Ni Tundu Lissu pekee(Sababu moja sifa kumi)

meningitis

meningitis

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2010
Messages
8,076
Points
2,000
meningitis

meningitis

JF-Expert Member
Joined Nov 17, 2010
8,076 2,000
Wanajamvi habarini!

Niliweka post hivi majuzi na kuahidi kurudi tena na kuelezea kwa nini nimeamua kushawishi umma wa Tanzania ya kwamba TANZANIA ya leo inamuhitaji Tundu Lissu kama mwajiriwa mkuu wa wananchi.

wakati umefika na wakati ndio huu!

Utangulizi:

Nikijikita katika mada moja kwa moja napenda kusema kuwa Tanzania ya leo sio Tanzania ya Nyerere,hapa namaanisha sio Tanzania yenye maadui watatu yaani Ujinga,Umasikini na Maradhi...maadui hawa walishadhibitiwa usiniulize lini au na nani bali tulie tuelezane.

Watanzania wa leo wana elimu bwana...watu wanatumia simu,TV na teknolojia za kigeni bila shida.elimu ya msingi kwa sasa ni kidato cha nne,maelfu kwa maelfu ya vijana wako vyuo vikuu.hivyo sitarajii kumsikia mtu akilalamika juu ya watanzania kupata elimu iwe bora au hiyo hiyo ya kuungaunga...Adui alikuwa ni upatikanaji wa elimu na sio ubora wake!!!

Swali la kujiuliza jee elimu hii wanayopata vijana wetu hasa ile asilimia 75 ya wakulima na labda kwa kuongezea asilimia 10 ya wafugaji inafanana na ile wanayopata asilimia chini ya kumi ya tabaka la viongozi/masingasinga na washirika wao?

Hivi hii elimu waliyopewa watoto wa mbwa imelenga kuajiriwa au kujiajiri?

Watanzania wa leo sio maskini bwana.mabarabara ya lami kila kona,umeme vijijini wa kuwasha taa tu(wanakijiji wataanza kuchelewa kulala).Watu wanamiliki simu,toyo na mafundi cherehani wa sikuhizi hawajui kuweka viraka.Ukiongelea msosi hii sio issue tena kwani siku hizi hakuna kupanga foleni ya mkate huku kuna skonzi za Azam.

Umasikini hakuna tena...naam

Watanzania wa leo hawaumwi kipindupindu,Ukoma,vikope n.k watanzania wa leo wanaumwa dengue,B.P na rare cases kansa ya Tezi....
Isitoshe kuna zahanati au kituo cha kutoa huduma za afya kila kijiji.Adui alikuwa ni upatikanaji wa huduma za afya sasa zipo.

Jiulize sasa huduma hizi za hospitali hata ile zahanati kuu ya Muhimbili zinakujia kwa hisani ya nani?Jibu lako kaa nalo.

Wakuu msichoke naendelea na utangulizi.

ADUI WA TAIFA HILI NI YUPI HASWA KWA SASA??

Kabla sijamtaja ningependa kusema kuwa inawezekana miaka yote tuliyofanya uchaguzi hatukuwahi kuwa na ajenda kama taifa bali tuliendelea kuimbishwa kama kasuku kuhusu maadui hawa watatu.Sasa
ni wakati muafaka tukaingia kwenye uchaguzi huu tukiwa na ajenda ya pamoja.

Adui pekee aliyebaki Tanzania ni UFISADI...yaani huyu ndiye kubwa la maadui .Hata hayati JKN hakustuka au aliunderestimate uwezo wa Adui hili na ndio maana leo hii limekuwa kubwa la maadui.

Tanzania ya leo inakwamishwa na Ufisadi ama mfumo na mtandao wa kifisadi unaokuwa kwa kasi.....

Vijana wanakosa mikopo ya kusoma vyuo vikuu mpaka wanasingizia wazazi wao ni vilema au wafu ili tu wapate mkopo ilihali kuna mafisadi wamehifadhi vijisenti uswisi.

