Kichankuli
JF-Expert Member
- Dec 18, 2008
- 887
- 191
Ukiacha undugu wa damu, sheria pia inakataza kuolewa na mume wa mama au kuoa mke wa baba!
Ndugu kuoana ni mbaya lakini vipi kwa wale wasiojuana kama ni ndugu?
Kuna dada kaoana n akaka yake waliyeshangia baba bila kujuana maana mama zao walipata mimba halafu wakaolewa na watu wengine na mimba hizo zikawa za wababa waliowaoa yani waliwabambika watu wengine, walivyokuwa wakubwa, hao watoto wamepisha na miaka saba yaani mvulana kamzidi msichan miaka saba sasa walivyooana, mama zao kila mmoja kwa wakati wake akaamua kumwambia mwanae ukweli kwamba huyu siyo baba yako kila mmoja bila kujuana akamweleza mwanae ukweli na akampa maelekezo mahali baba yake alipo na jina, wakafunga safari mpaka hicho kijiji wakaenda kwanza kumtafuta baba wa msichana kufika yule msichana alishtuka yani huyo baba na mume wake wamefanana utafikiri mapacha mume wake ana kovu usoni na huyo baba analo, bai wakakribishwa yule dada akajieleza akamtambulisha mume wake sasa yule mwanaume akashangaa majina ya baba zao yanafanana si ikabidi na yeye ajieleze baba yao akawaomba msamaha akasema endeleeni tu maana mmeishafunga ndo na mlikuwa hamjuani sisi ndo wenye makosa.
sasa hapo kuna makosa kweli? na wale wamama walivyojua wakawaambia watoto wanyamaze maana wakisema ndoa zao zitavunjika kwa hiyo wanaendelea.
Tunavyoamini dini zote ni kwamba Mungu alimuumba Adamu halafu akampa usingizi mzito na baadaye kumfanya Mwanamke (Eva/Hawa) kutoka kwenye ubavu wa Adamu. Kwa maaana hiyo walikuwa wawili tu, lakini kwa sasa katika ulimwengu huu tuko mamilioni ya mwanaadam. Je huo uharamu haukuwakumba kizazi cha awali cha Adam na Eva/Hawa?
Zimeharamishwa katika Kitabu cha Mambo ya Walawi 18:22 inayosema:Na hizi ndoa za watu wa jinsia moja zimeharamishwa wapi? Maana ni kama kaugonjwa sasa hivi humu mitaani tunamoishi. Naombeni verses tafadhali.