Hamza Nsiha
JF-Expert Member
- Jul 25, 2022
- 208
- 191
Leo, nimetenga muda wangu kupitia maoni ya ndugu zangu kuhusiana na changamoto juu ya mabasi yaendayo kasi, ni dhahiri kuwa ni jambo ambalo kwa sasa linahitaji kutiliwa maanani kwa sababu hata mimi leo nime_experience hizo changamoto hadi nikaamua kughairi safari ilihali nilikuwa nmeingia ndani ya kituo nikiwa na dhumuni la kuelekea Kimara kutokea Magomeni mida ya saa kumi na mbili jioni.
Kwangu, ninaweza kusema kuwa kuongeza mabasi ndio suluhisho kuu lakini kwa kuwa kila jambo linahitaji process ikiwemo masuala ya budgeting n.k lakini mamlaka husika ingekuwa ikitoa hata Mrejesho wa mara kwa mara kuhusiana na changamoto hizo.
Kutotoa taarifa, huleta tafsri tofauti tofauti na huibua maswali mengi kwa walengwa kwani hata kama jambo haliwezi kutimia katika siku za hivi karibuni La! Hasha tunahitaji kuhuishwa juu ya upokelewaji wa kero zetu, mikakati iliyowekwa na ni kwa muda gani tunaweza subiri ili tuandae fikra zetu.
Anyway, nmekosa hadi usingizi nikitafakari juu ya 750/=Tsh yangu ambayo imekwenda bure pasipokufanikisha safari yangu.