Madawa yanakosekana katika zile zahanati za kila kijiji ikiwemo ile zahanati kuu kisa ni madeni au labda watu wanataka kujipigia 10%

Kwa ufupi ufisadi ni janga janga janga la kitaifa kwani hata umeanza kujidhihirisha makanisani.

Tunahitaji kuwawajibisha,kuwachukia na ikiwezekana kuwapoteza.

Kazi hii hahitaji mtu legelege bali mwenye dhamira na tabia isiyokoma ya kuwa na misimamo isiyoyumba....Hii ndio SABABU MOJA YA KUMPA LISSU KIJITI KWA TIKETI YA UKAWA.

Tunapomkabidhi Mama Tanzania tumwambie kazi yako ni moja tu ya kutuondolea ufisadi na mafisadi.

Kama ni viongozi tunao tunachohitaji ni kuwaondoa viongozi wenye nasaba za kifisadi.

Kama ni madaktari au waalimu au majaji wapo na tutaendelea kuwapata lakini tunahitaji kusafisha watumishi wote wenye genes za kifisadi.

Hatuna uhaba wa maafisa ugavi au wahasibu wanaoshiriki ufisadi tunahitaji kuzalisha wagavi au wahasibu waadilifu n.k n.k

SIFA KUMI ZA TUNDU LISSU KWA MUKTADHA WA HOJA HII

1-Tundu Lissu ni mkweli kwa kimombo yuko Honest.mara nyingi hujiweka wazi katika misimamo yake na hivyo kuwafanya wake kumuelewa na wao kuamua au kuchukua upande.Kijiko hukiita kijiko na sio beleshi dogo!

2-Maono/Malengo yaliyonyooka ama kwa kimombo niseme anaweza kufocus.
Kama uliwahi kumsikiliza bungeni basi utajua hajaikosa hii tabia kwani hata panapotokea distractions kama vile kutukanwa basi yeye hubaki katika mstari na kuendelea kukifafanua au kukifikia kile anachotaka.

3-Heshima kwa utu.Toka mwanzo wa siasa/harakati Tundu lissu amejikuta akipambania utu wa mwanadamu,rejea harakati za migodini.

4-Uwezo wa kujenga hoja na kushawishi.
Hili ni jambo muhimu kwani ukienda Zanzibar Tundu Lissu ameweza kuwavutia wazanzibar mpaka kupachikwa jina la Messi wa Ukawa.Naweza kusema hakuna kiongozi kutoka bara tena mkiristo anayeweza kuwa na ushawishi kwa upande wa zanzibar isipokuwa TL.iwe ndani au nje ya UKAWA.

Na hii ndio turufu muhimu kwa UKAWA kwa wakati huu.

5-Ujasiri
Tundu lissu hajawahi kuogopa especially kuwaogopa mafisadi.

6-Ujuvi au labda kwa lugha ya malkia niite Arrogance.Arrogance ni tabia isiyopendwa na wengi lakini Tabia hii ndio inayohitajika pindi unapopewa kazi ya kipambana na mafisadi papa na watumishi wajuaji.

pia ni sifa hii inayohitajika pale utakapokutana na mataifa makubwa yanayotaka kunyakua rasilimali za nchi hii.

7-Ni kijana na bado ni mkakamavu.

8-Ni mwanasheria nguli anayejua kucheza na sheria na hiki ndio kiama cha mafisadi kwani watafilisika kwa kukodi mawakili wa kupambana na Rais mwenye dhamira ya kuwanyoosha.

9-Ameishi na kukulia katika umasikini.Amekumbana na kuchukia dhahma za kuchangishwa michango ya kipuuzi huku kodi zikiliwa na mafisadi.

10-Anajifunza na kucope na mazingira kwa haraka.Uwepo wake ndani ya bunge baada ya Dr Slaa kuondoka umekuwa ni chachu ya mabadiliko nchini.


