Ni nani yuko nyuma ya BBC Swahili?

Ni nani yuko nyuma ya BBC Swahili?

Yatosha tu kusema kaandika mwalimu mkuda. Reasoning capacity sifuri. Anakiri mabaya yapo. Hataki yasemwe na BBC bali yasemwe mazuri tu. TBC inaimba usiku na mchana mazuri na sifa kedekede hata za kubumba, hilo halioni! Njia rahisi na ya uhakika kama hutaki mabaya yako yasemwe ni kutoyafanya. Hakuna atakayesema kisichokuwepo. Utakuwa uongo. Mwalimu wa sampuli hii ni wa kukimbiwa kama corona. Anafundisha ujinga!
Naunga mkono hoja yako kwa 100% kama hawataki BBC iwaulike waache kuwatendea uonevu uovu wapinzani.
 
Natamani hii channel ingefungiwa airtime Tanzania. Huyo Kikeke atafute uraia huko kwa wakoloni

Nyie mnataka muishi dunia gani iliyo na uelekeo mmoja tu??

Hiyo dunia ya namna hiyo mnayotaka kuishi ndani yake haipo dude....!

Na kulazimisha kitu kisichokuwepo, kiwepo ni kujiumiza na kujitafutia matatizo ya bure bila sababu......

Tunaishi katika dunia kinzani. Na ukinzani huu ndiyo unaoleta UZURI na MAANA ya maisha...

Tunaishi dunia ya leo UNACHEKA, Kesho UNALIA....

Tunaishi dunia ya leo mwingine UNAPATA, kesho UNAKOSA...

Tunaishi dunia ya leo UMETIWA MOYO, kesho UMEVUNJWA moyo...

Tunaishi katika dunia ya leo UNAPONGEZWA, kesho UNAKOSOLEWA...

Hamuwezi kupingana na LAW OF THE NATURE... Haya ndiyo maisha ya binadamu....

Yesu Kristo mwana wa Mungu katika umbo na sura na mwili wa kibindamu alikabiliana na hali na aina hii ya maisha....

Hakulalamika. Hakupingana na mazingira yake. Hakubadilisha mazingira ya uonevu na ya kukatisha tamaa yaliyokuwa yanamzunguka...

Alishinda na zaidi ya kushinda ktk mazingira hayo hayo...

Nyie mna nini? Mnataka kutengeneza dunia yenu yenye uelekeo mmoja tu? Mtaweza na CCM na Magufuli wenu?

Kaeni tayari na mjiandae NATURE kuwabadilisha iwapo mnashindwa kubadilika kulingana na ASILI....
 
Watetezi wa CCM mitandaoni acheni kuwalaumu BBC chombo huru cha habari kipenda haki usawa na Amani, tumeini fursa hii kuwashauri CCM waache siasa za maji taka, waache uonevu kwa wapinzani wajikite kwenye maendeleo tu wataona BBC itawasifia zaidi, wasifanye mabaya wakataka BBC iyalee kama TBCCCM inavyowafanyia wananchi.
 
The fear of unknown inakusumbua....

Yaani yeyote anapotoa maoni kinzani na serikali anakuwa anatumiwa? Kuna kuwa na "mtu fulani nyuma yake?"

Yaani unataka kila mtu, kila chombo cha habari kiimbe propaganda zenu na za Magufuli?

Wengine wana akili na siyo "ndege kasuku" anayeiga kila sauti na kupokea tu bila kujiuliza maswali kwa kila kisemwacho na watawala waovu....

Ukisema upendalo watu wasikie, ni lazima waende kuchunguza na upande wa pili kuna nini. Hicho ndicho msichotaka kukisikia. Lakini mpende msipende, lazima msikie tu....

Kwanini mnaogopa na kuanza kukimbia mpaka vivuli vyenu nyie????
Wana CCM wamekuwa watumwa wa zidumu fikra za mwenyekiti wa CCM na fikra za Naibu Rais Bashite, hawataki kukosolewa wanajiona ni malaika hawana Dhambi, wametafuna trilion 1.5 wakamtoa CAG kafara nayo hawataki BBC waseme? zipo wapi bilion 12 za Ndungai? Napo BBC wakae kimya? Ujenzi wa chato Airport kienyeji pasipo idhini ya bunge hawataki BBC ihoji?
 
Bado trillion zaidi ya 4 zile za Kangi na mkuu wa zimamoto (Ambaye ameteuliwa majuzi tu kua mkuu wa mkoa wa kigoma)..
Wizi kibao ila hawaongelea hayo..

Wanatamani kila chombo cha habari kowe kama TBcmm na hao wakina ayoccm
 
USHAURI WANGU
Endeleeni kuripoti habari zenye kujenga na kuelimisha. Acheni taarifa zenye mashambulio binafsi kwa mtu. Hii kamwe haitawajenga, kumbuka BBC ni taasisi, hii chuki itaota mpaka ndani ya taasisi.

Mzalendo
Mwl James Katunga
Inatosha tu kusema huna uzalendo wowote.

Kujivisha uzalendo, sio kuwa mzalendo.
Bandiko lako refu nimesoma mistari miwili ya mwanzo likanichosha.

Zidi kuomba sana kama upuuzi huu uliobandika hapa utakuwezesha kupata uteuzi, na watu kama wewe mnapopata uteuzi ndipo taifa linapozidi kudidimia.

Bure Kabisa. Hopeless.
 
Inatosha tu kusema huna uzalendo wowote.

Kujivisha uzalendo, sio kuwa mzalendo.
Bandiko lako refu nimesoma mistari miwili ya mwanzo likanichosha.
Neno uzalendo huko CCM ya sasa linatumika vibaya, kwa CCM ya sasa uzalendo ni kuwabambikia kesi kuwaonea upinzani kuwafanyia kila lililo la uonevu mkubwa.
 
Bado trillion zaidi ya 4 zile za Kangi na mkuu wa zimamoto (Ambaye ameteuliwa majuzi tu kua mkuu wa mkoa wa kigoma)..
Wizi kibao ila hawaongelea hayo..

Wanatamani kila chombo cha habari kowe kama TBcmm na hao wakina ayoccm
Kigoma CCM wamelipwa pesa kwa ajili ya kujenga bwawa la umeme mtu malagalasi lakini wameipiga hiyo pesa wakasingizia imekwenda kujenga bwawa jipya mbugani rufiji
 
Hii ni baadhi tu ya watu waliojawa na wivu ndani yao na wasiopenda kuona wengine wakionekana kuwa juu zaidi

Hiyo kufuta ule uelimishaji kuhusu 5G alioelezea mchungaji gwajima ni dhahiri kwamba wapo watu ambao wako nyuma ya pazia wanajaribu kujificha nyuma ya BBC ili wasifahamike maana wanajua kile wanachokifuta ni cha kweli
Hivo hawataki isambae kote kwa sababu ya huo wivu uliowajaa
Gwajima anaelimu gani ya kujua madhara ya G5 kama sio ukichaa unaowasumbua nyinyi watu.

Mnataka taifa zima tuwe wajinga kama nyinyi, hii haitawezekana, tutapambana na hamuwezi kushinda vita hii.

Mnaishi enzi hii ya uwazi lakini mnataka watu wawe wajinga kama nyinyi, yaani hata hamuoni aibu kabisa kuzungumzia mambo ya kipuuzi kama haya, tena kwenye mtandao mashuhuri kama huu wa JF?

Hivi hamna akili ya kujua kwamba dunia ya leo huwezi kufungia watu ndani ya nchi yako wasijue chochote kinachoendelea duniani?

