Ni Tanzania pekee ambapo kuna elimu ya chuo yenye mwisho

NOKIALUMIA

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
396
275
Ndugu zangu wanaJF mimi sio mjuzi sana katika nyanja za elimu ila kuna mambo nime yasikia yamekua yakinichnganya saana. maswali makubwa niliyonayo ni pamoja na

1. NACTE kufuta baadhi ya kozi bila kushirikisha wadau mbalimbali na bila wazir mwenye dhamana ni ubabe au ndo utaratibu wa kiutendaji? mfano NACTE mwaka huu imefuta kozi ya ADVANCED DIPLOMA IN CLINICAL MEDICINE (AMO) je wamehusishwa wadau katika kuangalia mbadala au ni mbinu ya kutaka kuiua kozi ya clinical medicine?

2. Wastani wa clinical officer kujiendeleza utapungua kutokana na changamototo za ufaulu ambao nacte wanabdilisha kila siku wanapoamka! kwa mfano miaka ya nyuma clinical officer akiwa na GPA ya 3.0 Na kuendelea alikuwa na uwezo wa kijiendeleza kusoma MD ikumbukwe kuwa mtu mpka kuja kupata GPA ya 3.o Manake amepata UFAULU Wa wastani wa B Kwenye masomo yake yooote ya mtihani wa mwisho. Ila sasa TCU wameongeza wastani wa kwenda MD mpaka 3.5 ikwa na maana kuwa na B+ Kwenye masomo yoote .hii ni ishara ya uonezi ikizingztiz kuwa mtu ashakuwa na exposure kubwa kwenye swala la medicine lakini badae anakosa haki ya kijiendeleza kabisa kibaya hata kama atapata GPA ya tano akienda chuo anaenda kuanza kusoma na mtoto alietoka form six hata kama kafanya kazi miaka kumi .

3. Je, serikali ina mkakati gani kwenye hili . Endapo serikali yetu haitaharibu hali hii ya kuwa na elimu yenye mwisho Tanzania bado itakuwa nyuma katika utoaji wa huduma bora .ukizingatia kila siku technolojia na mambo mengi yanabadilika kila siku baada ya miaka 20 clinical officer atatumia skills za mwaka 2010 (curriculum) kumtibu mgonjwa mwaka 2035 kwa sababu tu amekosa nafasi ya kujiendeleza.

4. Kwa wenye ndugu anaesoma clinical medicine kama yupo mwaka wa kwanza ni bora akamwambia abadilishe kozi mapema iwezekenavyo, kwani kwanza anasoma vitu limited pili ni vigumu kwelikweli sio mzaha ,na atajuta huko mbela atakapo skia kozi hii inafutwa (just prediction) na hatapewa taarifa

5.Nashauri serikali iangilie vitu vifutavyo
A. Ifute kabisa hii kozi ya clinical medicine
B. AU itafute suluhu ya kujiendeleza kwa clinical officer mwenye GPA chini ya 3.5
EITHER imruhuru mwanafunzi arudie mitihani yake ya nta level 6 ili ajaribu tena na tena kupata wastani unao hitajika kama ilivyo level nyingine za sekondari mtua akifeli anarudia,
C. Ifanyie kazi proposal za nyuma za kuanzishwa kwa banchelor of clinical medicine (kama wanavyofanya zambia .. ingi official website ya UNIVERSITY OF ZAMBIA au google baadhi ya university za china ,malawi etc
D. Itamke wazi kuwa clinical officer akitaka kujiendeleza afanye nini. serikali iandae foundation course ili wadogo zetu nao wasome
E. NASHAURI Wafute hii kozi ,ili iwe rahisi wao kuamua mambo yao bila kuadhiri mambo na elimu za watu wengine
 
PERFORMANCE YA SEMESTER 6
Sorry kidogo.Nina mdogo anasoma hiyo course ya clinical officer. sijaelewa jinsi gpa zao zinavyorelate na average anaoupata.Anaweza kukuambia ana wastani wa B ila gpa ya 3,hivyohivyo anaweza kukuambia anawastani wa B ila gpa ya 2.8.Hizi gpa zatafutwa vipi?.
 
Calculation inategemea na mwaka pia
 
pole mkuu, nami nashauri tuangalie namna ya kuifuta kabisa ili tutengeneze MDs wengi wakuja kujaza hilo gap, na nguvu ielekezwe kwa MMDs etc, hii italeta ushindan ndani na nje ya nchi, pia vijana wengi wenye ufaulu wa div1&2 watapata nafasi kwa wingi
 
kwanza nianze kwa kuwapongeza waliofuta hiyo AMO, naomba wasisahau kufuta na CA. Bora kubaki CO, MD na juu ya hapo.