Nimalize kwa kusema kuwa Tundu Antiphas Mughwai Lissu ni aina ya kiongozi anayehitajika kwa sasa.


Tuungane kutokomeza ufisadi!!!
 
BONGOLALA

BONGOLALA

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2009
Messages
16,183
Points
2,000
BONGOLALA

BONGOLALA

JF-Expert Member
Joined Sep 14, 2009
16,183 2,000
Naunga hoja mkuu,hapo ma ccm lazima yahame nchi
 
Kimilidzo

Kimilidzo

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2011
Messages
1,347
Points
1,225
Kimilidzo

Kimilidzo

JF-Expert Member
Joined Jan 3, 2011
1,347 1,225
Hebu tuwekee matokeo yake ya mtihani, kuanzia darasa la Saba, form four, form six, first degree GPA na masters GPA tumcheki kama ubongo unachaji. Mambo ya kurudia kuwa na raisi wa GPA 2.1 mvivu hata kupitia hotuba hata ripoti ya cag hasomi hatuyataki...

Ila naskia huyu jamaa hajawahi kuomba wala kupokea rushwa, kama ni kweli magamba watasanda
 
mandella

mandella

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2011
Messages
2,894
Points
2,000
mandella

mandella

JF-Expert Member
Joined Oct 29, 2011
2,894 2,000
Hebu tuwekee matokeo yake ya mtihani, kuanzia darasa la Saba, form four, form six, first degree GPA na masters GPA tumcheki kama ubongo unachaji. Mambo ya kurudia kuwa na raisi wa GPA 2.1 mvivu hata kupitia hotuba hata ripoti ya cag hasomi hatuyataki...

Ila naskia huyu jamaa hajawahi kuomba wala kupokea rushwa, kama ni kweli magamba watasanda
Acha kwanza CV za Tundu Lisu.. kwa hatua za awali naomba fanya hiviii..

Embu kaa chini na CV zako(hizo unaziona ziko sawa) Tafuta CV za John Mnyika kisha rudi kwnye swala la maamuzi na effect katika kujenga nchi kati yako na yeye.

utajua nafasi ya GPA ni ipi .

ukimaliza hapo endelea kutafuta ya Tundu lisu sasa .
 
Kimilidzo

Kimilidzo

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2011
Messages
1,347
Points
1,225
Kimilidzo

Kimilidzo

JF-Expert Member
Joined Jan 3, 2011
1,347 1,225
Umejenga hoja japo sina hakika km TL ni president material kwa sasa. Mimi namwona km AG. Asante mkuu meningitis
Kama President material ndio hao akina Kikwete ni bora tumpe Tundu Lissu. Nina uhakika wanaCCM wengi watampa kura akiwemo Anna Makinda
 
Last edited by a moderator:
mandella

mandella

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2011
Messages
2,894
Points
2,000
mandella

mandella

JF-Expert Member
Joined Oct 29, 2011
2,894 2,000
Hoja yako imekaa sawa japo kuna sehemu zina mzaa .
Sasa sijui ndio umetumia kuchangamaha thread or vip.

Ila mapendekezo yako bado si sahihi .

Nchi kwa sasa haiitaji kukaa mikononi mwa mtu mwnye janzba nanmwnye miamko.

Tunahitaji busara zaidi kwnye kitu hiki.
 
CattleRustler

CattleRustler

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2013
Messages
1,057
Points
1,250
CattleRustler

CattleRustler

JF-Expert Member
Joined Oct 26, 2013
1,057 1,250
Hebu tuwekee matokeo yake ya mtihani, kuanzia darasa la Saba, form four, form six, first degree GPA na masters GPA tumcheki kama ubongo unachaji. Mambo ya kurudia kuwa na raisi wa GPA 2.1 mvivu hata kupitia hotuba hata ripoti ya cag hasomi hatuyataki...

