Ni sahihi kunywa dawa na maziwa mgando (mtindi)?

Wakuu kwema?

Ni sahihi mtu kunywa dawa (Vidonge)na akatumia maziwa mgando?

Asanteni
Kwa ujumla, hakuna madhara yanayojulikana ya kunywa maziwa mgando wakati unatumia dawa. Mtindi una virutubisho vingi, kama vile kalsiamu, protini, na bakteria hai, ambayo inaweza kuwa na faida kwa afya yako.
 
Kwa ujumla, hakuna madhara yanayojulikana ya kunywa maziwa mgando wakati unatumia dawa. Mtindi una virutubisho vingi, kama vile kalsiamu, protini, na bakteria hai, ambayo inaweza kuwa na faida kwa afya yako.
Asante sana mkuu
 
Kwa ujumla, hakuna madhara yanayojulikana ya kunywa maziwa mgando wakati unatumia dawa. Mtindi una virutubisho vingi, kama vile kalsiamu, protini, na bakteria hai, ambayo inaweza kuwa na faida kwa afya yako.
Ndugu unammislead mleta mada

Hutakiwi kutumia maziwa ya aina yeyote unapokuwa kwny dozi, maziwa yanaua nguvu ya dawa kufanya kazi
 
Inategemea ni dawa gani, dawa nyingine hamna athari....kwa maelezo zaidi muone daktari
 
Wakuu kwema?

Ni sahihi mtu kunywa dawa (Vidonge)na akatumia maziwa mgando?

Asanteni
Kagamee kwani wee masai, maana wale jamaa maziwa ni kila kitu kwao, hata kuoga wanaweza kuongea. Anyway, dawa chache sana zinazuiliwa kutumia maziwa na ukipewa hizo lazima utaambiwa na mtoa huduma au utakuta maelezo kwenye bango kitita (karatasi ya maelezo ndani ya boksi la dawa), nyingi ya dawa tunazotumia kwenye maisha ya kila siku hazina shida na maziwa. Na hata hizo zenye muingiliano na maziwa, mara nyingi ukitumia masaa mawili kabla au baada ya kumeza dawa, nayo hakuna shida, kwenye dawa za sindano nadhan ndo hakuna kabisa zuio la kutumia maziwa labda uwe na sababu specific sana au maziwa yenyewe kama ndo chanzo cha ugonjwa wako, vinginevyo maziwa yana faida nyingi sana mwilini mwako kuliko hasara, ni protein ya kutosha kabisa kwa lishe yako na familia yako hasa watoto chini ya miaka mitano, nchi yetu pamoja na kuzalisha maziwa mengi tuna matumizi hafifu ya maziwa, karibu ni wa mwisho Africa mashariki, sasa tuache visingizio, tutumie maziwa kwa wingi, kwa afya zetu.
 
Ndugu unammislead mleta mada

Hutakiwi kutumia maziwa ya aina yeyote unapokuwa kwny dozi, maziwa yanaua nguvu ya dawa kufanya kazi
Hii research uliifanyia wapi mkuu? Huu ni upotoshaji.

Kikubwa ni kuwa kuna aina za dawa haitakiwi kunywa na mazima kwasababu ya reaction zake. Ila sio kwasababu maziwa yatapunguza nguvu ya dawa.
 
Kagamee kwani wee masai, maana wale jamaa maziwa ni kila kitu, hata kuoga wanaweza kuongea. Anyway, dawa chache sana zinazuiliwa kutumia maziwa na ukipewa hizo lazima utaanbiwa na mtoa huduma au utakuta maelezo kwenye bango kitita (karatasi ya maelezo ndani ya boksi la dawa), nyingi ya dawa tunazotumia kwenye maisha ya kila siku hazina shida na maziwa. Na hata hizo zenye muingiliano na maziwa, mara nyingi ukitumia masaa mawili kabla au baada ya kumeza dawa, nayo hakuna shida, kwenye dawa za sindano nadhan ndo hakuna kabisa zuio la kutumia maziwa labda uwe na sababu specific sana au maziwa yenyewe kama ndo chanzo cha ugonjwa wako, vinginevyo maziwa yana faida nyingi sana mwilini mwako kuliko hasara, ni protein ya kutosha kabisa kwa lishe yako na familia yako hasa watoto chini ya miaka mitano, nchi yetu pamoja na kuvalisha maziwa mengi tuna matumizi hafifu ya maziwa, karibu ni wa mwisho Africa mashariki, sasa tuache visingizio, tutumie maziwa kwa wingi, kwa afya zetu.
Mtutsi na mqziwa ni mapacha mkuu
 
Wakuu kwema?

Ni sahihi mtu kunywa dawa (Vidonge)na akatumia maziwa mgando?

Asanteni

Kuna maswali mawili ndani ya swali moja:
1: Kunywa dawa na baadaye kunywa maziwa.
2: Kunywa dawa kwa kutumia maziwa.

Jibu ni:
Inategemea aina ya dawa:
1: Kuna dawa kulingana na zilivyotengezwa na vilivyomo, zinayeyuka vyema kwenye maziwa. Hivyo, hurahisisha dawa kufyonzwa na kuingia mwili.

2: Kuna dawa kwa jinsi zilivyotengenezwa na vilivyomo, vikikutana na maziwa hutengeneza mchanganyiko ambao mwili hauwezi kufyonza dawa husika. Hivyo, dawa nyingi hupitiliza na kufanya lengo la dawa kutofikiwa.

Mtoa huduma ya afya huweza kushauri, dawa hii ukitumia kunywa maziwa ni jambi jema au usinyewe maziwa unapotumia dawa hii.

Kwa msingi huo, usimpe mtu maziwa kama amekunywa sumu iwapo hujui SUMU husika INAYEYUKA vyema kwenye maziwa. Maana badala ya kumuokoa unaweza KURAHISISHA KIFO kwa kusababisha sumu kufyonzwa vyema.
 
Back
Top Bottom