Haya ngoja niwape ushauri, nendeni mkajifunze Korea Kaskazini, ndiyo nchi pekee sasa ambako watu wake wanategemea kusikia habari zinazosambazwa na serikali yao. Hapa mtashindwa.
 
kudamademede,

Wewe ni mwalimu wa chekechea na mzalendo wa Tanzania unataka kila chomho cha habari dunia nzimà kiunge mkono juhudi ili upate uteuzi. Vyombo vyetu vya habari vimefungwa mdomo wewe akili zako za kijinga zinakutuma ushauri Serikali ivifunge mdomo pia vyombo vya dunia visivyounga mkono juhudi kwa kuwa vinatumia Kiswahili lughà yako ya Taifa. Kiswahili ni lughà tu kama lughà nyingine na yeyote anayeijua anaruhusiwa kuitumia hata akitaka kutukana lakini anayetukanwa aende Mahakamàni nao huko wapate kazi. Kuna Msemaji rasmi wa Serikali wewe na ujuha wako unatoka wapi kushauri chombo cha Habari Cha Serikali ya nchi nyingine kifungwe mdomo kama vya kwenu?
 
BBC nilishawashtukia kitambo tu. Wamekaa kwa mlengo wa magharibi. Wanatuteka kisaikolojia kwa kujiita BBC Swahili...lakini ni wakoloni mambo leo wale. Know you know
 
NANI YUKO NYUMA YA BBC SWAHILI?

Kama tunavyofahamu wote kuwa BBC Swahili ni chombo cha habari kinachoripoti habari za ulimwengu wa njia ya Kiswahili ambayo ni lugha ya Taifa letu Tanzania.

Kwa muda mrefu sasa chombo hiki kimekuwa kikiripoti taarifa zinazotokea ndani ya nchi kwa njia inayoleta ukakasi kwa watanzania hasa wazalendo wa nchi yetu pendwa Tanzania.

Dunia nzima ilikumbwa na janga la homa ya mapafu COVID-19 ambayo imekuwa gumzo duniani kote ikipelekea maisha ya watu kubadilika na tabia mpya kuzaliwa.

Katika kupambana na janga hili lililotishia sana maisha ya watu, Wizara ya Afya iliyochukua tahadhari zote kama zilivyoelekezwa na wataalamu mbalimbali wa afya ndani na nje ya nchi. Jitihada hizi kwa mara nyingi zilibezwa na kuhujumiwa kupitia chombo cha habari cha BBC Swahili kwa kuripoti habari zenye kutia hofu watanzania na kukosoa utendaji kazi wa wizara ya afya hapa nchini.

HII INAPELEKEA KUHOJI NI NANI YUKO NYUMA YA BBC SWAHILI
Ni kweli kwamba hamna anayewapangia BBC Swahili waripoti nini, lakini pia wajue tuna ruhusa ya kuhoji wanachoripoti hasa kama kina maslahi na nchi yetu.

Kuna mambo mengi yaliyofanywa na Rais wa Tanzania mheshimiwa John Magufuli kwa kipindi cha miaka mitano ya muhula wake wa kwa za wa urais; chombo hiki kimekinga mgongo kutoongelea mambo haya kabisa huku kikiwa mstari wa mbele kuwapa nafasi wale wanaoonesha nia ya kuikosoa na kupinga serikali ya Tanzania pamoja na utawala wa rais Magufuli.

Wakati huu ambao vuguvugu la uchaguzi linaendelea kupanda na kila kona gumzo kuu ikiwa ni uchaguzi mkuu wa Oktoba 2020, yameonekana matukio mengine ambayo sio ya kufumbia macho hasa kutokana na sintofahamu kwamba chombo cha habari cha BBC Swahili kinafanya vitu hivi kwa ajili ya kumnufaisha nani hasa.

Katika kipindi ambacho Tanzania imekuwa kwenye mapambano na janga la COVID-19, muhubiri mmoja hala nchini mwenye maelfu ya wafuasi ambaye ni mwanzilishi na msimamizi wa makanisa ya Ufufuo na Uzima duniani kote, Askofu Josephat Gwajima alikuwa mstari wa mbele akitoa elimu kwenye jamii kupitia vipindi vya ibada kanisani kwake.

Siku ya Jumapili tarehe 05.07.2020 BBC Swahili kupitia ukurasa wao wa Twitter walichapisha habari inayolenga kukanusha kile Askofu Gwajima alichosema kuhusu hatari ya mionzi ya 5G na jinsi unavyoathiri afya ya seli katika mwili wa binadamu.

