Ni nani anayemdanganya Edward Lowassa?

Ni nani anayemdanganya Edward Lowassa?

Lowasa pesa zake ndo zinamdanganya mengine yoote ni hadithi kama angekua hana pesa hakuna ambae anagehangaika nae!!
Lowassa ana uwezo mkubwa kifikra wa namna ya kuwa fisadi papa lakini hana uwezo kifikra wa namna ya kuwa Rais wa Tanzania.

Kazi iliyobaki kwa sasa ni kulea wajukuu na kuchunga ng'ombe.

Siasa awaachie wapiga dili kama kina Mbowe ambao ni political hustler!
 
Dunia inatambua Lowassa ana utajiri wa kifikra kuhusu njia ya kuwa fisadi nchini Tanzania. Kinachoendelea kwa sasa kinadhihirisha Lowassa anahitaji huruma za kisiasa kutokana na mwenendo wake kisiasa. Anahitaji sana ushauri usio wa kinafiki kuhusu hatima yake kisiasa nchini.

Nilivyomsikia kwa mara ya kwanza akitoa madai kuwa ukimya wake baada ya Uchaguzi Mkuu umesababisha kuwepo amani nchini, nilidhani kinachomsumbua ni mihemko ya kisiasa.

Nilipomsikia pia kwa mara ya pili akitamka maneno hayo Mkoani Arusha wakati akishiriki katika kampeni za Uchaguzi wa Jimbo la Arusha ambao uliahirishwa katika siku ya Uchaguzi Mkuu baada ya kifo cha mgombea wa ACT-wazalendo Estomih Mallah sikushangaa sana.

Kilichonishangaza zaidi ni pale nilipomuona tena kwa mara ya tatu ndani ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri, Usharika wa Monduli akisema kunyamaza kwake baada ya wananchi kupiga kura kwenye Uchaguzi Mkuu 2015 kumewafanya wananchi wasiuane. Eti anadai wananchi walikuwa wanasubiri neno lake ili waingie barabarani na kuanza kuuana.

Lowassa anataka kutuambia watanzania wengi ni kama nyumbu kwamba kila atakalolisema watalifuata au kulitenda. Anataka kutuambia watanzania wengi wanafanya mambo yao kwa kutegemea kauli zake. Anadhani yale aliyokuwa anayaita mahaba kwenye mikutano yake ni unyumbu.

Hawa watu wanaomshauri Lowassa waache kumdanganya. Kuna baadhi ya watu wanamjaza ujinga ili adhani ana hekima na busara zaidi ya Watanzania wengi.

Lowassa na wapambe wake hawafahamu kama watanzania wengi wana haiba ya kutopenda vurugu. Hafahamu kama kuna chaguzi kuu nne zimefanyika na Tanzania imeendelea kuwa nchi ya amani na kuheshimiana. Hafahamu utawala wa machifu uliokuwa na nguvu kubwa (powerful influence)katika jamii nchini ulipigwa marufuku na Tanzania ikaendelea kuwa na amani na kuheshimiana. Hafahamu tuna makabila zaidi ya 120 yenye imani za kidini tofauti lakini yanaishi katika msingi wa kuheshimiana na undugu.

Lowassa anataka kutufanya wajinga kama hatufahamu kuwa kitendo cha kuita waandishi wa habari na kujitangaza mshindi wa Urais halafu akaitaka NEC imtangaze ilikuwa ni dhamira ya ku-instigate violent lakini wananchi wengi walimpuuza.

Lowassa na wapambe wake wangetafuta kwanza uzoefu kuhusu haiba ya Watanzania kutoka wapinzani ambao wamekuwa katika uwanja wa upinzani kabla yeye hajawaza/kufikiria kama kuna siku atakuja kuwa mpinzani wa serikali ya CCM.

Kinachoonekana kwa sasa Lowassa yuko katika safari ya kisiasa ambayo Augustino Mrema amepitia! Lowassa has gone from hero to zero! As a politician, he is finished. There is no way back for him.

Ni nani anamshauri Edward Lowassa? Mwacheni akachunge ng'ombe wake Monduli!
We na bosi wako membe mngefanya juhudi za kuing'arisha CCM NA ACT

MTASHANGAA NYIE ACT (CCM B) Mnakua chama cha msimu wa UCHAGUZI

NA KIONGOZ WENU MCHUMIA TUMBO
 
Badala ujenge chama chako cha ACT unadhani una ubavu wa kupambana na Lowasa!

Wewe utabaki kudanganya wajinga wenzio kama kina Machemli na matokeo yake wanaishia kupata kura 1820...
Huyu mbugila anajiona ana akili sana

Km yeye ana akili mbona hatujawahi kusoma vitabu vyake au avumbue kitu kipya
Zitto anapenda kujikweza
Mjivuni CHIKU ABWAO alimshauri eti atamshinda msigwa pale iringa
Kilichotokea ni aibu kwa zitto na pesa za gaddafi mlizokula hazijazaa matunda

Zitto amekua mnafiki anatafuna maneno yake

Alisema hawatokua sehemu ya ukawa ila watashirikiana kuhakikisha CCM inatoka madarakani lakin mwisho wa siku ACT WAKAWEKA MGOMBEA na hiyo ni baada ya kupewa pesa na membe.

Shukuruni katiba inayotumika ni ya 1977
 
Kuwa na yesu huku unamjadili shetani ni ungese.na hivyo hivyo kumjadili mtu ambae unaamini ni dhaifu ni ungese mwingine mkuu.kumjadili mtu mliyekuwa mnashindania nae kitu na mmemshinda ni kumwogopa.lowassa bado ni tishio.kwanini hukuja na mada ingine ukaja na hii.lowassa anakereketa sana.halafu lowassa ni mtu mzito sana humu nchini.aidha ukatae au ukubali lowassa atapaa kama tunavyompaisha wote tunaochangia mada hii.
 
Nadhani ifike mahali mtu ujipambanue mwenyewe umeachieve nini au umeacha legacy gani kwenye hii nchi kabla ya kumponda mtu kama Lowassa. Hata wale waliokua wanaongea vibaya juu yake ni kutokana na uchaguzi..pamoja na hayo yote walikua makini sana katika maneno yao
wengi ni wanasiasa mashuhuri nchini
leo hii anakurupuka mtu hajui hata kesho yake na elimu yake ya brn...Lowassa,lowassa...uchaguzi umeisha EL atabaki kua mtu mwenye influence kubwa sana nchini.(Hata ukipinga ukweli wa namba utakusuta,moyoni unaelewa) hivyo anasikilizwa na watu wengi na bado hekima zake zinahitajika.Tujenge nchi acheni uoga.
Kina binadamu ana nafasi yake katika maisha na taifa.

Kina binadamu anapimwa na kuchambuliwa kutokana na nafasi yake katika maisha na taifa.

Kina binadamu ana legacy kulingana na nafasi yake katika maisha na taifa.

Ninamchambua Lowassa kutokana na nafasi yake.

Suala la Lowassa kusikilizwa na wengi siyo mjadala kwa sababu hata shetani anasikilizwa na binadamu wengi sana!
 
Huyu mbugila anajiona ana akili sana

Km yeye ana akili mbona hatujawahi kusoma vitabu vyake au avumbue kitu kipya
Zitto anapenda kujikweza
Mjivuni CHIKU ABWAO alimshauri eti atamshinda msigwa pale iringa
Kilichotokea ni aibu kwa zitto na pesa za gaddafi mlizokula hazijazaa matunda

Zitto amekua mnafiki anatafuna maneno yake

Alisema hawatokua sehemu ya ukawa ila watashirikiana kuhakikisha CCM inatoka madarakani lakin mwisho wa siku ACT WAKAWEKA MGOMBEA na hiyo ni baada ya kupewa pesa na membe.

Shukuruni katiba inayotumika ni ya 1977
CDM bhana akisemwa Lowassa wao mashambulizi wanahamishia kwa zitto
 
wewe kenge maji usiongee kama unapumuliwa kisogoni!
Kwani wewe ukiwa unapumuliwa kisogoni huwa unaongea kama ninavyoongea?

Nadhani unafahamu binadamu tunapishana kwenye uzoefu.

Inaonekana una uzoefu sana kwenye masuala ya kupumuliwa kisogoni!
 
Hivi wakuu kuna kitu ambacho nashindwa kuelewa.. Lowassa alishindiwa uchaguzi... Pamoja na fyeka fyeka ya hapa kazi tu.. Pamoja na mzee lowasa kunyamaza kimya na vilevile kama alivyohahidi akishindwa atarudi kwao kufuga ngombe...swali langu ni kwanini Lowassa anaendelea kujadiliwa.. Haswa anabezwa anatukanwa sana...si jf, facebook, twitter.. Etc whats wrong?kwanini watu wasimjadili magufuli na kasi yake ya hapa kazi tu?
Ningetegemea lowassa asingejadiliwa kabisa especially kipindi hichi ambacho magufuli ana sifiwa dunia nzima kwa hapa kazi tu...?
Conclusion
Nachoona hapa huyu mzee ni kwamba ana nyota kali sana... Kwanin nasema hivyo.... Aliomba kibali kwa ajili ya mikutano ya kuwashukuru wananchi inchi nzima. Wakamkatalia alijaribu kule tanga.. Police wakaibuka.....
Hata na matangazo yake kama matatu yamepigwa pini kutotangazwa sijui yalikua yanalenga nini lakini yalipigwa stop kabla hata hajayatangazwa.... ITV walijaribu wakaishia kukirusha robo.. Kitu cha kujiuliza kama tayari ameshindwa ningetemea serikali wamuache afterall. Ni political loser nikitegemea kwamba kwenye mambo atakayofanya atafanya mistakes kibao na itakua political suicide........lakini naona serikali bado imebana.... Kwanin wanambana mtu ambae ni political loser... Kumbuka wamesema richmond yeye... Sijui fisadi.... Mara kanunua watu.. Blah blah kibao... Sasa kwa mtu ambae amechafuka hivyo nilitegemea aruhusiwe afanye mikutano yake afterall ni political loser... Lakin kama serikali ikiendelea kubana hivi basi serikali watakua wanajua jambo... Labda katika intellengisia inaoenekana labda ni tishio kwa serikali...
Mfano mwingine.... Wamefuta kazi bodyguard wa lowassa.. Sasa sijui kama hiyo ilikua politically motivated au ni kweli jamaa alikiuka procedure za kazi.. Lakini katiba ya inchi inasema waziri mkuu mstaafu na viongoz waliowahi kushika madaraka wanapswa kupewa ulinzi...
Naomba kuelemishwa why media is stil on lowassa?
 
Nadhani huu ushauri ungeanzia kwanza kwa Edward Lowassa ambaye kwa sasa kila anapokutana na kundi la Watu anaanza kudai amani iliyokuwepo baada ya uchaguzi mkuu imetokana na yeye kukaa kimya baada ya uchaguzi.
Nadhani huu ushauri ungeanzia kwanza kwa Edward Lowassa ambaye kwa sasa kila anapokutana na kundi la Watu anaanza kudai amani iliyokuwepo baada ya uchaguzi mkuu imetokana na yeye kukaa kimya baada ya uchaguzi.


tujuze,machafuko yatokanayo na uchaguzi duniani huwa yanasababishwa na nin?kwann viongozi hata wa upinzani tumesikia wanapelekwa ICC?Je,wanamchango gani kwenye machafuko?je,Tanzania haiwezi ingia huko?kwanin?
Ukiweza kutafakari maswali hayo basi utamuelewa lowassa!
Tatizo ni ujinga na umbumbu ulionao ndio unakuendesha!
 
Kwahiyo ulitaka tuuane au?
Tuuane kwa sababu gani?

Una maana unataka kusema tuuane kwa sababu Lowassa amesema maneno kuhusu uchaguzi mkuu.

Watanzania wengi wana hekima na busara lakini pia wana haiba ya kutopenda vurugu.
 
Mpuuzi ni yule anayedhani amani ya Tanzania alikuwa ameishikilia kwenye mdomo wake!

Mpuuzi ni yule anayedhani Watanzania wengi ni kama manyumbu!
Ukweli ni kwamba endapo Lowassa angekuwa hana busara wala hekima, na kuamua kuwashawishi watanzania zaidi ya MIL 6 waingie barabarani, leo hii nchi nzima ingekuwa eneo la makaburi.

Dunia nzima inahubiri amani na kwa watu wenye uelewa wanatambua kuwa kwa "hekima & busara za Edward Lowassa" leo Tanzania ina utulivu.
 
Niwe mkweli, sijamaliza kusoma UZI wako wote, nimeishia hapo uliposema Watanzania sio Manyumbu; sina hakika kama Lowassa kasema ukweli au wewe ndio umesema ukweli cause wote inaonekana mmetumia utashi wenu ku conclude mlichokisema yaani wewe pamoja na Lowassa; labda tufikiri hivi kidogo; Ni kwanini serikali imesitisha mikutano ya Chadema/Ukawa ili hali ccm wao wanafanya? Kumbuka kwenye hiyo mikutano ya Ukawa Lowassa ndio alitakiwa kua main speaker!? Serikali inaogopa nini? Baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa, hali za wasikilizaji wengi/Watanzania zilikuaje? Nimeanza kupiga KURA mwaka 1990 ki ukweli kabisa (hapa watu wazima wenzangu either wataniunga mkono au watakataa) sijawahi kuona nchi ina hali ya kupoa kama ilivyokua mwaka 2015; sina hakika kama Lowassa angetamka neno hali ingekuaje? Kwakweli sina hakika. Lakini pia hebu tujiulize, ilikuaje hata serikali ikanunua magari ya washawasha zaidi ya 700? Usije sema tu Watanzania sio manyumbu bila kujiuliza hayo maswali. Vita vya wenyewe kwa wenyewe duniani kote hua lazima mwanzilishi/kiongozi awepo, watu wanakua na mahaba na mtu Fulani and then mtu huyo akitamka neno lolote UPEPO hua unabadirika. Fatilia kilichotokea Kenya, Congo (zamani Zaire) Burundi ya sasa n.k. Kote huko ni kwasababu kuna mtu alitamka neno tofauti na watawala wanavyotaka. Yawezekana kwa ubishi wako hapa ndio we utaonekana hufikirii vizuri. Serikali ilijua, Usalama wa taifa walijua na hata waelewa pia walijua and this is why baadhi ya makanisa yalitangaziana maombi ya wiki kadhaa kwa kufunga na kumwomba Mungu ili AMANi iwepo, may be ndio maana Lowassa akakaa kimya. Think twice brother/sister
 
Dirty politics ndicho anacholalamikia kuna followers wanapata kind of harassment kutoka kwa watendaji wanaoendekeza ushabiki mfano mganga aliyeukataa msaada wa Mbunge Bukoba kisa ajapata maelekezo.......
 
Umendika utumbo eti Lowassa kaita waandishi wa habari na kujitangaza mshindi ,lini ? Wapi? Angefanya ivo unadhani ungekuwa JF muda juu??? Acha uzushi.
 
Back
Top Bottom