Ni nini wanawake humaanisha wanaposema wanahitaji 'Real man'

Royal Son

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2016
Posts
1,467
Reaction score
2,760
NINI WANAWAKE HUMAANISHA WANAPOSEMA WANAHITAJI "REAL MAN" [ MWANAUME WA KWELI ]?

Hii sio kauli ngeni kwa wanawake kusema wanahitaji "real man", huwa unawaelewa? Real man kwa wanawake haimaanishi ile maana ambayo dunia tunaijua, wao wana maana yao.

Bro ukiona mwanamke anakuita "real man" basi hesabu maumivu. Tuone nini huwa wanamaanisha wanapotamka hilo neno "real man".

1. Kwa mwanamke real man ni yule mwanaume ambaye hana shida mkewe kutoka bila kuaga na kwenda kusikojulikana na hata akachelewa kurudi nyumbani.

2. Kwa mwanamke real man ni yule mwanaume ambaye hana shida mkewe akawa anawasiliana na ma x zake.

3. Kwa mwanamke real man ni yule mwanaume ambaye hana shida mkewe anapotumia pesa hovyo.

4. Kwa mwanamke real man ni yule mwanaume ambaye hana shida mkewe kwenda kwao mara kwa mara tena bila sababu za msingi.

5. Kwa mwanamke real man ni yule mwanaume ambaye hamgombezi anapokosea tena kusudi kabisa.

6. Kwa mwanamke real man ni yule mwanaume anayeelewa hata anapomkuta katika mazingira tata na mwanaume mwingine.

7. Kwa mwanamke real man ni yule mwanamke ambaye hawezi kumkataza chochote.

8. Kwa mwanamke real man ni yule mwanaume ambaye anaruhusu rafiki za mke wake wawe na nguvu kwa mke wake kuliko yeye.

9. Kwa mwanamke real man ni yule mwanaume anayemtawala, yani mwanaume hasemi kitu kwa mkewe.

10. Kwa mwanamke real man ni yule mwanaume ambaye yeye sio mwenye maamuzi ya mwisho pale nyumbani.

Kwa kifupi mwanamke anaposema mwanaume wake ni real man, au akasema mwanaume wake ni muelewa, basi jua huyo mwanaume ni bwege, huyo mwanaume ametawaliwa, huyo mwanaume hana mamlaka juu ya mkewe,huyo mwanaume hana misimamo, hicho ndicho wanawake wanachomaanisha.

Lakini unamuona mwanamke anakwambia mimi mme wangu mtata kishenzi, anatumia tu hiyo kauli kutia huruma ila anachojaribu kukwambia ni kwamba mume wangu hataki ujinga, anajaribu kukwambia mume wangu ana misimamo, anataka kukwambia kwamba mume wangu amenyooka.

Nikupe mfano mmoja hapa ambao utabeba hayo maelezo yote hapo juu;

Fikiria kwamba una demu wako, ambaye anaishi na wazazi wake, halafu hiyo siku akakuja kwako anakwambia "mimi hata nikilala hapa nikarudi asubuhi nyumbani poa tu, baba yangu hana shida". Hivi huyo mzazi ni kweli hana shida kuacha binti yake ambaye hajaolewa kulala nje au ni mzazi mpumbavu na asiyejielewa?

Kwahiyo mwanamke anapokwambia mwanaume wake hana shida, muelewa unatakiwa kujua huyo mwanaume ni bwege, anapelekeshwa tu, na wanawake wanapenda kweli wanaume wa aina hiyo. [ Mwanaume

Credit: Stanslaus Simon Masiva
 
Fikiria kwamba una demu wako, ambaye anaishi na wazazi wake, halafu hiyo siku akakuja kwako anakwambia "mimi hata nikilala hapa nikarudi asubuhi nyumbani poa tu, baba yangu hana shida".
Napenda mwanamke wa hivi, wale wenye tabia za kilokolelokole ndio wabaya hata kuwaangalia, huwezi kuwafikiria vibaya ila wanayoyafanya ukija kujua utasaga meno. Sitaki mwanamke mwenye kujifanya ana tabia za Malaika kumbe ni Shetani kwenye umbo la Malaika.
 
Oyaa unajiita real man huku unashindia tende kama adriz Na Lucha ?

Real man ni kama Yule padre alizama chaka akawa anakula karanga na miti shamba.
Padre Nikata kaongoza sala miaka mingi tunaamini hawajawahi kula mzigo kumbe Padre ana pisi yake anachapa taratibu na anaihudumia kwa miaka 9, pisi imemtema mwamba kaamua ajiteke ajichimbie pori kavaa na boshori ili tusimtambue
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…