Ni nani anaemiliki kiwanda cha ARV feki?

Ni nani anaemiliki kiwanda cha ARV feki?

kwa profile kama hizi nadhani itakuwa wazi sasa ni kwa nini hii nchi haipigi hatua. Lakini kama ni kweli watu wale wale walio tufikisha katika matatizo makubwa haya ya kiuchumi na kijamii wameamua sasa kutengeneza dawa ili watuue, kitu gani kingine tunaweza kusema!!!







































wanaingia kwenye siasa kwa kuchakachua kura ili wapate kuchakachua dawa za wagonjwa wa ukimwi, ama kweli ccm ni janga kuu kuliko ukimwi.
 
Ni bahati ARVs feki zimeshitukiwa.
Tujiulize; ikiwa hizo ARVs feki zilizoshitukiwa TPI wameshakula chao kabla ya kuzizalisha kutoka Serikalini au Bil Gate, Je, dawa za malaria na nyinginezo wanazozitengeneza ambazo hawana uhakika wa soko, hali ikoje?
Kuna kikundi cha wanasiasa na watawala wanachezea afya za Watanzania.
Kuanzia leo sitatumia wala kununua dawa za TPI, liwalo na liww!
 
Wanaohusika ni pamoja na Mbunge wa CCM, Zarina Madabida.

Ni kweli ni mbunge Zarina Madabida. pia anamiliki pharmacy za Hito pharmacy. pia nyuma yake inasenekana yupo EL kama mwanashea. wanashea wengine wanajanvi ongezeeni majina kama mbawajua. ila kwenye hili sakata mbona sijasikia mkurugenzi Wa TFDA kusimamishwa? kwa sababu yeye ndiye anayezihakiki sawa.
 
Hapa mnaowaita mafisadi hili hawahusiki nalo isipokuwa Madabida na Madabida na rais Kikwete si uhusiano wao unajulikana. Nyie jifanyeni wajanja muendelee kuchonga, mtafuatawa hapa hapa jamii forum. Ohhh mnaitania serikali. Mie ngoja nikae kimya. Niwe mwangaliaji. Kama mnabisha waulizeni waliokuwa wanamfuatafuata kwenye jengo la machinga complex, Ni Madabida huyo huyo
 
Hapa hakuna cha dawa feki,TPI watakuwa walichemsha wakati wa production wakaamua kufunika kombe mwaharamu apite.
Ndio U-fake wenyewe huo.., kuachia bidhaa duni kuingia sokoni.., hii kampuni ishapata doa inabidi kunyanganywa tender zote na kufungiwa na watu kuwajibishwa
 
Mi nafikiri km Tume ya Haki za Binadamu inaweza kuishitaki serikali huundo wakti wake, kwanza ile ya Mwangosi na pili hili la ARVs, sioni cha kungoja hapo maana haki za binadamu zimekiukwa kwa kiasi cha kutisha tena kwa muda mfupi, labda kwa kuwa nayo hio tume ipo kwa ajili ya kuilinda serikali.
 
Kuchakachua dawa za binadamu???
Hapa ndipo unasikia viongozi wote wa vyama wangeungana bila siasa na kama ni kweli basi huyu pharmacist angeadhibiwa kwa kufungwa jela miaka ya maisha yake yote aliyobakiza hapa duniani .
 
Do! Ukiona chochote chenye makona ujue magamba yapo! nakumbuka kuna kiongozi wa serikali alikanusha nimemsahau sijui anajiskiaje
 
