Ni sawa Mwanaume kujipaka lipbum?

Ni sawa Mwanaume kujipaka lipbum?

Ndugu wanaJF,
Kuna baadhi ya vitu huwa vinatumiwa tu na wanawake, lakini pia vipo vinavyotumiwa na wanaume tu, japo vipo ambavyo twaweza kutumia pamoja. Sitaki kuzungumzia perfume maana nahc kutakuwa na ubishi sana. Unakuta perfume imeandikwa 'for women' lakini mwanaume kajipulizia nyingi, vitu kama simu kutegemeana na rangi twaweza kutumia wote.

Hoja yangu ni matumizi ya LIPBUM kwa wanaume. Mimi huwa nikienda salon nikipakwa najihc kama njiani nasemwa kwasababu sijui. Naomba tusaidiene hapa hasa wale wanaotupaka au wanaotengeneza au wauzaji.

Nililazimika kuzitrumia kwa mara ya kwanza Iringa ilikuwa ni mwezi wa sita, kuna baridi na upepo mkali sana. Nilipasuka lips mpaka zikawa zinatoa damu pamoja na kujilamba sana lakini haikusaidia, nikaletewa hayo mafuta ya mdomomoni na yalinisaidia sana kupona.

Kikubwa inategemea mtu anazitumia katika mazingira yepi, anajipodoa tu au anatumia kwa sababu za msingi??
 
Na huu upepo....acha kujipaka uone lips zinavokuwa kama kisigino
mi sioni shida ila zisiwe za rangi kama wanazopaka kina ommy dimpoz na wabana pua wenzie

Ha haaa eti lips kama kisigino,sio kama goti la mbuzi?
 
Nililazimika kuzitrumia kwa mara ya kwanza Iringa ilikuwa ni mwezi wa sita, kuna baridi na upepo mkali sana. Nilipasuka lips mpaka zikawa zinatoa damu pamoja na kujilamba sana lakini haikusaidia, nikaletewa hayo mafuta ya mdomomoni na yalinisaidia sana kupona.

Kikubwa inategemea mtu anazitumia katika mazingira yepi, anajipodoa tu au anatumia kwa sababu za msingi??

aise mkuu sijui tulikua wote,mimi pia niliwahi kutumia kipindi nimeenda iringa kule huna ujanja bwa shee ni lazima utumie tu hasa kwa mtu mgeni.kwa huu upepo wa daa kama ni kupaka basi iwe ni kiasi kidogo sana hakuna baridi ya kutisha.
 
Powa tu.. ila hupaki kama ke, lips zinashine sana. Kiasi inatosha inasaidia lips zisipasuke bana.

by the way.. ukipaka hiyo na poda, ujiandae kuombwa.
 
sio LIPBUM tu,, ila katika kila tunavyovifanya au kuamua kuanza kufanya ni lazima kila mtu aichunguze DHAMIRA yake ya ndani ,,,,
kama kweli unamaanisha kutunza midomo, endelea kwa ujasili lakini kama unamaanisha kuuza sura au uonekane na kina flani, au nafanya kama fulani.....................nikupe pole sana kwa kupoteza lasilimali MUDA, FEDHA na kula kwa pozi kwa hofu ya hayo madude kuachia mdomo
 
Ni nafuu hata kupaka Lip bum kuliko mwanaume anayetengeneza nywele (kuweka curl). Mi huwa simwelewi dume wa aina hiyo.
 
Majuzi apa ilikuwa wanaume kuvaa cheni..leo lip bum...naona uyu dogo benteke anajidai haijui lol

Ila sasa tunarudi kule kule kutojua matumizi yake lakini pia orthodox thinking tu kwamba nikitumia kitu flani nitakuwa "mwanamke" hata kama hatujajua faida/hasara zake.....sasa lip bum sehem za baridi na upepo mkali inasaidia sana ili mradi hupaki lip stick na sio za kung'aa sana, muhim kwa afya ya lips.
 
Last edited by a moderator:
mie jana tu nimeona mtangazaji wa television moja hapa tz kapaka lipstic ya pink imemkolea kweli kweli sa sijui ndo fashion

Ulikuwa unaangalia kipindi au umeconcentrate kumwangalia mtangazaji mwallu
 
Last edited by a moderator:
kwa nchi za baridi hata wanaume wanatumia hio kwa sababu midomo inakauka hadi inapasuka,usipotumia hio utapasuka midomo hadi inatoa damu. ila kwa hapa dar tuwaachie dada/mama zetu.

Ulichosema ndio nilichotaka kusema.
 
sweetie mimi natumia vaseline petroleum jelly

Ya kipind cha barid na upepo ni mazuri hayangai kwenye lipi na wala hayana harufu....
Afu baby Nina kesi njoo home haraka miss neddy anasema anajua lip unazotumia wewe na shahid ni yeye...
 
Last edited by a moderator:
Mimi kitu cha kujipaka akishatumia mama watt huwa sikitumii kbs...utapakaje vitu anavyopaka mkeo?
 
Ya kipind cha barid na upepo ni mazuri hayangai kwenye lipi na wala hayana harufu....
Afu baby Nina kesi njoo home haraka miss neddy anasema anajua lip unazotumia wewe na shahid ni yeye...

hahaha miss neddy mchokozi huyo hajui loloteee
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom