Ni nani anayemdanganya Edward Lowassa?

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,991
Dunia inatambua Lowassa ana utajiri wa kifikra kuhusu njia ya kuwa fisadi nchini Tanzania. Kinachoendelea kwa sasa kinadhihirisha Lowassa anahitaji huruma za kisiasa kutokana na mwenendo wake kisiasa. Anahitaji sana ushauri usio wa kinafiki kuhusu hatima yake kisiasa nchini.

Nilivyomsikia kwa mara ya kwanza akitoa madai kuwa ukimya wake baada ya Uchaguzi Mkuu umesababisha kuwepo amani nchini, nilidhani kinachomsumbua ni mihemko ya kisiasa.

Nilipomsikia pia kwa mara ya pili akitamka maneno hayo Mkoani Arusha wakati akishiriki katika kampeni za Uchaguzi wa Jimbo la Arusha ambao uliahirishwa katika siku ya Uchaguzi Mkuu baada ya kifo cha mgombea wa ACT-wazalendo Estomih Mallah sikushangaa sana.

Kilichonishangaza zaidi ni pale nilipomuona tena kwa mara ya tatu ndani ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri, Usharika wa Monduli akisema kunyamaza kwake baada ya wananchi kupiga kura kwenye Uchaguzi Mkuu 2015 kumewafanya wananchi wasiuane. Eti anadai wananchi walikuwa wanasubiri neno lake ili waingie barabarani na kuanza kuuana.

Lowassa anataka kutuambia watanzania wengi ni kama nyumbu kwamba kila atakalolisema watalifuata au kulitenda. Anataka kutuambia watanzania wengi wanafanya mambo yao kwa kutegemea kauli zake. Anadhani yale aliyokuwa anayaita mahaba kwenye mikutano yake ni unyumbu.

Hawa watu wanaomshauri Lowassa waache kumdanganya. Kuna baadhi ya watu wanamjaza ujinga ili adhani ana hekima na busara zaidi ya Watanzania wengi.

Lowassa na wapambe wake hawafahamu kama watanzania wengi wana haiba ya kutopenda vurugu. Hafahamu kama kuna chaguzi kuu nne zimefanyika na Tanzania imeendelea kuwa nchi ya amani na kuheshimiana. Hafahamu utawala wa machifu uliokuwa na nguvu kubwa (powerful influence)katika jamii nchini ulipigwa marufuku na Tanzania ikaendelea kuwa na amani na kuheshimiana. Hafahamu tuna makabila zaidi ya 120 yenye imani za kidini tofauti lakini yanaishi katika msingi wa kuheshimiana na undugu.

Lowassa anataka kutufanya wajinga kama hatufahamu kuwa kitendo cha kuita waandishi wa habari na kujitangaza mshindi wa Urais halafu akaitaka NEC imtangaze ilikuwa ni dhamira ya ku-instigate violent lakini wananchi wengi walimpuuza.

Lowassa na wapambe wake wangetafuta kwanza uzoefu kuhusu haiba ya Watanzania kutoka wapinzani ambao wamekuwa katika uwanja wa upinzani kabla yeye hajawaza/kufikiria kama kuna siku atakuja kuwa mpinzani wa serikali ya CCM.

Kinachoonekana kwa sasa Lowassa yuko katika safari ya kisiasa ambayo Augustino Mrema amepitia! Lowassa has gone from hero to zero! As a politician, he is finished. There is no way back for him.

Ni nani anamshauri Edward Lowassa? Mwacheni akachunge ng'ombe wake Monduli!
 
Last edited:
Cha
Dunia inatambua Lowassa ana utajiri wa kifikra kuhusu njia ya kuwa fisadi nchini Tanzania. Kinachoendelea kwa sasa kinadhihirisha Lowassa anahitaji huruma za kisiasa kutokana na mwenendo wake kisiasa. Anahitaji sana ushauri usio wa kinafiki kuhusu hatima yake kisiasa nchini.

