Kina mama, japo kwa uchache waambieni watoto wenu wema wa baba zao

bakundande jr

JF-Expert Member
Oct 22, 2021
507
670
Kwa kuanza nianze kuwasalimi wadau wote wa jamii forum. Amani iwe juu yenu/Assalam aleykum kwenu nyote mabibi na mabwana.

Kwa muda mrefu na mara nyingi katika familia zetu kina mama hukaa muda mwingi na watoto wao kuliko kina baba ambavyo hukaa nao, hii inatokana na utekelezaji wa majukumu mbalimbaili ya kijamii na kiuchumi.

Hali hii hupelekea watoto kujenga urafiki sana hasa na kina mama, hufikia hatua mtoto akiwa na shida yoyote huanza kumueleza mama kabla ya baba na wakati mwingine huogopa kabisa kumweleza baba yake shida alionayo na kupelekea kina mama kuwa kama daraja la mawasiliano baina ya baba na mtoto.

Sisemi ni jambo baya ila mara nyingi kina mama wengi hutumia nafasi hiyo kujikweza kwa watoto na kuficha uwajibikaji wa waume zao wakati wa kutatua shida za watoto. Mfano unakuta mtoto kaomba pesa kwa ajiki ya manunuzi ya vifaa vya shule ama matumizi mengine bila kuficha mama humwambia mumewe kuwa kijana wetu anashida hizi.

Cha ajabu baba akitoa pesa ni kina mama wachache ambao huweza kusema hii pesa baba yako katoa kwa ajili yako. Kitu pekee ambacho kina mama wengi huwaambia watoto kuhusu baba zao ni "SUBIRI BABA YAKO ARUDI" hii ndio huwa kauli inayotolewa na kina mama pale tu mtoto anapokosea.

Jambo hili hupelekea watoto kuona baba zao kama mahakama. Na kupelekea watoto wengi kutokuwa na mapenzi hasa kwa baba zao.

Kwenu kina mama sio kosa kumwambia mwanao mame na mazuri ya baba yake ili kudumisha upendo baina ya baba na mtoto.
 
Nitawaambia mazuri ya baba yao wanangu...

Japo mimi niliambiwa mabaya mpaka baba yangu anakufa namjua kwa mabaya...

Nilikuwa nikimuona baba naona kama kituo Cha polisi...

Kumbe kulikuwa na ya nyuma nisiyojua...

Na alishakufa siwezi muona tena...

Mungu nisamehe mimi...
 
Na mara nyingi mtoto hujua mema ya baba pale akianza kujitegemea
 
Umeandika jambo la maana na lenye ukweli 95%.

Kina mama wakizingatia hayo patakuwa na balance ya baba na mama kwenye makuzi ya mtoto.

Naunga mkono hoja yako
Yaan nimejikuta naadika hivi haada ya kuangalia ngoma ya ney wa mitego ft linah
 
Hili limenitesa sana miaka mitatu nyuma.
Lakini haya ni makosa ya kutengeneza
 
Mkuu umewaza vyema.
Mama zetu wamepanda mbegu mbaya kwa watoto kuhusu baba zetu.

Unahitaji akili na hekima sana kujua thamani ya baba.

wanaume hatuna tabia ya kuwasemea vibaya wanawake kwa watoto wetu. Kinyume na wanawake.

Baba baba baba
Sema kiasi flani inabidi kina baba japo watenge mda mfupi japo kuongea na watoto wao hii inaweza saidia
 
Wababa kuweni karibu na watoto wenu hata kama upo busy kiasi gani tafuta nafasi. Wema unajionyesha wenyewe sio lazima mama aseme...
Tumeishi tukiona wema wa baba zetu hata mama hakuwahi kutuambia. Tulikuwa tunaona wenyewe.

Sasa wewe kaa hapo usubiri mkeo awahadithie watoto wema wako, kiukweli utasubiri sana.
 
Nitawaambia mazuri ya baba yao wanangu...

Japo mimi niliambiwa mabaya mpaka baba yangu anakufa namjua kwa mabaya...

Nilikuwa nikimuona baba naona kama kituo Cha polisi...

Kumbe kulikuwa na ya nyuma nisiyojua...

Na alishakufa siwezi muona tena...

Mungu nisamehe mimi..

Ata Mimi inaniuma Sana..Mama yetu alifanya baba yetu akawa mbali na sisi..nikimkumbuka dingi naumia Sana..endelea kupumzika kwa Amani BABA..HALIKUWA KOSA LETU WANAO...
 
mimi nimejifunza/nimeujua wema wa baba yangu kwa kuuona mwenyewe bila kuambiwa na mama,,,,ingawa baba alikuwa mtu wa kusafiri lakini akirudi nyumbani anatupa muda anakuwa karibu na sisi kiasi akiondoka ni huzuni,,,,hivyo kwa mtazamo wangu wema au uzuri wa baba sio lazima usemwe na mama unajionesha wenyewe
 
Nitawaambia mazuri ya baba yao wanangu...

Japo mimi niliambiwa mabaya mpaka baba yangu anakufa namjua kwa mabaya...

Nilikuwa nikimuona baba naona kama kituo Cha polisi...

