Ni ngumu kuamini kama kaka yangu amefariki dunia

Shamkware

JF-Expert Member
Nov 25, 2013
1,740
2,244
Tuliongea mara ya mwisho Jumatatu mchana baada ya kusikia ile habari ya wagonjwa Mbeya, kaka akawa ananiambia mdogo wangu nasikia hali sio nzuri jikingeni jamani nyie mnaoishi kwenye mikusanyiko mikubwa.

Nilimwambia kaka sio huku tu popote ulipo chukua tahadhari tu wewe, kama wewe maana hujui siku wala saa akaniambia sisi huku mkoani watu wala hawajali kabisa tunaendelea na shughuli zetu 😓

Usiku wa kuamkia Alhamisi majira ya saa 9 usiku alianza kupata maumivu ya kifua na kubanwa anakosa hewa, akaamua kutoka na kukaa nje ili apate hewa vizuri, ilipofika saa kumi akawa anashindwa kabisa kupumua vizuri.

Mkewe alimpigia simu dereva wake awahi ili wampeleke hospital. Alipelekwa hospital fulani ya wilaya majira ya saa 11 alfajiri. Ilipofika majira ya saa 2 asubuhi alinipigia simu kunipa taarifa, akaniambia mdogo wangu nabanwa na kifua sana, nakosa hewa na kukosa nguvu halafu nahisi kama nina kitu kizito kifuani ila naendelea poa mdogo wangu, usijali leo naweza rudi home.

Cha kwanza nilimuuliza, umepimwa covid? Akanambia hakuna kipimo hapa ila nimepimwa tu malaria mpaka xray ya kifua sina tatizo wala. Nikwambia hama hiyo hospital uende private inayoweza shughulikia covid-19. Akasema kesho nitaomba rufaa nije Muhimbili tu, nikasema sawa.

Kabla hata kesho haijafika, usiku alibanwa mno mpaka wakamuwekea mashine ya kupumulia bado haikusidia, asubuhi ya Ijumaa majira ya saa 1:12 asubuhi akafariki dunia kaka yangu. (Ameumwa siku mbili tu) Inaniuma sana. Tumezika jana na naomba tu Mungu maana msiba haukuwa na tahadhari wala kujikinga kwa aina yoyote, nawaza sipati picha, Mungu atusaidie tu.

Please guys be carefully hii kitu itacost maisha ya watu wengi bila hatua kuchukuliwa ikiwemo kuhimiza watu kujikinga.
 
Watalii wazidi kuja Tanzania, hii ni fursa adimu nchi kupata watalii wengi kwasababu nchi nyingine zimepiga marufuku watalii na huku mtalii akija anapimwa tu joto kichwani, hakuna ule usumbufu wa mtalii kuwekwa quarantine kujitenga siku 14.

Sisi tunapenda wetalii hata kama wao wametufungia kwenda kwao sisi tunawakaribisha ili watuchangie pato la Taifa.

Tanzania hakuna corona labda nimonia tu.
 
Mimi nikisimulia mkasa wa kuondokewa na kaka angu humu kwa changamoto ya kupumua watu watanijua, na msg zake za mwisho WhatsApp ninazo, Nazisoma kila muda, R.I.P Brother Padre.
Pole pia mkuu
 
Mimi nikisimulia mkasa wa kuondokewa na kaka angu humu kwa changamoto ya kupumua watu watanijua, na msg zake za mwisho WhatsApp ninazo, Nazisoma kila muda, R.I.P Brother Padre.
Ni padri nani na wa wapi?
 
Back
Top Bottom