Ni nani anayemdanganya Edward Lowassa?

Ni nani anayemdanganya Edward Lowassa?

lowasa alipata, kura, milioni kumi ccm wakachakachua...ni rais wetu halali
Hakuna anayekukataza kuishi katika matumaini hewa!

Sema Lowassa ni Rais wako! Usiwaweke watanzania wote katika mwanvuli wa fikra zako.
 
Tukujadili wewe au tumjadili Lowasa? Anyway, kafikirie tena upya ili utambue utofauti kati yako na Lowasa.
 
Nadhani huu ushauri ungeanzia kwanza kwa Edward Lowassa ambaye kwa sasa kila anapokutana na kundi la Watu anaanza kudai amani iliyokuwepo baada ya uchaguzi mkuu imetokana na yeye kukaa kimya baada ya uchaguzi.
Hakukaa kimya baada ya uchaguzi, yeye na bavicha wenzake waliitisha maandamano yasiyo na kikomo nchi nzima wananchi wakawapuuza
 
Hoja ni nini tena? Ukiyajua hayo maswali huwezi uliza unachouliza.Ni mgombea gani wa upinzani aliwahi pata kura 6+m?
Wingi wa kura alizopata una uhusiano gani na amani ya Tanzania?

Kwa fikra zako kwa sababu watu zaidi ya milioni sita walimpa kuwa kwa hiyo hata fikra zao amewashikia!
 
Huyu mzee ni janga kwa ulimwengu!
 
Ni punguani peke yake ndiyo anaweza kukubaliana na hizo porojo za Lowassa, anadhani watanzania wote wana akili za nyumbu.
 
Lowassa hana effect yoyote Tanzania amebakiza porojo tu.
 
Wingi wa kura alizopata una uhusiano gani na amani ya Tanzania?

Kwa fikra zako kwa sababu watu zaidi ya milioni sita walimpa kuwa kwa hiyo hata fikra zao amewashikia!
Uliza duniani kote nini maana ya wafuasi halafu ukipata jibu utagundua.Wafuasi siku zote huwa wanasikiliza kiongozi wao anasema nini na ukiangalia hata kwenye history uprising zote zilitokea hivyo
 
Mzee Lowassa ni good looser! ('sina msamiati wa kushindwa'by El)
 
Lowassa lowasa lowasa my ass!!!!anadhani watu walikua wanampenda saaana hajui kama siasa ni unanifiki tu?!hajachelewa bado!awatume vijana wake waingie mtaani tuone
 
Nimekubali sana uchambuzi wako mkuu, ila kwa kuongezea kidogo ni kuwa, mazingira ya kisiasa ya nchi yetu hayajaegemea sana ukabila kama ilivyo kenya. Lowassa hata kama angesema lolote, athari yake ingekuwa dogo.

Jengine ni kuwa, baada ya jumuiya za kimataifa (pengine kasoro chache) kuupongeza uchaguzi wa Tanzania, Lowassa alikosa hoja ya kusema lolote kwani angetoa kauli eti vijana waingie barabarani nadhani pamoja athari yake ingekuwa ndogo ila wale jamaa wa ICC wangemtia nguvuni na hapo ccm wangechekelea mno.

Lowassa asiwadanganye watu kuwa ameepusha umwagaji damu ila moyoni kwa lowassa ninauhakika alikuwa anaihofia ICC
 
Dunia inatambua Lowassa ana utajiri wa kifikra kuhusu njia ya kuwa fisadi nchini Tanzania. Kinachoendelea kwa sasa kinadhihirisha Lowassa anahitaji huruma za kisiasa kutokana na mwenendo wake kisiasa. Anahitaji sana ushauri usio wa kinafiki kuhusu hatima yake kisiasa nchini.

Nilivyomsikia kwa mara ya kwanza akitoa madai kuwa ukimya wake baada ya Uchaguzi Mkuu umesababisha kuwepo amani nchini, nilidhani kinachomsumbua ni mihemko ya kisiasa.

Nilipomsikia pia kwa mara ya pili akitamka maneno hayo Mkoani Arusha wakati akishiriki katika kampeni za Uchaguzi wa Jimbo la Arusha ambao uliahirishwa katika siku ya Uchaguzi Mkuu baada ya kifo cha mgombea wa ACT-wazalendo Estomih Mallah sikushangaa sana.

Kilichonishangaza zaidi ni pale nilipomuona tena kwa mara ya tatu ndani ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri, Usharika wa Monduli akisema kunyamaza kwake baada ya wananchi kupiga kura kwenye Uchaguzi Mkuu 2015 kumewafanya wananchi wasiuane. Eti anadai wananchi walikuwa wanasubiri neno lake ili waingie barabarani na kuanza kuuana.

Lowassa anataka kutuambia watanzania wengi ni kama nyumbu kwamba kila atakalolisema watalifuata au kulitenda. Anataka kutuambia watanzania wengi wanafanya mambo yao kwa kutegemea kauli zake. Anadhani yale aliyokuwa anayaita mahaba kwenye mikutano yake ni unyumbu.

Hawa watu wanaomshauri Lowassa waache kumdanganya. Kuna baadhi ya watu wanamjaza ujinga ili adhani ana hekima na busara zaidi ya Watanzania wengi.

Lowassa na wapambe wake hawafahamu kama watanzania wengi wana haiba ya kutopenda vurugu. Hafahamu kama kuna chaguzi kuu nne zimefanyika na Tanzania imeendelea kuwa nchi ya amani na kuheshimiana. Hafahamu utawala wa machifu nchini ulipigwa marufuku na Tanzania ikaendelea kuwa na amani na kuheshimiana. Hafahamu tuna makabila zaidi ya 120 yenye imani za kidini tofauti lakini yanaishi katika msingi wa kuheshimiana na undugu.

Lowassa na wapambe wake wangetafuta kwanza uzoefu kuhusu haiba ya Watanzania kutoka wapinzani ambao wamekuwa katika uwanja wa upinzani kabla yeye hajawaza/kufikiria kama kuna siku atakuja kuwa mpinzani wa serikali ya CCM.

Kinachoonekana kwa sasa Lowassa yuko katika safari ya kisiasa ambayo Augustino Mrema amepitia! Lowassa has gone from hero to zero! As a politician, he is finished. There is no way back for him.

Ni nani anamshauri Edward Lowassa? Mwacheni akachunge ng'ombe wake Monduli!
mumeo si ndo mshauri wake?ukimtema mumeo lowasa atatulia
 
Back
Top Bottom