Hapa mnaowaita mafisadi hili hawahusiki nalo isipokuwa Madabida na Madabida na rais Kikwete si uhusiano wao unajulikana. Nyie jifanyeni wajanja muendelee kuchonga, mtafuatawa hapa hapa jamii forum. Ohhh mnaitania serikali. Mie ngoja nikae kimya. Niwe mwangaliaji. Kama mnabisha waulizeni waliokuwa wanamfuatafuata kwenye jengo la machinga complex, Ni Madabida huyo huyo
hili ndilo limetufikisha hapa tulipo, na sina uhakika kama unakaa kimya sababu ya unafiki au woga.
lakini ukumbuke, waliotumia utawala wa Mwalimu kutisha wananchi wakati wa Mwinyi nguvu yao haikuwa kubwa tena, na wa wakati wa Mwinyi pia uliwaona akina Bhaghdad wakiswekwa jela hivyo hivyo hata wale wa wakati wa Mkapa kesi kibao ziko mahakamani na uhenda wakaishia jela. Hawa wa wakati wa JK, nao watake wasitake watafuata mlolongo huo huo.
Lakini kikubwa zaidi ni kwamba tunakuwa wanafiki sababu ya woga lakini haina maana kuwa ukiwa mwoga ndio utakuwa hufi, hata hao mafisadi wenye uwezo wa kwenda hospitali yoyote duniani (hata mwezini) wanakufa na hata kuuawa! Sasa wewe endelea na uoga wako ili usifuatwe na serikali hapa jf lakini utakula hizo dawa za ARV au hata za Malaria badindia na bado utakufa tu kabla ya siku zako.
Tetea maisha yako maana ukumbuke kuwa problems are there to be solved na kwa case kama hizi hapa kwetu ccm is a problem!

 
More info
Mr. Ramadhani Mabadiba - Trustee
Chief Executive Officer of Tanzania Pharmaceutical Industries Limited

Mr. Ramadhani Madabida studied business policy from the Curtin University of Technology, Australia where he attained a Master's degree in Business Administration in 1981. He has as well a Graduate Diploma in Business Administration from the same Institute having specialized in the management of marketing distribution channels.

He has a wide administrative and managerial experience having worked in both the public and private sectors for the last twenty-eight years. He is currently the Chief Executive Officer of Tanzania Pharmaceutical Industries Limited, which is one of the privatized former public enterprises.

Mr. Madabida has played aleading role in the privatization of the Tanzanian public pharmaceutical manufacturing sector. He was the Team Leader in the Preparation and submission of a proposal for Management participation in the ownership of Tanzania Pharmaceutical Industries Limited, conducted a Technical and Management Audit of Tanzania Pharmaceutical industries Limited and conducted a Due Diligence Review of Tanzania pharmaceutical manufacturing companies which were listed for privatization whose reports were submitted to Tanzania Venture Capital Fund for investment decision between January 1995 and July 1996.

He eventually prepared a Feasibility Study for rehabilitation and financing of capital items for Tanzania Pharmaceutical Industries Limited (TPI), the company he now leads and which he has done a great deal to transform. Under Mr. Madabida's leadership the company has managed to attract investments from both overseas and local investors. In the process the company is now implementing, in collaboration with Action Medeor (a German Medical Aid Organization), a Euro 5 million project financed by the European Union.

Apart from his normal duties, Mr. Madabida is the Chair of Tanzania Pharmaceutical Manufacturers Association; he is a member of the Governing Council of the Confederation of Tanzania Industries and seats on the Board of Katani Ltd – one of the largest Agro-Industrial businesses in the country and Chairs the Board of Directors of Tancord (1998) Limited.

In 2003 Mr. Madabida participated in the drafting and writing of a paper which was presented to the Institute of Medicine Committee on the ‘Role of Pharmaceutical Industry and Technology and its appropriate regulation in improving antimalarial drugs and producing them inexpensively (using artemisinins as an example). He has also participated and presented papers in seminars and workshops both nationally, regionally and internationally.
Source: ..::Unit Trust of Tanzania::..
 