Leo tena tarehe 10.07.2020 BBC Swahili imechapisha taarifa ya kuondolewa kwa ujumbe unaofanana na huo kwenye ukurasa wa Instagram wa Askofu Gwajima. Hii bila shaka ni kuijulisha dunia mafanikio ya jitihada zake za kutaka kile alichokiongea Askofu Gwajima kisisikike kwa watu duniani kote.

Ikumbukwe kuwa Askofu Gwajima ni mtia nia wa kiti cha Ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi CCM katika jimbo la Kawe- Dar es Salaam. Hii imezua sintofahamu kwa maelfu ya watu nje na ndani ya nchi wanaompenda na kumfuatilia Askofu Gwajima huku wakiamini ni mtu ambaye amejitoa sana katika kipindi kigumu cha janga la Corona hasa ukizingatia hofu iliyokuwa imetanda.

HII IMEPELEKEA KUHOJI TENA; NANI ALIYE NYUMA YA BBC SWAHILI?
Je, kuna mtu ndani ya Tanzania ambaye anawaza kufanya hivyo kutomchafua Askofu Gwajima na kuondoa imani kubwa iliyo kwa wananchi juu yake?

Je, BBC mliwezaje kufahamu kuwa ujumbe umefutwa kwenye ukurasa wa Instagram? Hii inaleta maana kwamba jitihada zote za kuondoa ujumbe huo zimefanywa nanyi. Nani hasa anawatuma au anawaomba kufanya hivyo.

Je, vyama vya upinzani ndio vinafanya jambo hili? Kwanini BBC Swahili mtumike kisiasa katika jambo hili?

Je, hamuoni wafuasi wenu wanafatilia taarifa kwenye kurasa zenu watapunguza mapenzi nanyi hasa ukizingatia kuwa wapo watu wengi ambao wasingependa kabisa Askofu Gwajima aonewe?

Je, hamuoni kuwa mnachofanya ni shambulio binafsi ambapo chombo cha kimataifa kama BBC Swahili kufanya hivyo ni kushusha hadhi yenu na kutia doa ubora wa taaifa zenu?

Ikumbukwe watu wenye uhusiano wa moja kwa moja na BBC Swahili wanajulikana na tungependa serikali iwachunguze na kuangalia mahusiano yake na jambo hili. Hatutakubali hujuma za aina yeyote kwenye nchi yetu.

Kuona mabaya tu ya nchi na ukatafumbia macho mazuri ya yanayofanyika kila siku ni ujumbe wa aina yake kuonesha uadui wa kimaslahi au kutumiwa na mtu au kundi lenye chuki binafsi.

USHAURI WANGU
Endeleeni kuripoti habari zenye kujenga na kuelimisha. Acheni taarifa zenye mashambulio binafsi kwa mtu. Hii kamwe haitawajenga, kumbuka BBC ni taasisi, hii chuki itaota mpaka ndani ya taasisi.

Mzalendo
Mwl James Katunga
Kama kweli wewe ni Mwalimu uliyesomea UALIMU basi ni shida inabidi uache ukafanye biashara/kazi nyingine maana utawapotosha watoto wetu huku shuleni.

Hivi wewe na UBOYA wako unaamini kabisa 5G inasababisha Covid-19? Hivi unaweza kutupa mchanganuo wa jinsi hao corona virus wanavyosafiri kwa kutumia hiyo technology ya 5G , Huyo Mlaza watu kifo cha Mende Amfifiro ni Mpiga Deal na hana chochote anachokijua kuhusu corona virus au covid19 zaidi ya KUPAYUKA tu na kuwaadaa MISUKULE yake imuamini na kuendelea kumpa sadaka.

Nashangaa mwalimu kama wewe kuamini UPUUZI wa "MKONO WA BAUNSA" na Unafeel the passion zaidi ya telemundo mapanchi mengi hata touch akizima mdundo bye bye!!
 
Back
Top Bottom