Ni Nini Hasa Mwanamke Anahitaji?

Ukweli ni kwamba complete satisfaction is impossible.
Bali kwa hofu ya kumkasirisha Mungu ndio inawezekana kuzuia tamaa zisizo za msingi kwa wanadamu

You have said all!!!
 
vyote ulivyotaja ni muhimu katika maisha na kupewa kila kitu haimanishi
kuridhika lazima uchunguze wapi kuna tatizo je ni tabia ya
huyo mke au hapati kile anachotaka kwa mumewe mpaka anaamua
kuhonga kupata kile anachotaka.
 
duh!! mambo yote hayo ni mwanamke tu!!

lbd na ww mkaka unamatatizo tena makubwa tu, haiwezekani eti umfanyie mtu yote hayo alafu bado atoke nje, lbd jogoo lako halipandi!!!

Refer item 6 of main post. Kama kuna kitu hakijawa covered uliza tutaleta majibu toka kwa wahusika.
 

Duh! naona lugha inakuwa ngumu kuelewa. Umeambiwa:

Mume anakuridhisha kwa mahitaji yako yote ya kimapenzi, kimwili, kihali na kimali lakini bado hutulii wewe na wanaume tu.

Ziada ni kuwa Bibie aliachiwa maamuzi yote makubwa katika nyumba na ya kimaendeleo lakini interest yake ni almost nil.
 
bado ana search apate yule anayemfaa....yawezekana ana list ndefu tu,akimpata yule amatakaye atatulia

Not necessarily; pengine hajui anachotaka.....pengine anapenda mahusiano na mwanaume zaidi ya mmoja!! wapo watu kama hao! (both sexes)
 
Tabia ya mtu ni kama rangi ya ngozi, hata uichubue itarudi asili yake. Pia, jasiri haachi asili. Nahisi huyo Mama ana matatizo makubwa sana ya akili. Sio kwamba haridhishwi na mume wake. Huenda ikawa katika maisha yake ya utotoni aliwahi kuambiwa kuwa figa moja haliinjiki sufuria, ila mafiga matatu ndo yanafaa kuinjika sufuria. Maombi yafanyike, hakuna kinachomshinda Mungu. Manake jamaa akifanya mzaha ataukwa ugonjwa wa zinaa, sasa cjui atamlaum nani na anavumila yote hazn. Wito, wanawake na wanaume wenye tabia chafu kama hizi badilikeni, hii ni sawa na kutapanya mali, hata Mungu mwenyewe hapendezwi na hii tabia.
 

Naona tutafika mpaka asubuhi kwaheri
 
tokea uchumba huyo jamaa anaonekana kumvuta demu kwa pesa na si upendo wa thati,huyo demu bado hataona mapenzi kwenye pesa coz hayapo hapo,bali ni upedo wa kweli...............makosa yapo tokea pre-marriage period,it wasnt love bt cashhhhh:smash:
 
Mi naona Hulka na tabia ya mtu tu.
Kama mtu unafanyiwa kila kitu, na mume wako, kinachokupeleka nje sio, shida wala tamaa ya pesa.
Ni mwili wako tu, na tamaa za mwili wako uko hivyo.

Kwa mtoto wa kike, ni mbaya sana kufumaniwa na mume wako zaidi ya mara mbili halafu unaomba msamaha,
unasamehewa unarudia tena na tena.
Hata kama huridhiki namna gani, kwa mwanamke kutoka nje tena waziwazi namna hiyo ni mbaya, mi naona utakuwa humpendi huyo mume,
labda unaishi naye kwa tamaa ya vitu vyake tu.

Kwanza Biblia inasema Mwanamke ni mlinzi wa Mume wake, yeye ndo anatakiwa akae amuombee Mume wake asivutwe na makahaba,
kwa sababu wanaume wao huvutwa kwa kuona. Yeye ndo anatakiwa atengeneze mazingira ya kumsaidia mume wake, asishawishike na vibinti huko barabarani. Halafu tena mwanamke wewe ndo unakuwa wa kwanza kufanya huo uasi. Binafsi naona haipendezi kabisa.

Sina maana kwamba wanaume wafanye hivo hapana, lakini mwanamke amepewa nafasi ya pekee ktk kumtunza na kumlinda mume wake.
Kama humpendi ndo utamfanyia hayo mambo ya ajabu hivyo. Wanawake wamepewa Roho ya kuvumilia na kusamehe uovu wa waume zao kuliko hata wanaume. Sasa iweje mwanaume ndiyo awe na roho ya kuvumilia na kusamahe kwa kiasi kikubwa kuliko mwanamke?

Haijalishi huridhiki namna gani, njia ya kutatua tatizo lako sio kuruka ruka na huku unataka ubaki kwa mume wako.
Kama unaona hakuridhishi mwambie, halafu uamue kumuachia baba wa watu uhuru ili ukatafute hicho unachokitaka,
kwa uhuru zaidi.
 
Naona tutafika mpaka asubuhi kwaheri

Unaweza ukawa ni Mwanaharakati wa haki za wanawake which is good. Kuna wengi pia tunajali haki za wanawake.