Ni ya mbunge mmoja wa ccm yeye na mume wake majina yao yamenitoka kidogo ila walianza kuwa maduka ya phamarcy baadae huyo mama akawa anachezesha upatu baadae akawadhurumu wanawake wenzake yeye na mume wake ndio wakafungua kiwanda cha Dawa wenye data zaidi watakuja kuwapa A-Z

....wanaitwa MADABIDA...
 
kiwanda hiki kilikuwa na matatizo sana ya kuwalipa wafanyakazi mishahara,hali iliyosababisha wa pharmacia vichwa kukihama,inaoneka issue ya formulation wakati wa uzalishaji ndio inawanyonga sasa hawa jamaa
wamiliki ni Watanzania ngozi nyeusi wakiongozwa na Rama Madabida. wamefanya kazi kubwa kufikia hapo kutokana na ushindani toka makampuni ya watanzania wenye asili ya India! kuna uwezekano wa uzembe wakati wa kuzalisha hizo dawa ama hujuma! ushauri ni kwa bodi ya wakurugenzi na menejimenti kuwa makini sana ktk uzalishaji wa madawa yenye viwango!
 
sasa hapa wa kulaumiwa nadhani ni TFDA
Ndio U-fake wenyewe huo.., kuachia bidhaa duni kuingia sokoni.., hii kampuni ishapata doa inabidi kunyanganywa tender zote na kufungiwa na watu kuwajibishwa
 
Inatakiwa tuige sheria za China ni kunyonga tu watu kama hawa.

Haiwezekani kuwanyonga au kuwashitaki. Wako kwenye mtandao-ufisadi ambao ndio wamiliki wapya wa CCM na serikali yake. Zamani wakati umiliki wa CCM ulivyokuwa katika mikono ya wakulima na wafanyakazi kuwashitaki kama wahujumu uchumi ingewezekana. Kwa sasa watu kama hawa na kwenye mradi wa fedha ndefu na ambao wakubwa wameweka vimirija ka kunyonya asali, kuwakamata sio rahisi. Simply put they are in complicity with those supposed to catch and put them behind bars!

Halafu anakuja Hussein Mwinyi anamsimamisha kazi Mkurugenzi wa MSD! Tha is very naive and ameteurish! I think this country needs a Kipunga revolution
 
they will never succeed, tufiakwa! Hivi tulitokana wapi na watu hawa???

Waliletwa na majini; eti hayo majini ndio yanawalinda kwa wao kuvaa mapete makubwa mikononi!!! Elimu haijawasaidia bado wanaamini ushirikina!!
 
A point of interest, ni nani wa mbele na nyuma ya pazia wanamiliki hiki kiwanda? acheni wanaojua watujuze.

Ramadhani Madabida alishawahi kuwa Meneja wa RTC na mke wake Zarina Shamte Madabida alikuwa Meneja wa kampuni ya tAIFA YA MADAWA (NAPCO) makampuni hayo yote yamekufa katika hali ya kusikitisha kifisadi, wanafamilia hawa wamechelewa sana kujiingiza katika siasa, lakini baada ya kuwaona wenzao waliokuwa nao katika system enzi za Board of Internal Trade (BIT) Akina Mwapachu, Salome Mbatia , Henry Shekiffu, Athuman Janguo na wengine wameingia katika siasa na kupata mafanikio na wao wakaamua kuingia kwa kutumia nguvu nyingi ili kujinufaisha kupitia CCM, Zarina ni mwenyekiti UWT DSM na Mbunge viti maalum CCM, Ramadahani Madabida ligombea ubunge (CCM) Jimbo la Kilwa akangushwa na jamaa wa CUF, ........ lakini kwa wale waliowahi kufanya nao kazi ni watu wanaoijua pesa, ni wajanja wajanja, kile kiwanda cha Arusha, wanamiliki wao Mke ndio mtaalam wa Madawa mume ni mtu wa masoko na utawala na kuna kila la uwezekano wameamua kutafuta pesa za ziada kwa njia yoyote kama hii ya kudhuru maisha ya binadamu wenzao,..... ninaamini serikali hii haitawafumbia macho na itawachukulia hatua stahili
 
Back
Top Bottom