Nilivyomsikia kwa mara ya kwanza akitoa madai kuwa ukimya wake baada ya Uchaguzi Mkuu umesababisha kuwepo amani nchini, nilidhani kinachomsumbua ni mihemko ya kisiasa.

Nilipomsikia pia kwa mara ya pili akitamka maneno hayo Mkoani Arusha wakati akishiriki katika kampeni za Uchaguzi wa Jimbo la Arusha ambao uliahirishwa katika siku ya Uchaguzi Mkuu baada ya kifo cha mgombea wa ACT-wazalendo Estomih Mallah sikushangaa sana.

Kilichonishangaza zaidi ni pale nilipomuona tena kwa mara ya tatu ndani ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri, Usharika wa Monduli akisema kunyamaza kwake baada ya wananchi kupiga kura kwenye Uchaguzi Mkuu 2015 kumewafanya wananchi wasiuane. Eti anadai wananchi walikuwa wanasubiri neno lake ili waingie barabarani na kuanza kuuana.

Lowassa anataka kutuambia watanzania wengi ni kama nyumbu kwamba kila atakalolisema watalifuata au kulitenda. Anataka kutuambia watanzania wengi wanafanya mambo yao kwa kutegemea kauli zake. Anadhani yale aliyokuwa anayaita mahaba kwenye mikutano yake ni unyumbu.

Hawa watu wanaomshauri Lowassa waache kumdanganya. Kuna baadhi ya watu wanamjaza ujinga ili adhani ana hekima na busara zaidi ya Watanzania wengi.

Lowassa na wapambe wake hawafahamu kama watanzania wengi wana haiba ya kutopenda vurugu. Hafahamu kama kuna chaguzi kuu nne zimefanyika na Tanzania imeendelea kuwa nchi ya amani na kuheshimiana. Hafahamu utawala wa machifu nchini ulipigwa marufuku na Tanzania ikaendelea kuwa na amani na kuheshimiana. Hafahamu tuna makabila zaidi ya 120 yenye imani za kidini tofauti lakini yanaishi katika msingi wa kuheshimiana na undugu.

Lowassa na wapambe wake wangetafuta kwanza uzoefu kuhusu haiba ya Watanzania kutoka wapinzani ambao wamekuwa katika uwanja wa upinzani kabla yeye hajawaza/kufikiria kama kuna siku atakuja kuwa mpinzani wa serikali ya CCM.

Kinachoonekana kwa sasa Lowassa yuko katika safari ya kisiasa ambayo Augustino Mrema amepitia! Lowassa has gone from hero to zero! As a politician, he is finished. There is no way back for him.

Ni nani anamshauri Edward Lowassa? Mwacheni akachunge ng'ombe wake Monduli!
Chaguzi zilizopita kuna mgombea aliwahi kupata kura 6m? Chaguzi zilizopita ziliwahi kuwa na mwamko ulioonyeshwa na wananchi kama uchaguzi huu? shirikisha akili kidogo acha kufikiria ndani ya box.
 
Hoja yako hapa ni nini?

Kwamba mwamko wa kisiasa umesababishwa na Lowassa?

Jaribu kwanza kutafuta maandiko/research kuhusu historia ya vyama vingi na chaguzi zake.
 
Hoja ni nini tena? Ukiyajua hayo maswali huwezi uliza unachouliza.Ni mgombea gani wa upinzani aliwahi pata kura 6+m?
 
Kwa nini wewe umeleta ujinga wako hapa? Ungepeleka pia kule.
Eti wewe ndie msemaji ukweli? Basi wakweli kwenu hawako. Ulianza vzr baadae naona munkari ukakupanda, ndio ukaanza kuandika ujinga. Muache Mungu aitwe Mungu, lakini shurti walivyorudia kuhesabu kura Tunduma za urais na ikaonekana wamekosea, pale pale angekataa matokeo yote ndio ungejua nini kingefuata.
 
Badala ujenge chama chako cha ACT unadhani una ubavu wa kupambana na Lowasa!

Wewe utabaki kudanganya wajinga wenzio kama kina Machemli na matokeo yake wanaishia kupata kura 1820...
 
Back
Top Bottom