Ni nani mlinzi wa rasilimali za Nchi?

ANAUPIGA MWINGI

JF-Expert Member
Apr 14, 2022
389
753
Ni nani ni Mlinzi wa Rasolilimali za Taifa kwa sasa?

Ni Bunge? Hapana hawa walishakuwa sehemu ya Serikali na kazi yao ni kusifia na pia wengi wao wameingia madarakani kwa wizi wa kura, hawa hawawezi kamwwe kuwa walinzi wa Rasilimali, hawa sio wa kuwategemea kabisa, ni sawa na kuavhia Fisi Bucha.

Ni Mkuu wa Nchi? Angeweza kuwa lakini kwa aina ya wakuu wa nchi kama huyu Chifu kwa kweli tusitarajie, huyu hawezi kuwa mlinzi wa Rasilimali, na haeleki kuwa mlinzi kabisa.

Hayuko Serious na inaelekea yuko upande wa wanao fisisi nchi hasa walio wahi kufisidi nchi kipindi fulani.

Ni Jeshi? Hawa hapama kabisa, Jeshi la sasa liko very corrupt, hawa pamoja na kupiga kwata lakini wako corrupr some how, kina upigaji sana hata huko kwao na hawawezi kupata nguvu za kuwa walinzi.

Ni Raia wenyewe? Tungeweza kuwa yes lakini Raia wengi wako tunaabudu na kusifia na kuabudu watawala mafisadi, na wanao salia hawako Serious, raia wanachukulia poa Ufisadi, lakini hawajui impact yake hasa kwa watoto wao. Nigeria leo raia wao wana safa ni kutokana na ufisadi ulipigwa na watawala hasa enzi za wakina Sani Abacha.Impact yake ndo inafanya kazi leo hii, nchi ina kiwango kikubwa sana cha ukosefu wa kazi.

Raia wa Tanzania tunachekelea sana lakini Madhara ya Upigaji ni huko Mbele ya Safari, Fikiria Trilion 5.8 zinapigwa, Hizi pesa zingeweza sana kutatua shida ya ajira kwa graduate.

Sasa ni nani mlinzi?
Kwa kifuoi sioni mlinzi, hii ni shamba ya Bibi,
 
Shamba la bibi hili
Wasomali wanavuna, waarabu wanavuna

Watanganyika tumewekwa kati
 
Back
Top Bottom