Ni ndugu au rafiki?

M-bongotz

JF-Expert Member
Jan 7, 2010
1,734
405
Waungwana hebu nisaidieni kwenye hili suala ambalo nimekuwa nikilifikiria kwa muda mrefu bila jibu sahihi.,ni hivi eti mke wako ni ndugu yako au ni rafiki yako?
 
Hii tushawahi jadili.... ngoja nikupastie.... comment yangu alafu fuatilia Link hapo juu...

Mume/Mke ni ndugu sababu undugu si wa damu tu...
ndugu ni mtu ambae mnajaliana, pendana, saidiana, wasiliana,
na muhimu zaidi ni kua uko kwa ajili yako no matter what!

Mume/Mke ni rafiki sababu rafiki aweza kua ni ndugu au mtu baki...
Rafiki ni mtu ambae anakuelewa kwa upana jinsi ulivyo, wapi akuguse
kukuumiza, wapi aguse kukufurahisha, kitu gani unapenda/chukia,
jinsi gani aku handle ili msikwazane, ni mtu uta confide siri zako bila
kuogopa atatangaza, ni mtu ambae pamoja ya kwamba mnaweza mkawa
siio blood relatives but ni mtu wa muhimu mno katika maisha yako ya kila siku...

Huo undugu na urafiki kati yenu ndo hufanya muwe best couple au vice versa
tokana na jinsi mnavyo handle undugu au urafiki wenu....
 
Mke wako siyo ndugu yako kwa sababu ndugu huwezi kufanya naye mapenzi! Mke wako ni rafiki yako.
 
Ndugu ni yule uliyezaliwa nae tumbo moja! Watu wengi wamekuwa wakiwaita marafiki ndugu ili tu kuonesha uzito wa urafiki wao. Rafiki ni rafiki na ndugu ni ndugu na mkeo si ndugu yako
 
Huyo mkeo ni rafiki tu.. kwani wakati wa safari ya mahusiano ulipoanza ulikuwa unataka awe rafikiyo au nduguyo.
pili, undugu hauombwi lakini wakati unaingia katika uhusiano naye ulikuwa unaomba akukubali muwe pamoja, umeenda kuonga kwao mahari na baada ya kukubaliwa mkasheherekea kwamba amekukubali (harusi) na ndoa yenu sio sehemu ya kuhalalisha undugu bali urafiki.
 
Hebu tutafakari/tujadili mke au mume wako ni nani hasa na ana nafasi gani ktk maisha. Ukisema ndugu hapana maana hakuna ndugu anayepewa talaka, ukisema rafiki sijui?
 
Back
Top Bottom