Ila naskia huyu jamaa hajawahi kuomba wala kupokea rushwa, kama ni kweli magamba watasanda
Mimi sihitahi kuona vyeti. Yake kujua kama jamaa ni kichwa maana kazi yake ni first class. Mimi naona sifa yake kubwa ni mzalendo na na amumunyi. Uzalendo ninaouongelea ni ule wakuwatetea masikini walioondwa kwenye machimbo. Na kuto kumumunya kama munakumbuka bunge la escrow kunawakati watu walijiuliza kama raisi hatatekeleza maazimio ya bunge itakuwaje?. Jamaa aliibuka nakusena tunamu-impeach. Nazani kunawabunge wa CCM walijikojolea.
 
Kimilidzo

Kimilidzo

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2011
Messages
1,347
Points
1,225
Kimilidzo

Kimilidzo

JF-Expert Member
Joined Jan 3, 2011
1,347 1,225
Acha kwanza CV za Tundu Lisu.. kwa hatua za awali naomba fanya hiviii..

Embu kaa chini na CV zako(hizo unaziona ziko sawa) Tafuta CV za John Mnyika kisha rudi kwnye swala la maamuzi na effect katika kujenga nchi kati yako na yeye.

utajua nafasi ya GPA ni ipi .

ukimaliza hapo endelea kutafuta ya Tundu lisu sasa .
Mnyika ni namba nyingine, darasa la Saba aliongoza mkoa na form four akapata point Saba. Ndio maana akili ya Mnyika inachaji Sana...

Angalia watu waliofeli darasa la Saba na kurudia mara tatu kama Sospeter Muhongo, au waliorudia mara moja moja kama HKigwangali aka Saidi Bagaile au Lameki Madelu aka Mwigulu Nchemba walivyo watu wa kukurupuka na kutotumia akili. Sio kwamba hawapendi kutumia akili, ila hawana hiyo akili. Nadhani umeelewa kwa nini nataka kujua matokeo ya awali ya TL sasa.
 
Kimilidzo

Kimilidzo

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2011
Messages
1,347
Points
1,225
Kimilidzo

Kimilidzo

JF-Expert Member
Joined Jan 3, 2011
1,347 1,225
Hoja yako imekaa sawa japo kuna sehemu zina mzaa .
Sasa sijui ndio umetumia kuchangamaha thread or vip.

Ila mapendekezo yako bado si sahihi .

Nchi kwa sasa haiitaji kukaa mikononi mwa mtu mwnye janzba nanmwnye miamko.

Tunahitaji busara zaidi kwnye kitu hiki.
Busara mbele ya wezi na mafisadi haijitajiki. Kuna raisi alikuwa na busara nchi hii kumzidi Ally Hassan Mwinyi? Alitupeleka wapi na busara zake mzee ruksa. Tunahitaji mtu wa vitendo
 
kilambalambila

kilambalambila

JF-Expert Member
Joined
Nov 16, 2013
Messages
8,430
Points
2,000
kilambalambila

kilambalambila

JF-Expert Member
Joined Nov 16, 2013
8,430 2,000
tundu lisu ana akili lakin ana jazba sana hafai
 
Head teacher

Head teacher

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2012
Messages
1,806
Points
0
Head teacher

Head teacher

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2012
1,806 0
Lisu the president...slaa naye is best lakini Mzee...tuleteeni lisu tu yatosha
 
Sangarara

Sangarara

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2011
Messages
13,114
Points
2,000
Sangarara

Sangarara

JF-Expert Member
Joined Sep 29, 2011
13,114 2,000
Kiukweli kama UKAWA wanataka kushinda kiulaini wampitishe Tundu Lissu.
Uchaguzi mdogo umeonyesha njia.
Ni jimbo lililofanya vizuri kuliko yote nchi nzima.
Pia kama Tunataka kweli kupambana na UFISADI,Tundu Lissu atosha japo wanaSingida Mashariki tutapata pigo bungeni.
 

Forum statistics

Threads 1,335,208
Members 512,271
Posts 32,499,184
Top