Ni sheria japo hazijaandikwa

Ni sheria japo hazijaandikwa

Ilushenisti

Senior Member
Joined
Mar 11, 2013
Posts
118
Reaction score
46
Hizi ni sheria, ni kama katiba ila haihitaji mchakoto mrefu na malumbano kama ya CDM na CCM na kwenye katiba mpya ya Tanzania. Hii haijaandikwa popote japo mwanaume unatakiwa kufahamu. Ni sheria ambazo dume lolote halina budi kuzizingatia.

1. Ni marufuku kutembea na dada au ndugu wa karibu wa rafiki yako isipokuwa tu kama unataka kuoa kabisa

2. Ukibaini rafiki yako ana mipango ya kando ni mwiko kumweleza mkewe ama rafiki yake wa kike. Kaa nayo moyoni.

3. Ukigundua rafiki yako anadanganywa/anaibiwa na mkewe/rafiki yake wa kike, funga mdomo, unaruhusiwa kumwambia kama ni mtu wako wa karibu sanaaaa.

4. Ukimkopesha rafiki yako pesa usitangaze, usimdai hadharani.

5. Kamwe usipende kwa moyo wako wote na akili yako yote, bakiza kiasi, jua unaweza kutendwa, usiingie mzima mzima, unaruhusiwa kufanya hivyo mara moja tu katika maisha.

6. Uanaume ni kuwajibika kwa matendo yako na matokeo yake, mwanaume hafanyi maamuzi alafu akakimbia matokeo yake,

7. Mwanamume ni kichwa, usikubali hata siku moja kuuongozwa na mwanamke ndani ya uhusiano. Chukua ushauri wake, sikiliza maoni yake, pata mtizamo wake lakini maamuzi ya mwisho ni lazima yawe ya kwako. Inakubalika lakini kwa ajili ya amani umdanganye kuwa ana madaraka fulani kipindi fulani. Kurudi nyuma kujipanga inakubalika lakini kujisamisha kabisa ni mwiko!

Nitaendelea wakuu, ila karibuni muongeze
 
Back
Top Bottom