Unajua kama umefuatilia visa vingi vya mauaji!
Mara nyingi inakuwa kama game kati ya muuaji (hasa wale wauaji wataalamu) na mpelelezi husika.
Na mara nyingi huwa kunajengeka aina flani ya mahusiano kati ya watu hawa, na kwenye baadhi ya mauaji, muuaji anakuwa anawasiliana na upande wa pili aidha mpelelezi au maadui zake waliobakia... Wakati mwingine huwa inafurahisha japo haya ni maisha ya watu...
Sasa kama hii ni game na mara nyingi sana polisi huwa wanashinda ila kwenye hichi kisa cha Sophie naona sio tu polisi wamechemka bali ni taifa zima la Ireland limeangukia pua.
Kama hamna hujuma kubwa hapo (kwamba tuseme ni mchezo wa wakubwa) basi huyo muuaji ni balaa sana na alikuwa na lengo maalumu ndio maana ametumia staili amabyo hata wapelelezi wameshindwa kuoanisha na kumbukumbu zao na hata zile za Ufaransa...
Vyovyote vile kisa kitakavyokuwa ila huyo muuaji ni ameshinda hiyo game na kama ameshinda basi hiyo nchi sio salama sana.