Ngonepi
JF-Expert Member
- Jun 2, 2013
- 1,872
- 1,200
Wanajamvi nimetumia muda mwingi kutafakari ni kwa nini sisi watu weusi tunabaguliwa na Wazungu pamoja na kabila zingine zisizo za kiafrika, na bado sijapata majibu kwa kweli.
Tuliona ubaguzi Afrika ya kusini na mataifa mengine hapahapa afrika yenye mchanganyiko wa weusi na jamii ya watu wengine,
Nchi za magharibi Amerika na ulaya vivyo hivyo hali ni mbaya kwa mtu mweusi, tatizo letu ni nini? Tuna nini kisichowafurahisha au kuwaudhi kwenye ngozi yetu!!
Nchi kama Urusi hali ni mbaya zaidi, ukipata simulizi za waafrika wishio Urusi jinsi wanyanyasavyo ni mbaya mbaya kabisa, waafrika wanajeruhiwa hata kwa vitu vyenye ncha kali kwa sababu tu ya ngozi yao!
Mbaya zaidi hata uzaliwe na mzazi mmoja mweupe na mwingine mweusi bado hali ni mbaya tu kwako.
Tuna nini sisi waAfrika!!? Tumekosewa wapi? Hapa afrika tunaishi na kila jamii kuanzia Wazungu, Waarabu, wachina, wahindi na jamii nyingi nyigine na hatuwabagui! Tuna nini sisi?
Kwa mnofahamu nini kinasababisha ubaguzi huu tufanyiwao nawaomba Elimu tafadhali, maana naogopa hata kusafiri!!.