Ni sawa kwa Mama Tunu Pinda?

Status
Not open for further replies.
UK waziri mkuu alikuwa mwanamke,mume wake akatumia peni na karatasi za ofisi ya waziri mkuu kwa shuguli zake akatupwa jela miaka kazaa.
 
Reactions: Nzi

Acha jazba, rudia kusoma ulichoandika then hoji ' itifaki' inasemaje kuhusu uwakilishi wa Waziri mkuu kwenye Msiba huo.
 
Kwenda kwa Mama Pinda na gari ya serikali kwenye msiba wa Kanumba tena lenye nembo ndiyo kumesababisha TZ iwe na uchumi mbaya duniani?Safari hiyo ya Mama Pinda na gari hii ndiyo kumesababisha tusiwe na umeme wa uhakika,madawa kwenye hospitali zetu,kufeli kwa vijana wetu,dubious contracts;migomo ya wafanyakazi na matatizo mengine mengi yanayotukabili?

Mm naona tumeacha kujadili matatizo yetu makubwa yanayotukabili na sasa tunaanza kujadili vitu vidogo vidogo sana ambavyo SIO NDIYO VIMETUFIKISHA KTK HALI MBAYA HII YA UCHUMI!CCM wanafurahia sana tukiacha kujadili issues!
 
UK waziri mkuu alikuwa mwanamke,mume wake akatumia peni na karatasi za ofisi ya waziri mkuu kwa shuguli zake akatupwa jela miaka kazaa.

...thibitisha tafadhali,...ni waziri mkuu yupi na mwaka gani yalitokea hayo,
otherwise unazungumzia udaku wa kijiweni.
 
Naona hatari kubwa hapo watu wamejikusanya karibu kabisa na transformer. Inabidi manispaa ya KInondoni ije kuwaondoa kwa kuwa ni eneo hatarishi kama Ubungo.
 
Kwa mfano waziri mkuu angekuwa mwanamke harafu mume wake aende na gari lake msibani namna hiyo ingekuwaje?. Just curious..
Mkuu hii sijui nayo inakaaje? Natamani tupate PM mwanamke halafu awe ni mke wangu nami niwe natanua na jigari lenye nembo kwenye mabaa na misiba. Yaani itakuwa ni full kujiachia.
 
UK waziri mkuu alikuwa mwanamke,mume wake akatumia peni na karatasi za ofisi ya waziri mkuu kwa shuguli zake akatupwa jela miaka kazaa.
Tuombe Waryoba alikumbuke hili ili uwekwe utaratibu wa first ladies na first gents!
 

Mkuu hawa wametumwa na mbwana zao kuja kujibu hoja, lazima magogoni wameshaambiwa kunapost inayowaponda huku. Kunawatanzania wanaotumika kama vijiko, yani kazi yao ni kuhakikisha mafisadi wa rasli mali za nchi zanaliwa ilihali wao na ndg zao wanateseka. Hakuna hasara kama kuwa na ubongo kama wa samaki.
 

....'mabwana' zao ni kiashiria cha inferiority capacity of thoughts....
stick to the rules za jf, jibu hoja kwa hoja...
mama Tunu keshawahi tumia mpaka ndege ya serikali,
it's all about protocol...na hii ipo nchi nyingi duniani,
uwakilishi wa kiongozi. Soma itifaki inasemaje.
 

Umepoteza muda kuandika jibu refu, lakini hujui swali la hoja ni nini; kinachojadiliwa si gari alilokwenda nalo msibani, bali kutumia NEMBO YA TAIFA badala ya namba zingine za kawaida kwenye gari.
 

Kwa maana nyingine kupotea kwa maadili katika utendaji na uvunjaji wa taratibu siyo tatizo la kujadili? Huna habari kuwa yote uliyoyataja yalianza kwa kupuuzwa misingi ya kimaadili katika uwajibikaji?
 
Umepoteza muda kuandika jibu refu, lakini hujui swali la hoja ni nini; kinachojadiliwa si gari alilokwenda nalo msibani, bali kutumia NEMBO YA TAIFA badala ya namba zingine za kawaida kwenye gari.

Nishakujibu kwamba hilo gari lenye nembo limetumika makusudi kuwaonyesha wazi watu kwamba kuna ujumbe wa familia ya PM hapa, hawakukosa shangingi la STK hawa watu wana magari kama wewe ulivyo na suruali labda.

Mwishowe utasema Waziri Mkuu asipande kwenye gari lenye nembo na mkewe, mkewe amfuate nyuma anajiendesha kwenye ki-Datsun.
 
Umepoteza muda kuandika jibu refu, lakini hujui swali la hoja ni nini; kinachojadiliwa si gari oalilokwenda nalo msibani, bali kutumia NEMBO YA TAIFA badala ya namba zingine za kawaida kwenye gari.

umesema nembo ya taifa....na liko kwa wananchi..whats wrong with that??
 
Mama ni VIp na hawezi enda mahali na usafiri tofauti na huo kwa ajili ya usalama wake. Kunamambo mengi makubwa na madogo lakini sio kitu kama hichi. Njaa Gani hizi?

you mean alienda kama deligate wa serikali?au alienda kama mwananchi wa kawaida?
Kwani hana bodygurds pale kwa mzee pinda hamna hata ka rav4 ambako wanakatumia kwa shughuli binafis kama hizi.au kwa kuwa wanatumia mafuta ya bure.
 
serikaali inapokosa jambo la kimaendeleo la kuonesha itashika hadi tawi la mti ...hapo wataenda wote mke wa pinda ,mke wa kiwete, na kiwete mwenyewe....

kimsingi akiwa kwenye shughuli rasmi mke wa waziri mkuu na makamu wana haki ya kutumia nembo yA ikulu kwenye gari...
 

Swali langu ni fupi tu kwako,je yule mama alikuwa anawakilisha serikali pale msibani? Je ile nembo inaruhusiwa kutumiwa na mke wa waziri mkuu,pasipokuepo yeye? Vipi na mtoto au mjukuu wake kesho akilitumia protokali inaruhusu? Swali hapo ni,kwa nini atumie nembo inayotumika kwa viogozi wa juu tu. Swala hapo ni kwamba,aliomba atumie gari la pm,dereva akasaau,au kwa maksudi akaicha nembo.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…