Looking into things from the information provided and provide feedback is a mature way.

In cases where u may think information is not enough for you to provide the feedback, u can always ask and get required answers.

However, making arguments for sake of arguments without any basis of facts advanced, does not necessarly entitle your comments to be a depandable opinions to be appreciated.
 
tokea uchumba huyo jamaa anaonekana kumvuta demu kwa pesa na si upendo wa thati,huyo demu bado hataona mapenzi kwenye pesa coz hayapo hapo,bali ni upedo wa kweli...............makosa yapo tokea pre-marriage period,it wasnt love bt cashhhhh:smash:


Inaweza ikiwa kweli, we will get answers.

Lakini bado kuna maswali kama kwa hao wanaume wengine alio nao kwa mpigo ndiyo suluhisho la anachokikosa?
 


hapo kwenye red hapo:dance:
 
Jinsia zote mbili zina matatizo na matamanio yasiyo na mipaka. Hakuna kinachomridhisha mwanadamu na akaganda nacho mwanzo wa uhai wake hata mwisho. Binadamu ni mtu wa adventures bila kujali ubaya na uzuri wake. Ila kwa kuwa tuna akili na dhamira, mambo mengine tunayaonea haya, na wakati mwingine tunayafanya kwa uficho ili walimwengu wasitubaini.

Sijui kama kuna mtu ambaye yuko kwenye mapenzi kapata chaguo lake kwa asilimia mia kama alivyotaka iwe. Hakuna. Hapo ndio mwanzo wa matatizo. Kupewa mahitaji yote ya kibinadamu sio tiketi ya kumpenda mtu. Mwanamke anahitaji ulinzi. Sio ulinzi kama wa Ultimate security. Ulinzi wa kihisia, kimali, kimwili, n.k. Ulinzi wa kiroho atatoa Mungu. Mwanaume mmoja kutimiza yote hayo ni ngumu sana. Wapo ambao watakosa baadhi ya mambo fulani na watatulia kwa kuwa hawana jinsi. Wapo wanaotaka kila kitu na ndio maana unashangaa mwanamke anachapwa nje ya mahusiano.

La msingi ni ni kukubali kuwa si kila kitu unaweza kupata. Pia si kila kitu mwenza wako anaweza kukupatia. Gharama ya kupata hicho ulichokosa yaweza kuwa kubwa kuliko gharama ya kutokuwa nacho. Ni hayo tu
 

Umenikumbusha kisa kimoja: Jamaa alimfumania mkewe live kitandani. Akaamua kumuua mkewe. Alipoulizwa kwa nini alifanya hivyo badala ya kumuua mbaya wake alijibu " Niliogopa kuendelea kuua wanaume kila baada ya siku chache!!". Baadhi ya wanawake hata wasuguliwe kisawasawa bila mapumziko watatoka nje. Kwao mumewe na wanaume wengine wa nje hawana tofauti na katika harakati zao hizo wanaweza kupambana na wanaume ambao hawana uwezo wa kusex kama walionao waume zao. Lakini hata wanawake watakuambia nao wanaume wako hivyo na zaidi.
 
Watu hawafanani..hivyo wanawake hawafanani!Ndo maana kuna ambao bila pesa hawezi kua na wewe ila sura..umbo na tabia hajali n.k.Situation ulizotaja hapo juu zinaweza kua ideal kwa baadhi ya wanawake ila sio wote!Ukirejea kwenye hizo story inawezekana kabisa aina ya mwanamke unayemwongelea hawezi kuappreciate anayofanyiwa bali anatumia huo kama udhaifu wa mumewe hivyo anautumia kikamilifu..au labda ana tabia tu ya kurandaranda..au labda hajaridhika!Kama kuna muhusika kweli ni vizuri akaulizwa yey
 
hapo lazima kuna something wrong bwana sio bure!!!
 
mahusiano yanajumuisha mambo mengi,huwezi kutazama upande mmoja na kuutolea majibu.kinachoniridhisha mie kwenye mapenzi sio lazima kiwe kinafanana cha mwingine.

lakini kutokana na maelezo yako kama ni kweli huyu dada anafanyiwa yote hayo na bado anatoka nje ya ndoa yake atakuwa na matatizo ambayo sijui kama ataweza kutulia kwenye relationship yoyote ile,

tunapokuwa kwenye mahusiano hatutegemei kukutana na malaika,au kuchukua mapungufu yetu na kuyaweka kichwani pa wengine ili tukamilike ndio maana kuna neno uvumilivu la sivo utakuwa na mahusiano mapya kila siku.

nachoona huyu dada anatafuta mkamilifu ambaye hayupo na wala hatakaa atokee,anaendelea kujiongezea list ya watu wataompa stress zaidi za maisha .

nina maswali kwa dada ,kama alitoka mara moja hakuna jambo alilojifunza kwa kufanya ivo na je alipoanzisha uhusiano mwingine hakujiuliza maswali, lilimtoa kwa mumewe na kwenda kwa huyu mwanaume wa nje na bado wameachana na sasa ana mwingine.

kwangu huyu dada namuona kama !!!!..........nilikuwa niseme vibaya lakini ndo ukweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…