Ni Tukio gani ambalo umewahi kulifanya, au kufanyiwa katika siku ya Wajinga

The last don

JF-Expert Member
Aug 3, 2011
989
992
Habari Wadau wa Chit-Chat,
Tukiwa tumebakisha masaa kadhaa kabla watu na vijarida mbali mbali kutufanya wajinga kwa muda mfupi katika maadhimisho ya sikukuu isiyo rasmi April Fools' Day.

April Fools' Day maarufu huku kwetu kama 'siku ya wajinga' ni siku ambayo huadhimishwa duniania kote Tarehe mosi ya mwezi wa nne,ingawa hadi hivi sasa chimbuko au asili yake rasmi bado haijafahamika ingawa kuna hadithi nyingi sana zinazoelezea ilipoaanza kuadhimishwaa mbali huko takribani kuanzia karne ya kumi na nne,ikiwa ni siku maalumu ambayo taarifa/habari ambazo hazina madhara (harmaless hoax/pranks) huwa zinasambazwa kwa marafiki au majirani kwa minajili ya kujiburudisha na kupima (mental alertness) uwezo wa kupokea,kuchambua na kufanya maamuzi sahihi taarifa za ghafla na za kustusha.

Je wewe ni tukio gani ambalo umewahi kufanyiwa au kumfanyia mtu katika siku hii na nini ilikuwa reaction yake Kariiibuni.
 
Habari za Fool's Day, Valentines Day, sijui siku ya Wanawake duniani....

Kwetu sisi Waislamu ni haramu haramu.

Hatuna muda na mambo ya kipuuzi kama hayo
Hayo ni maoni yako Chief,lakini lengo la thread ni kutaka kuweka awareness ya siku hii,maana watu wengine ufanya zaidi ya lengo la siku yenyewe na kusababisha madhara makubwa,hivyo kwa kuwa haya yanatokea katika jamii ambayo ni mchanganyiko wa watu wa tamaduni na imani zote na sisi tupo katika hizi jamii basi sioni taabu kuelimishana ili tuone to what extent siku hii inaweza leta madhara au faida..........(Not to that Extent mkuu).
 
1-4-2017 Goal.com walitangaza kuwa Messi kasajiliwa na Real Madrid, kwanza Madrid siipendi maana mimi ni shabiki wa Barca, so nikazidi kuilaani Madrid.
 
Back
Top Bottom