanganyiko wa matunda mbalimbali?
 
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
40,095
Points
2,000
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
40,095 2,000
Faida ya juice za matunda mchanganyiko kama tiba ya mwili wa binadamu

Katika ulimwengu wa vyakula, inafahamika na kuaminika kuwa chakula ni dawa. Chakula unachokula leo ndicho kinachoamua hali yako ya kiafya kesho. Unaweza kuishi bila kuugua kama ukila vyakula vyote muhimu vinavyohitajika mwilini.

Leo nitakutajia orodha ya juisi zilizotengenezwa kwa matunda na mboga na fadia zake mwilini. Katika orodha hii, utaona kuna mchanganyiko wa matunda au mboga mbili hadi nne na kazi zake mwilini, zikitumika kama tiba au kinga ya magonjwa.

KAROTI, TANGAWIZI NA TUFAHA
Juisi yenye mchanganyiko wa matunda hayo matatu huondoa sumu mwilini na kuimarisha mfumo wa kinga ya mwili. Tufaha ndiyo apple kwa Kiingereza.

TUFAHA, TANGO NA FIGILI
Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya ni kinga dhidi ya saratani, huondoa lehemu (cholestrol) mwilini, husafisha tumbo na pia huondoa maumivu ya kichwa.

NYANYA, KAROTI NA TUFAHA
Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya hufanya ngozi ya mwili mzima kuwa nyororo na huondoa harufu mbaya mdomoni.
TANGO CHUNGU,
TUFAHA NA TANGO LA KAWAIDA
Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya huondoa harufu mbaya mdomoni na hupunguza joto la mwili.

CHUNGWA, TANGAWIZI NA TANGO
Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya hung'arisha rangi ya ngozi na kuifanya kuwa laini. Pia hupunguza joto la mwili. Kwa wale wenye matatizo ya kuwa na ngozi kavu, juisi hii itawasaidia sana.

NANASI, TUFAHA NA TIKITIMAJI
Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya hufanya kazi ya kuondoa chumvi nyingi mwilini, husafisha kibofu cha mkojo na figo. Juisi hii ni nzuri kwa wale wenye matatizo ya kibofu na figo au wanaotaka kujikinga na magonjwa hayo.

TUFAHA, TANGO NA ‘KIWI'
Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya hung'arisha rangi ya ngozi. Kiwi ni aina ya matunda ambayo hujulikana pia kama ‘matunda-damu'.

PEASI NA NDIZI

Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya hurekebisha kiwango cha sukari katika damu. Inawafaa sana wagonjwa wa kisukari na inaweza kuwa sawa na kinga dhidi ya ugonjwa huo.

KAROTI, PEASI, TUFAHA NA EMBE
Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya huzuia athari ya sumu mwilini, hupunguza shinikizo la damu na kuondoa mlundikano wa uchafu mwilini.

MASEGA YA ASALI, ZABIBU, TIKITIMAJI NA MAZIWA
Juisi yenye mchanganyiko huu huwa na kiasi kikubwa cha Vitamin C na Vitamin B2 ambazo huimarisha chembechembe hai na kinga ya mwili.

PAPAI, NANASI NA MAZIWA
Juisi hii ina kiwango kikubwa cha Vitamin C, E na madini chuma. Huimarisha rangi ya ngozi na mfumo wa usagaji wa chakula tumboni.
NDIZI, NANASI NA MAZIWA

Juisi hii yenye kiasi kikubwa cha vitamini na virutubisho mbalimbali vyenye faida mwilini, huzuia tatizo la ukosefu wa choo.

Ili kupata faida hizo zilizoainishwa katika kundi la matunda hayo, usafi wa matunda yenyewe hauna budi kuzingatiwa wakati wa kutayarisha juisi yake. Vilevile hakikisha unatumia matunda yaliyoiva vizuri na uyatayarishe kwa kuzingatia kanuni ya ‘mtu ni afya'.

Unaweza kutumia mashine maalumu ya kukamulia matunda (blender) au kutumia njia ya asili ya kutwanga kwa kinu maalumu na kupata juisi hiyo. Kama utaongeza sukari, inashauriwa kuweka kiasi kidogo sana. Ni bora zaidi usipoweka sukari, kwa sababu matunda mengi yana sukari ya asili.

chanzo: https://www.jamiiforums.com/jf-doctor/190306-faida-ya-juice-za-matunda-mchanganyiko-kama-tiba-ya-mwili-wa-binadamu-2.html

:Ushauri wangu: Pendelea kula Matunda kabla ya kula chakula itakuwa ni jambo zuri sana kiafya yako.

copyright:MziziMkavu
 
S

sokoinei

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2012
Messages
1,835
Points
0
S

sokoinei

JF-Expert Member
Joined Feb 27, 2012
1,835 0
Nimekubali ntaanza mara moja kua na ratiba ya matunda,ngoja tukubali kua wanyama,ni mboga za majan na matunda hapa kwangu up now
 
King Kong III

King Kong III

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2010
Messages
33,240
Points
2,000
King Kong III

King Kong III

JF-Expert Member
Joined Oct 15, 2010
33,240 2,000
Thanks MziziMkavu kwa shule Tosha.
 
Last edited by a moderator:
ng'wanankamba

ng'wanankamba

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2010
Messages
349
Points
225
ng'wanankamba

ng'wanankamba

JF-Expert Member
Joined Dec 15, 2010
349 225
Asante sana Mkuu MziziMkavu, ubarikiwe.
 
K

Karibuni masijala

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2012
Messages
409
Points
0
K

Karibuni masijala

JF-Expert Member
Joined Sep 13, 2012
409 0
ubarikiwe mzizi kweli we si mbinafsi tumefaid tunda la upendo ulilo nalo
unafananishwa na maana za matunda uliyotueleza yenye kuashiria pendo la kweli dhidi ya mwenzako
mods waiweke strickly isiondolewe
mie ni uwezo haurusu namsihi Mungu tuombeane juice ziwe kitu cha kawaida kwangu na watanzania wenzangu tutaepuka mambo mengi kuwa na afya bora
 
Fadhili Paulo

Fadhili Paulo

Verified Member
Joined
Sep 1, 2011
Messages
3,235
Points
1,195
Fadhili Paulo

Fadhili Paulo

Verified Member
Joined Sep 1, 2011
3,235 1,195
Unaruhusiwa kula matunda muda wowote iwe ni kabla au baada ya chakula, ingawa kwa wenye matatizo katika mifumo yao ya ming'enyo ya chakula wanaweza wakajisikia vibaya kula matunda kabla ya chakula.

Pamoja na kazi nyingi za matunda, mi napenda ufahamu kuwa matunda huondoa SUMU mwilini kirahisi zaidi, hivyo hakikisha isipite siku bila kupata matunda.

Unaweza ukajipangia pia kuwa chakula cha usiku leo kiwe ni matunda tu, hivyo utakusanya kwenye sahani yako papai, ndizi, embe, parachichi, nanasi, peazi, apple na kadharika na kadharika kutegemea na msimu wa matunda na uwezo wa mfuko wako, kwahiyo huo unakuwa ndio mlo wako kwa usiku huo, hakuna ugali wala wali hapo !.

Kwahiyo, iwe kabla au baada ya chakula,m kula matunda usiogope.
 

Forum statistics

Threads 1,296,597
Members 498,672
Posts 31,253,287
Top