Ni Tanzania pekee wananchi wako tayari kuburuzwa na kundi fulani la watawala

mkulima gwakikolo

JF-Expert Member
Nov 22, 2014
1,767
2,851
Ndani ya miaka sita ilyopita, nchi hii tumeshuhudia sheria zilizopo zikipindisha haki kwa kiwango cha kutisha. Raia wakitendewa ndivo sivyo katika nyanja mbalimbali.

Vyombo vya maamuzi zikiwemo mahakama vikifichwa mfukoni na kundi fulani, kitu kinachopelekea kundi lenye haki likiumizwa vibaya. Hivi punde kwenye kesi ya Mwananchi ambae ni kiongozi wa juu akisingiziwa kesi kinyume kabisaaa na utaratibu na hata Ushahidi ukionyesha uonevu.

Lakini mbinu mbalimbali zimekua zikitengenezwa ili aidha kumuumiza kisaikolojia ama kumfunga. Yote haya yakiwa yanatendeka Wananchi wako kimya bila kuonyesha hisia juu ya uonevu huu. Je, kundi hili limeshika dhamana ya wananchi ama limejishikia dhamana yake lenyewe?
 
Pumbaff kabisa. Acha mahakama itende haki kama ilivyofanya kwa Sabaya. Kuweni wavumilivu tu kasindano kaingie
 
Case study wazee wa Escrow na mashehe wa uhamsho wamewaweka ndani miaka kwa uonevu Mkubwa bila hata ushahidi, na kukosekana kwa ushahidi wakawaachia bila hata aibu. Kesi za kubandika hata ukikaa ndani miaka elfu ushahidi wa kuokoteza hauwezi patikana. Tegemea tu ya kingai na mahita.
 
Mkuu hata wewe kama mwananchi tayari umetimiza wajibu wako juu ya hili sakata.

Kwa hali ilivyo nchini mwetu usitegemee kuyaona maandamano ya kutafuta haki.

Hapa hapa jf ndiyo platform pekee unaweza kuonyesha masikitiko na kilio chako na ukaweza kupaaza sauti ikasikika kwa wahusika.
 
Back
Top Bottom