Chizi Fureshi
JF-Expert Member
- Oct 26, 2010
- 1,718
- 459
Well, nimeuliza na hapa chini nitapitia mawazo ya wachangiaji. Wakati wa Mwalimu alisimama na kutetea Ujamaa na Kujitegemea. Mzee Mwinyi, tunakumbuka na hasa wengi wetu alivyofungua milango ili kuimarisha Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea. Zama za Uwazi na Ukweli enzi za Ben zililenga kuijenga imara taswira ya TANZANIA katika awamu tangulizi. Jakaya amehanikiza mengi na kuiimarisha nchi; inafikika na ndiyo maana tunatakiwa kufanya kazi ili tutoke hapa tulipo. Nasema tena HAPA KAZI TU. Bahati mbaya miluzi imeanza tayari tena kwa sura mbalimbali, ukichagiza na hili la MCC ndo kila mtu ana lake. Mengi yako humu JF na bahati mbaya mmeanza kuchanganya na uwezo wa baadhi ya wateule. Finally......Mnataka Rais wa aina GANI?