Ni njia gani bora kabisa ya kukwepa kulipa nauli katika daladala?

Tembea tu kwa miguu mkuu hutambugudhi mtu na wala hutamdhulumu mtu,hakika hata kwa Muumba hutakuwa na dhambi. Zaidi ya hilo ni udhalimu tu
 
Njia bora nikuhifadhi risiti za daladala,halafu unakaa unajifanya unachati huku una risiti moja mkononi, konda akiona risiti anafikiri ulishalipa mda, hii ni njia rahisi, au unaweza ukawa umepanda na mtu anayeshuka mapema akakuachia risiti yake halafu utaionesha pale itakapohitajika.....
Kazi ni kwako
Kuna jamaa aliumbuka eti nimelipa tayari wskati konda ndio ananza kukusanya.
 
Sasa Siyo Siri Tena Kuwa Maisha Yamekuwa Magumu Ambapo Kama Usipokuwa Mbunifu Unaweza Kujikuta Hela / Pesa Yako Yote Ya Mshahara Unagawana Na Makondakta Na Kuishi Maisha Magumu Sana.

Hivyo Binafsi Nimetafakari Sana Na Nimeona Kuwa Inabidi Nijiongeze Ili Maisha Yaende Sawa Nimeamua Sasa Rasmi Kuwa Mbunifu Kwa Kukwepa Kulipa Nauli. Tafadhali Kama Kuna Member Yoyote Yule Mwenye Ujuzi Mbadala Wa Kunifanya Niweze Kuwakwepa Makondakta Katika Kuwalipa Nauli Zao au Kuchengana Nao Mule Mule Ndani Ya Basi Anisaidie Na Nitamshukuru Mno.

Kila Siku Najitahidi Kuwakwepa Lakini Wananishtukia Tu.
[/QU OTE]
Ndugu yangu Gentamycine mbona sikuelewi? Humu jamvini mnalalamika sana kuhusu majibu ambayo bado hayajatumbuliwa. Mnalalamikia uzembe, rushwa, matumizi mabaya ya fedha za umma vile vile mnazungumzia uadilifu na uaminifu kama taifa. Hizi ndiyo zimekuwa ngonjera zetu. Sasa wewe huoni kwa kufanya hivyo unajiingiza kwenye kundi la majipu? au malalamiko yetu yanatokana na kuwaonea wivu wale ambao wako jikoni na kutamani nasi tungepata nafasi hizo ili tule? Unachokifikiria hapa ni yale tunayoyapiga vita. Ushauri wa bure. kama kweli maisha ni magumu basi tuache vijumba hasara, tupunguze anasa na kula misosi ya mchana kwa bei za hatari wakati nyumbani tunaacha buku 2 ili hiki kidogo tunachokipata tuweze kutumia vizuri pamoja na familia zetu.
 
hakuna haja ya kusubir ID ya makonda wala nn,simple tupanda daladala ilovaaa full jitahd ukae upande wa drisha konda atakusanya nauli nauli,after then mbishie huku ukiwa na macho makavu kabsa kwamba nshakupa nauli,bisha kabisa kwamba ulikuw umesimama then ukapata siti baada ya abiria kushuka,mpaka hapo utasafiri bure tu ,otherwise NEVER TRY THIS AT HOME
 
Mbona simple tu kaka tafuta begi dogo la mgongoni hakikisha ndani yake kuna nguo unazovaa siku hiyo tafuta yale matambala yaliyochanika chanika tena hakikisha yana matobo hadi kwenye matako ukipanda daladala mda wwte vaa hayo kwanza ukifika unakokwenda jifiche sehemu badilisha vaa nzuri
 
Ongeza bidii nje ya mshahara wako ili nauli ya Daladala isiwe mtihani kwako.

Kukwepa tatizo si njia sahihi ya kutatua tatizo, bali kukabiliana na tatizo ndio njia sahihi
 
Njia bora nikuhifadhi risiti za daladala,halafu unakaa unajifanya unachati huku una risiti moja mkononi, konda akiona risiti anafikiri ulishalipa mda, hii ni njia rahisi, au unaweza ukawa umepanda na mtu anayeshuka mapema akakuachia risiti yake halafu utaionesha pale itakapohitajika.....
Kazi ni kwako
Labda sio kwa makondakta hawa wa Mbagala au Gongo la mboto
 
Back
Top Bottom