Kumbe kulikuwa na ya nyuma nisiyojua...

Na alishakufa siwezi muona tena...

Mungu nisamehe mimi...
ndio maana hata katika maisha ya kawaida tunaaswa kutobeba jumla maneno ya kuambiwa.

hilo la kuambiw baba yako hivi,baba yako vile inatakiwa upuuze kwanza ufike ukutane naye mwenyewe uone ana ladha ipi.
 
Ukiwa mtoto huwezi kupuuza...

Na ndio hapo wamama wanapowapata watoto wao...

Maana wanajua hawanauwezo wa kuchuja maneno wanayoambiwa...
 
Kwa kuanza nianze kuwasalimi wadau wote wa jamii forum. Amani iwe juu yenu/Assalam aleykum kwenu nyote mabibi na mabwana.

Kwa muda mrefu na mara nyingi katika familia zetu kina mama hukaa muda mwingi na watoto wao kuliko kina baba ambavyo hukaa nao, hii inatokana na utekelezaji wa majukumu mbalimbaili ya kijamii na kiuchumi.

Hali hii hupelekea watoto kujenga urafiki sana hasa na kina mama, hufikia hatua mtoto akiwa na shida yoyote huanza kumueleza mama kabla ya baba na wakati mwingine huogopa kabisa kumweleza baba yake shida alionayo na kupelekea kina mama kuwa kama daraja la mawasiliano baina ya baba na mtoto.

Sisemi ni jambo baya ila mara nyingi kina mama wengi hutumia nafasi hiyo kujikweza kwa watoto na kuficha uwajibikaji wa waume zao wakati wa kutatua shida za watoto. Mfano unakuta mtoto kaomba pesa kwa ajiki ya manunuzi ya vifaa vya shule ama matumizi mengine bila kuficha mama humwambia mumewe kuwa kijana wetu anashida hizi.

Cha ajabu baba akitoa pesa ni kina mama wachache ambao huweza kusema hii pesa baba yako katoa kwa ajili yako. Kitu pekee ambacho kina mama wengi huwaambia watoto kuhusu baba zao ni "SUBIRI BABA YAKO ARUDI" hii ndio huwa kauli inayotolewa na kina mama pale tu mtoto anapokosea.

Jambo hili hupelekea watoto kuona baba zao kama mahakama. Na kupelekea watoto wengi kutokuwa na mapenzi hasa kwa baba zao.

Kwenu kina mama sio kosa kumwambia mwanao mame na mazuri ya baba yake ili kudumisha upendo baina ya baba na mtoto.
Wema siku zote unaonekana hata usipo sifiwa,tengeneza connect nzur na watoto wako ww mwenyewe usikae kusubiria mkeo ndio akusemee kwa watotot labda Kama haupo hai.Yeye unaye subir awaeleze wanao wema wako hata yeye anatumia nafasi yake kuwaaminsha watoto yeye n bora zaidi,asa ww kaa tu utegemee mkeo ndio aanze kuadisia watoto wema wako.
 
Matendo yananena zaidi ya Maneno.

Timiza wajibu wako Kama baba kwa asilimia zote na ziada.

Wakati ukihitaji kutambulika mchango wako kwa watoto wako, ukumbuke Pesa inaweza kununua kila kitu lakini Pesa sio kila kitu na Pesa sio mbadala wa upendo na matendo ya upendo.

Unaposhindwa kutimiza wajibu wako hata kwa sekunde moja tu, tayari unatoa nafasi kwa yeyote kusimama kwenye nafasi yako ama kuchukua uhusika wako kwenye maisha ya watoto wako.

Wape watoto wako muda wako na elimu ya kujitambua kutoka kwako wewe maana wewe ndio muumbaji wao hapa duniani.

Wanawake wengi wanafanikiwa kuwa na support ya watoto wao kwasababu wanaume wanadhani malezi na makuzi ya watoto yanategemea Pesa pekee.

Malezi ya watoto ndani na nje ya ndoa yanahitaji uivue Ego yako, ushuke chini level ya watoto wako ili uwaelewe na wao wakuelewe.

Ni rahisi kumkuta mtoto anataniana na mama yake kwa sababu tangu kuzaliwa kwake mama amemfanya ni mwenzake na kila kitu chake.

Ni ngumu kumkuta mtoto anataniana na baba yake kwa sababu tangu kuzaliwa kwake baba anamuhesabu mtoto Kama sehemu ya ‘mali’ zake na sio binaadam mwenzake.

Malezi ya watoto ni jukumu la wote wawili, baba na mama.

Na malezi hayo sio kula, kunywa, kuvaa, kusoma na kulala pekee.

Malezi hayo ni kuyaishi maisha haya sasa hivi sambamba na watoto wako.

Wape nafasi ndani ya maisha yako. Wafanye wawe sehemu ya maisha yako kila sekunde ya uhai wako.

Mtoto wako ni wewe mwenyewe wa baadae. Iwe wa Kike ama wa kiume, ni wewe katika nyakati zijazo.

We don’t inherit the Earth from our ancestors, we borrow it from our Children.
 
Back
Top Bottom