Ni nani anyeithibiti matumizi ya $ Tanzania kati ya BOT na Sheria?

Danniair

JF-Expert Member
Feb 18, 2011
360
66
Ndugu zangu nimeshindwa kukiweka kichwa cha habari sawa, lakini naomba kujua ni nani anayetakiwa kuthibiti matumizi ya $ nchini Tanzania? Zamani ilikuwa pesa hizo huzigusi ila kwa kibali maalumu. Leo imefikia hata bidhaa za kuuziana sisi kwa sisi (mihogo kwa mchicha) tunatumia kigezo (Price index) ya US Dollari. Unaambiwa mchicha fungu ni $2 kazi kwako kuzibadili ktk fedha ya Tz. Je, ni nani anayetakiwa kusimamia sheria ya BOT kuhusu fedha /malipo halali ya shilingi? Je, shillingi si mojawapo ya alama za mtanzania kama ilivyo bendera na wimbo wa Taifa? Kwa nini hakuna usimamizi mzuri wa pesa yetu kama ilivyo ktk nchi zingine. Nasikia India huruusiwi kununua kitu chochote kwa hii dollari inakuaje hapa kwetu wao wanaruhusiwa kufungua maduka na kutuuzia computa kwa kigezo cha dollari? La ajabu hata TRA wanadai 'wauza nyanya wa kariakoo' pia wanunue mashine za mhesabu za VAT kwa US $. Ebu kama tunaipenda nchi yetu basi na tupate maoni ya wataalamu wa sheria ili wahusika wachukiliwe hatua. Tusipofanya sisi hakuna atakayetoka nje ya chini na kutufanyia. Asanteni.
 
Back
Top Bottom