Ni sahihi kuingia kwenye mahusiano mengine kwa haraka?

elyza

Senior Member
Joined
Oct 9, 2016
Posts
155
Reaction score
329
Hbr za weekend wakuu!

Tangu nimeamua kuachana na mchumba wangu kwa sabbu ya fumanizi kama nilivyoeleza kwenye uzi wa awali nimekuwa ktk wakati mgumu sana.

Tangu nimetupia humu uzi wa kumfumamia mchumba wangu nimekuwa nikipokea PMS nyingi za kutaka mahusiano na mm.

Mtaani pia wanaume wengi wanaojua kuwa nimeacha na mchumba wangu hawaishi kinifuatilia.

Kazini pia nafuatiliwa mpaka kero.

Binafsi sipendi kuingia kwenye mahusiano kwa haraka kwani naweza kosea kwenye kuamua kwangu.

Je naweza jipotezea muda kwa kutokufanya maamuzi ya haraka?

Wakuu naomba ushauri wenu kwenye hili natatizika ukingatia Nina 28 years sasa.
 
Ushauri wangu kwako,jipe muda wakutosha hata miezi 3 mpaka 6.
Screenshot_2016-10-23-14-19-47.png
 
Ni vyama kupima kina cha maji kabla hujaamua kuvuka.

Fanya uchunguzi wa kutosha juu ya mtu ambaye unahitaji kuwa na uhusiano nae kabla hujajiingiza rasmi ili badae usijute.
 
Asante kwa ushauri wako mkuu
 
Wewe kila kitu unaomba advise inaonyesha you are not strong emotionally. Fanya maamuzi kwa akili yako mwenyewe mawazo ya wengine ni opinions tu. Kwenye relationship kamwe huwezi predict future itakueaje dunia sasa hivi mambo yanaenda haraka sana kuwa smart bila kusikia watu wanashauri nini hasa.

Ukweli nikwamba kila mtu atakuumiza tu HATA UKIAMUA KUSUBIRIA HADI MWAKANI mkuu. Chagua mpenzi/mchumba unayedhani utaweza KUVUMILIA chochote kitakachotokea huko mbele. Usiwe "jinga" kama huko nyuma aliweza kumpenda mtu tofauti na wewe halafu wakaachana basi huna budi kukubali ANAWEZA akakuacha hata wewe tena. Usipojiandaa psychologically kwa hili utabadi kulialia tu mkuu.

Mtu sahihi wakumkabidhi MOYO WAKO ni wewe mwenyewe tu.
 
Ukweli mchungu mleta mada hawezi kukushukuru kwa ushauri sahihi uliompa
 
Binti wa miaka 28 inabidi uolewe sasa!..upo wapi mrembo
 
Wewe kila kitu unaomba advise inaonyesha you are not strong emotionally. Fanya maamuzi kwa akili yako mwenyewe mawazo ya wengine ni opinions tu. Kwenye relationship kamwe huwezi predict future itakueaje dunia sasa hivi mambo yanaenda haraka sana kuwa smart bila kusikia watu wanashauri nini hasa.

Ukweli nikwamba kila mtu atakuumiza tu HATA UKIAMUA KUSUBIRIA HADI MWAKANI mkuu. Chagua mpenzi/mchumba unayedhani utaweza KUVUMILIA chochote kitakachotokea huko mbele. Usiwe "jinga" kama huko nyuma aliweza kumpenda mtu tofauti na wewe halafu wakaachana basi huna budi kukubali ANAWEZA akakuacha hata wewe tena. Usipojiandaa psychologically kwa hili utabadi kulialia tu mkuu.

Mtu sahihi wakumkabidhi MOYO WAKO ni wewe mwenyewe tu.
Mkuu sina pakusemea zaid ya hapa..sijawahi kuwa na stress kwa kiwango hichi ..ndiyo maana unaona natafuta soln si kwamba siwezi amua mwenyewe ila natafuta hekima za wengine then nichanganye na za kwangu.
 
Chukua mda wakutosha kupumzika,wanaume ndio hao hao na hawaishi subiri ili upate mwanamme mwenye afadhali..
 
Mkuu sina pakusemea zaid ya hapa..sijawahi kuwa na stress kwa kiwango hichi ..ndiyo maana unaona natafuta soln si kwamba siwezi amua mwenyewe ila natafuta hekima za wengine then nichanganye na za kwangu.
Sawa endelea kupokea ushauri
 
Embu tulia kwanza... jipe muda.
Ni sahihi kinachokutesa wewe ni upweke na yale mazoea ya kuwa nae. Ukikurupuka hapo utaangukia pabaya zaidi. Jiweke bize.. jichanganye na marafiki.. Muombe Mungu sana.. maana yeye ndie anayejua nani anakufaa
 
Aaah mabazazi washaanza kukumendea......
Wanasukumwa na uzoefu kuwa kipindi kama hiki utakuwa lonely na desperate.....
Kuwa makini
 
je una kazi? kama una kazi unataka mwanaume wa nini? na kama hauna kazi tafta shughuri ya kufanya ikusaidie kama ukiendelea kumtegemea mwanaume mpaka akupe hela basi utaendelea kumwagwa maisha yako yote
 
Kifupi ninakazi tena inanitosha kbsa , ila tambua kwamba kazi ina nafasi yake na mume ana nafasi yake.
 
Back
Top Bottom