Ni nini kiliwasibu Dar Chat ?

Ni nini kiliwasibu Dar Chat ?

mamenrevy

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2014
Posts
583
Reaction score
351
Wana bodi Heshima yenu.

Hapo zaman za kale, kabla ya kushamiri kwa mitandao mbali mbali ya kijamii kama FB Twiter JF na mingine mingi, palikuwa na mtandao unaitwa Darchat wenyeji wa mjini mtakuwa mnaukumbuka.

Nataka kufahamu 1. Nani alikuwa mwanzilishi? founder. 2. Nini kiliwasibu mbona wamepotea kwenye mtandao.

Bila shaka kama wangekuwepo mpaka lei uenda wangekuwa juu kuliko JF.
 
Umenikumbusha long sana mkuu ulianza kama chatroom ukiingia kuna picha ya mvulana na msichana wamekaa kwenye bembea then unaweka any username unazama kwenye chatroom bila kusahau imabidi computer iwe installed na java software ili uweze kuchat.
Later wakaugeuza kama dating site ukawa na rangi ya damu ya mzee ikawa lazima ujisajiri. Scammers wa mtandao wakahamia kule full picha za mademu wakali kumbe fake.
Ulikuwa unaitwa marafiki.com au darchat.com vyovyote utakavyoandika una directiwa huko.
Nahisi walikosa wadhamini wakashindwa endelea uendesha kwa maana kuna kipindi walishindwa lipia hata hosting.
Mitandao mingi ilikufa mfano kilikuwa na ule wa ipp ukijulikana kama darhotwire, kulikuwa na mzibo.net.
Kitambo sana miaka ya 2004 huko
 
Na yahoo messenger video calls umeweka mahedifoni makuubwa kichwani.
Yahoo messenger kulikuwa na chatroom moja inaitwa Britney spears nilikuwa naipenda sana hiyo chatroom nachat na waarab na wahind kila dem namtongoz way back 2004
 
Jamii forums bado watu wengi hawaujua huu mtandao, ila kila anayekaa na mimi najaribu kuwashawishi watumie jamii forums takribani watu 25 hadi sasa wanatumia jamii forums. [emoji4] [emoji106]
 
Watu walikuwepo ila technology ya internet ilikua inaonekana ni ya watu wa tabaka fulani, accessibility ilikua sio rahisi as of today and expensive,ndio maana haijulilani na wengi hii thread hapa, leo smartphone umebadili situation, in every 10 ppl, 8 wana Internet access
 
Umenikumbusha long sana mkuu ulianza kama chatroom ukiingia kuna picha ya mvulana na msichana wamekaa kwenye bembea then unaweka any username unazama kwenye chatroom bila kusahau imabidi computer iwe installed na java software ili uweze kuchat.
Later wakaugeuza kama dating site ukawa na rangi ya damu ya mzee ikawa lazima ujisajiri. Scammers wa mtandao wakahamia kule full picha za mademu wakali kumbe fake.
Ulikuwa unaitwa marafiki.com au darchat.com vyovyote utakavyoandika una directiwa huko.
Nahisi walikosa wadhamini wakashindwa endelea uendesha kwa maana kuna kipindi walishindwa lipia hata hosting.
Mitandao mingi ilikufa mfano kilikuwa na ule wa ipp ukijulikana kama darhotwire, kulikuwa na mzibo.net.
Kitambo sana miaka ya 2004 huko
Hivi marafiki.com ndio darchat.com huo marafiki kiukweli niliutumia na ukanipa faida!.
Lakini hadi leo Marafiki ipo hewani bado.
Huo darhotwire ndio ulikuwa lazima utumie laini ya voda kuchat!?
Long time kweli!!..
 
Sisi wa miaka hiyo ndio tunajua darchat na darhotwire long time sana.. internet cafe ilikuwa saa moja buku..
 
Kipindi hicho kulikuwa na internet cafe flani magomeni mapipa kituoni ktk ghorofa la sea boys.
 
Darchat walikuwa wanatoa ofa ya vocha kwa wanachama wao waliokuwa wanawahi ku sign in asubuhi miaka hiyoo ya 2005- 2006.
 
Duh umenikumbusha mambo hayo enzi zileeee, nilikuwa naishi yombo vituka basi kuna jamaa alirudi toka US na komputer za kuokota akafungua internet cafee tukawa tunaenda kuzama kwa kulipia 500 kwa nusu saa, basi vile vi bling bling vya darhotwire, chat vinakumalizia muda kwa kushangaa, ukifungua email unasoma mpaka junk mail, hahaha, kweli mambo yamebadilika sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom