Zurie
JF-Expert Member
- Jul 6, 2014
- 2,002
- 5,534
Sauti Sol wanasema " Nakuomba Nerea, usitoe mimba yangu weee. Mungu akileta mtoto analeta sahani yake"
Sijui kama ni kweli kila mtoto anakuja na 'sahani' lakini naomba tudiscuss usahihi wa kutumia hii dhana katika kufanya maamuzi ya kuzaa. Najua mtoto akishazaliwa ataishi tu anyhow lakini naona kuzaa bila mipangilio au uwezo wa kumpa mwanao a good life ni kumdhulumu.
Mama yangu mdogo ana watoto sita. Mdogo tu hata 35 hajafika lakini ashajifungua watoto sita na hadi sasa hana pa kuishi kwahiyo anatangatanga kwa wanaume. Watoto amewagawa, wawili kwetu mmoja kwa bibi na wengine watatu kwa shangazi zao.
Anajua kuwa hajaolewa, kwanini anaendelea kubeba mimba ambazo anajua hataweza kutunza watoto? Sawa watoto wataendelea kuwa hai lakini kisaikolojia, kimalezi ashawaweka pabaya.
Mungu alisema tuijaze dunia, je hatuna wajibu wowote wa kutimiza kabla ya kuijaza au tujaze tu tukitumaini watakuja na 'sahani'?