Watu8
Platinum Member
- Feb 19, 2010
- 77,343
- 111,606
Habari wana MMU,
Waungwana husema ya kwamba, "Hasira hasara", na wengine pia wakatabanaisha ya kwamba, "Hasira za Mkizi,furaha kwa mvuvi". Binafsi kama ilivyo kwa wanadamu wengine nina kiboksi cha hasira ambacho kwa mtu atayenichokonoa si haba akakutana na dhahma itayomfanya ajiulize, ni kipi haswa kilichompata kanga hadi akawa na vidoti doti na wala si kuku....
Sasa basi hebu kwa uchache, tujadili ni nini chanzo cha hasira na pengine kwa wale wanaokasirika kwa wepesi tusaidiane namna ya kukwepa hali hiyo....
Nawakilisha....