Ni Tanzania tu au hata Ng'ambo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni Tanzania tu au hata Ng'ambo?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Gates, Feb 9, 2011.

 1. G

  Gates Member

  #1
  Feb 9, 2011
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Habarini wapendwa.

  Kuna suala moja limekuwa likinitatiza sana na nimekuwa najiuliza mara kwa mara bila kupata majibu yanayoridhisha.

  Jambo hili linahusiana na mgawanyo wa pato la taifa.

  Binafsi nimekuwa nikihisi kwamba wanaofaidi mali ya nchi ni wanasiasa huku wataalamu wa fani mbalimbali wakitelekezwa.

  Najua naweza kupata msaada wa mawazo hapa. Sioni sababu ya wabunge kulipwa zaidi ya wataalamu wetu kama madaktari, walimu nk.

  Sina hakika kama hili limekaa sawa na sina hakika kama nchi za wenzetu wanawalipa wanasiasa zaidi ya wataalamu.

  Kutokana na mgawanyo mbovu bunge limejaa wataalamu lukuki ambao wamekimbia fani zao zenye maslahi duni na kwenda bungeni kupiga longolongo na kujipatia maslahi maradufu. Tunakwenda wapi?

  Naomba msaada katika hili.

  Nawakilisha.
   
 2. 22nd

  22nd JF-Expert Member

  #2
  Feb 9, 2011
  Joined: Aug 1, 2010
  Messages: 498
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  nadhani ni bongo tu na nchi nyengine zenye ufisadi,japo kuwa hata huku ng'ambo wabunge wanalipwa sana tu,lakini inaweza kulingana na wataalam au hata wataalam wakawazidi hao wabunge. nchi ninayokaa, ukiwa mwalimu wa primary si kitoto,fresh from college anaanzia na kama euro alfu 4 hivi.
  sasa imagine huo ni mshahara wa mwalimu ambaye bongo ndio anadharaulika, je ukienda kwenye sector ya technology au healthy as nurses and doctors.

  judges wanakamata kama 1.5 mils per year,which is about 100milions shilings za kibongo per month,bado na marupu rupu.
  sijagusia kwenye kufuta kinyesi wale wazee. halafu eti nirudi bongo, wakati unaweza kuwa na hela na umeme ukakosa

  na ikumbukwe kwamba mshahara ulaya unalipwa kutokana na experience,kila mwaka,kiwango kinaongezeka. sio kama bongo, mshahara upo pale pale.hata ukiwa kazini miaka 50
  i cant wait to graduate.:popcorn:
   
Loading...