Ni sahihi mume kufungua handbag ya mke wake?

Ni sahihi mume kufungua handbag ya mke wake?

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
58,636
Reaction score
220,426
Vyuma vimekaza sikuhizi wanaume wanafungia handbag kutafuta simu kama ina credit aitumie. Wengine wanatafuta lotion kama ile ya mezani imekwisha anajua wife lazima atakuwa na lotion kwenye handbag.

Wengine wanatafuta pesa ya beer kabisa ile elfu kumi uliyoweka kwaajili ya lunch kesho baba yeyoo ameiwahi.

Hii ni sahihi kweli hata kama nyinyi ni mwili mmoja?
 
Ni sawa tu......hivi kwa mwanamke, kipi ni cha thamani kwake, mwili wake au vitu vyake?
 
Nyinyi ni mwili mmoja pochi na password kitu gani? Mimi Wangu nafungua kila kitu na nikipigika nachukua tu kwa kuwa yeye ni Wangu na kila kilicho chake ni changu
Mimi sishiki simu wala wallet na yeye afanye hivyo hivyo
 
Vyuma vimekaza sikuhizi wanaume wanafungia handbag kutafuta simu kama ina credit aitumie. Wengine wanatafuta lotion kama ile ya mezani imekwisha anajua wife lazima atakuwa na lotion kwenye handbag.

Wengine wanatafuta pesa ya beer kabisa ile Elgin kumi uliyoweka ua lunch kesho baba yeyoo ameiwahi.

Hii ni sahihi kweli hata kama nyinyi ni mwili mmoja?
Dah! Ila wanawake jamani mna roho ngumu mno!
Yani mwanaume kukubebea handbag ni romantic, ila kufungua ni weird?

Mi nnavoona mwanaume asijihusishe kwa namna yoyote na handbag ya mwanamke.
 
Mkishaoana kuna vitu autmatically viko na implied ruhusa. Mfano anaweza akakushika paja bila kukuomba, anaweza kushika nguo zako private na vingine vingi sidhani kama kuna vyenye kwene handabg unamficha so, sioni shida
Nyinyi ndiyo mnaokutana na ARV's huko
 
Back
Top Bottom