The August
JF-Expert Member
- Oct 9, 2018
- 1,080
- 2,024
Habari za weekend wakuu?
Kwa wafuatiliaji wa maendeleo ya sayansi duniani, inafahamika kuwa Artificial Intelligence ndio muelekeo wa dunia. Kwa sasa kuna magari na ndege yasiyo na dereva mwanadamu, pia kuna mwanadamu wa bandia mwenye hisia mithili ya mwanadamu. Hivi Karibuni kampuni ya kimarekani iliyopo nchini China ya Hanson Robotics imemzindua mtu huyu kwa jina anaitwa Sophia.
Tazama video hii, ambayo Muigizaji Will Smith akifanya mazungumzo na Sophia.
Hapa pia akifanya mahojiano na mwanahabari wa UN
Nirudi kwenye hoja/swali langu.
Tunajua kuwa dini (kwa maana ya Uislam na Ukristo) zimeeleza takribani kila kitu kitokeacho duniani kwa utabiri (Prophesized) au kimeweka msimamo wake juu ya jambo fulani aidha kwa kulikubali au kulipinga. Je, ni upi mtizamo au msimamo wa dini hizi kuu mbili juu ya Artificial intelligence? Je, ni inaweza kuwa ni muendelezo au mwanzo wa kile kiitwacho Mpinga Kristo (Anti Christ) ambaye anazungumzwa kwenye dini zote mbili?
Sent using Jamii Forums mobile app