Ni nini kiliwashinda UKAWA kwenda mahakani?

SPACED

Senior Member
Jun 7, 2016
137
132
Nimefuatilia mwenendo wa kesi ya kupinga ushindi wa Kenyatta nikaona jinsi haki inavyojidhihirisha mahakamani.

Nimelinganisha utendaji wa mahakama za Kenya na za hapa kwetu nikaona hakuna utofauti wowote linapokuja suala la kutoa hukumu/haki.

Waliotangaza ushindi wa Kenyatta ni majaji sawa kabisa na waliotangaza ushindi wa Magufuli na Shein. Waliotengua ushindi wa Kenyatta ni majaji wenye profession sawa kabisa na waliotengua ushindi wa Maalimu Seif.

Tofauti ni kuwa Nasa wameonyesha uzalendo kwa kuziamini mahakama zao na UKAWA wakawaamini wazungu ambao bado wanaendelea na upelelezi.

Swali langu ni kwa nini UKAWA hawakwenda Mahakani ikiwa walikuwa na ushahidi sana na waliokuwa nao CCM Longido na CHADEMA kule Bunda?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katiba inasema rais akishatangazwa na NEC ndo stori imeisha hapo, ni katiba mbovu sana hii! Chadema wakianzisha mapambano kutaka ya rasimu ya warioba nitawaumga mkono na ndio silaha pekee ya wao kuitumia! Kupinga ufisadi walishaipoteza kwa kumkaribisha lowassa.
 
Katiba ya Tanzania inasemaje kuhusu uchaguzi na ya Kenya inasemaje ? ukimaliza kujiuliza hilo swali utapata jibu kwa nini hawakwenda mahakamani.
 
Usikurupuke kuandika bila kuelewa jambo unaloliandikia. Itawachukua watanzania miaka mingi sana kuelewa maana ya kuwa na katiba mpya
 
Wewe katiba ya nchi umeisoma au unapiga tu makelele huku kwenye mitandao? Bendera fuata upepo?

Matokeo ya Uraisi Tanzania hayaruhusiwi kuhojiwa mahakamani au mahali popote. Nenda ukasome katiba ndo uje huku.
 
Hivi walioitosà katiba ya warioba ni CHADEMA? Kwanini unaogopa kulaumu wahusika unaañza kusakama wengine? Ndo nyie watu wanabomolewa nyumba kinyume cha sheria badala ya kulaumu wahusika mnalaumu chadema eti wapo kimya! Acheni uoga watanzania
 
Wewe katiba ya nchi umeisoma au unapiga tu makelele huku kwenye mitandao? Bendera fuata upepo?

Matokeo ya Uraisi Tanzania hayaruhusiwi kuhojiwa mahakamani au mahali popote. Nenda ukasome katiba ndo uje huku.
 
akili yako na wewe,hujui kupinga matokeo ya urais mahakamani inaelezwa kwenye katiba ya kenya,katiba yetu imezuia haki hiyo!!!!jiongeze na wewe


Huyu mleta uzi ni mtu wa ajabu sana, yaani hata elimu ndogo tu ya masuala ya uchaguzi hana? Hafahamu kuwa matokeo ya uchaguzi wa Urais hapa TZ hayapingwi mahakamani?
 
Wewe spaced ni mmoja wa watu wapuyzi na inaonekana hata hujui katiba yetu inasema mara baada ya Rais kuapishwa.
Kwa kukusaidia tu unataliwa unune kwa miaka mitano ukisubiri uchaguzi mwingine .
Na hapo kwenye kununa ndio hutokea visa vya kutomtambua Rais ,Maandamano ya hapa na pale ,kumpinga kwa karibu kila jambo(bahati mbaya wakati mwingine hata mambo ya msingi)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kabla hujakurupuka saa nyingine muulize hata jirani huenda akakueleza kitu kabla hujaleta jambo hapa JF
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…