Pia ingependeza zaidi kama GPA ya kutoka CO kwenda MD angalau ianzie 4. Maana hata hiyo 3.5 ni kama wanacheza tu, iwe ya kuingilia kozi nyingine.

Hii ni ili kuboresha elimu yetu, watu wawe serious na elimu.
Mtu unapolalamikia GPA ya 3.5 aisee hapo lazima kuna tatizo.
Ishu ni kukaza.
Na sio lazima kila akasome udaktari, ukiona vigezo vigumu soma vitu vingine mbona fani nyingi tu.
 
Bila shaka wewe ni niaje niaje some where ungekuwa kamili usingeweza kuandika hiyo maneno yako
 
soma kijana, usipende vitu rahisi rahisi
malalamiko yake yatasikilizwa endapo vyuo vingesema wanafunzi hawatoshi kisa vigezo viko juu. Lakini ndio hivyo vyuo viko saturated pamoja na kuchukua GPA ya 3.5+. Apambane tu na hali yake kwa maana hakuna sehemu imeandikwa lazima CO ajiendeleze kuwa daktari. Duniani lazima tuzidiane tu ili maisha yaende.
 
Umeboa uliposema waweke 4 kwa sababu labda wewe tayari ushafika huko na hautaki wengine tufike au?
Sio hivyo mkuu, katika maisha ni vyema kufanya kitu unachokiweza sio unachokipenda. Ipo siku watu watasema hata iwe 2.5 ili tu wengi wapate nafasi.
Mambo hayako hivyo, si lazima kila CO akawe MD. Na lazima viwango vya elimu vilindwe ili ubora uendelee kuwepo.
GPA ya 4 ni kiwango kizuri ambacho hauwezi kutiliwa shaka, ni passible kabisa mtu kupata hivyo.
 
N
malalamiko yake yatasikilizwa endapo vyuo vingesema wanafunzi hawatoshi kisa vigezo viko juu. Lakini ndio hivyo vyuo viko saturated pamoja na kuchukua GPA ya 3.5+. Apambane tu na hali yake kwa maana hakuna sehemu imeandikwa lazima CO ajiendeleze kuwa daktari. Duniani lazima tuzidiane tu ili maisha yaende.
Ndio hapo mkuu, vyuo nafasi hakuna, watu wapo eligible kusoma MD lakini wanaachwa kwa kuwa nafasi ni chache, halafu bado mtu anataka vigezo vishushwe.
 
Sio lazima uwe daktari mkuu..Kuna taaluma nyjngi tu zinafaa watu average kama wewe.
Wewe ni nani hadi unipangie cha kusoma?uzuri mmoja mitihani ya mwisho ya CO inasahihishwa nacte na siyo watu kama nyinyi ukifaulu unefaulu kiuhakika
 
kwanza nianze kwa kuwapongeza waliofuta hiyo AMO, naomba wasisahau kufuta na CA. Bora kubaki CO, MD na juu ya hapo.

Pia ingependeza zaidi kama GPA ya kutoka CO kwenda MD angalau ianzie 4. Maana hata hiyo 3.5 ni kama wanacheza tu, iwe ya kuingilia kozi nyingine.

Hii ni ili kuboresha elimu yetu, watu wawe serious na elimu.
Mtu unapolalamikia GPA ya 3.5 aisee hapo lazima kuna tatizo.
Ishu ni kukaza.
Na sio lazima kila akasome udaktari, ukiona vigezo vigumu soma vitu vingine mbona fani nyingi tu.
Unafikiri ishu nikusema kuwa ni kubwa sana ishu nikubadilikabadilika kama kinyonga leo kijani kesho nyeupe yaani kero tupu bora wasema gpa ya 5 afu watulie hapo
 
Sio hivyo mkuu, katika maisha ni vyema kufanya kitu unachokiweza sio unachokipenda. Ipo siku watu watasema hata iwe 2.5 ili tu wengi wapate nafasi.
Mambo hayako hivyo, si lazima kila CO akawe MD. Na lazima viwango vya elimu vilindwe ili ubora uendelee kuwepo.
GPA ya 4 ni kiwango kizuri ambacho hauwezi kutiliwa shaka, ni passible kabisa mtu kupata hivyo.
Ubora upi unaozungumzia?kutoka CO hadi MD huyo mtu mheshimu sana ni kwamba anajua kuliko hata wewe uliyeenda na form six yako,kwa hiyo mimi naona hao wa form six waende kuanza na CO ndo baadae waendelee wakishapata hiyo GPA ya 4
 
Mngekua mnaenda kujiendeleza ili kuongeza output ingekuwa vyema ila wengi wenu mnaenda kujiendeleza just for promotion and big salaries,
Acha mbanwe tu ili tupate ma dr waliokwiva na sio wenye gpa za 32.
 
Back
Top Bottom