Ni packaging, hujuma au ukwepaji kodi?! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni packaging, hujuma au ukwepaji kodi?!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by NasDaz, Apr 13, 2010.

 1. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #1
  Apr 13, 2010
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280
  Nazungumzia sabuni za unga ambazo hivi sasa zimeenea uswahilini kwetu. Sabuni za unga hizi ni tofauti katika packaging ukilinganisha na packaging iliyozoeleka ya sabuni za unga. Packaging iliyozoeleka tangu enzi za Mwalimu( na duniani kote kwa ujumla) ni ile ambayo unakuta sabuni ipo kwenye paketi safi yenye nembo na mbwembwe za kila aina! Ukiangalia tu, utajua kwamba ni FOMA, OMO, na zingine sawa na hizo. Hata hivyo, hivi sasa Uswahilini kuna sabuni za unga ambazo zinafungwa manuaaly kwenye mifuko isiyo na nembo yoyote. I guess, huko zinakotoka, sabuni hizi ama zinauzwa kwa kilo au njia nyingine sawa na hiyo halafu wanaonunua ndio wanazifunga kwenye mifuko sawa na maji maarufu kama MAJI YA KANDORO!! S asa, swali langu ni kwamba, je nini chanzo cha sabuni hizi ambazo zinaonekana hazikuw-packed viwandani? Ni wafanyakazi wanaiba kabla hazijakuwa packed na wao kuziuza mitaani(HUJUMA);N I new style of packaging toka viwandani; au NI UKWEPAJI KODI?! Suala kwamba ni njia ya ukwepaji kodi, ndio HOFU YANGU KUU! Ikumbukwe kwamba, sabuni hizi hivi sasa zinauzika zaidi Uswahilini kuliko sabuni zilizokuwa packed! I guess, zinauzika hata mara mbili zaidi ya zile sabuni geneuine! Sasa je, hii sio janja ya wafanya biashara wakwepa kodi ambao wana-amua kwa makusudi kuto-pack hizi sabuni na kuwauzia mawakala wao ambao nao wanaziuza ktk njia hii? Hivi kweli sabuni hizi zipo kwenye accounting books za viwanda husika? Na kama ni Hujuma, mbona sijasikia wenye viwanda vya sabuni wakilalamikia hali hii ambayo inaua soko la sabuni zilizokuwa packed viwandani?
   
Loading...