Ni nani alikuwa bora zaidi, Drogba Au Eto'o?

Kinachombeba Etoo ni bahati ya kucheza kwenye timu kubwa zenye uwekezaji maridhawa hivyo ni rahisi zaidi kupata mafanikio. Kama Drogba angecheza Barcelona au Inter Milan huenda angekua na record zaidi ya Etoo.

Binafsi nampa Drogba kwa fighting spirit aliyokua nayo, Etoo pia sio mchezaji mbaya ila mazingira yalimbeba zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Unamfahamu etoo wakati anacheza Real Malorca kwa mkopo? Waulize Real Mardlid.

Etoo wakati anaenda barca, barca ilikuwa iko hovyo(ilikuwa inazidiwa hadi na valencia ya benitez) na wakati huo pia chelsea pia ndio inaibukia kwenye ushindani badala ya roman kuinunua.

Viwango vya barca vs chelsea havikuwa na tofauti kiivyo.

Lakini mpaka muda huo barca ilibebwa na wachezaji watatu, gaucho, deco na etoo kabla ya gardiola.

Hivyo kwa hii hoja yako Etoo ni bora mara mia kuliko drogba.

Uzuri wote walihamia hizo timu kwa nyakati moja(hawakupishana sana)
 
Kinachombeba Etoo ni bahati ya kucheza kwenye timu kubwa zenye uwekezaji maridhawa hivyo ni rahisi zaidi kupata mafanikio. Kama Drogba angecheza Barcelona au Inter Milan huenda angekua na record zaidi ya Etoo.

Binafsi nampa Drogba kwa fighting spirit aliyokua nayo, Etoo pia sio mchezaji mbaya ila mazingira yalimbeba zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app

Kwahiyo Chelsea aliyocheza Drogba ya kina Makelele, John Terry, Ashley & John Cole, Cavalho, Lampard, Joy Cole then Malouda ilikuwa average isiyo na uwekezaji mbele ya Intermilan ya kina Cambiasso na Balotelli aliyocheza Eto'o ?
 
Upinzani katika kandanda ni miongoni mwa mambo yanayoufanya mchezo huu kuwa kipekee.

Mfano ni nani bora kati ya Cristiano Ronaldo na Lionel Messi, kati ya Pele na Maradona au Patrick Vieira na Roy Keane?
Achana na hao bara la Afrika limebahatika kuwa na mashujaa ambao wamefanya mambo makubwa kwenye mchezo wa Kandanda.

Leo tuzungumzie moja kati ya magwiji na vipaji maridhawa kuwahi kutokea barani Afrika nao ni Samuel Eto'o na Didier Drogba ni nani asielikumbuka lile goli la kichwa dakika za lala salama dhidi ya Bayern Munich? Au ile kombinesheni matata ya Eto'o na Diego Milito au Eto'o, Messi na Henry?

Ndugu wanajamvi, kwa mtazamo wako unafikiri ni nani mshambuliaji matata wa Kiafrika kati ya Didier Drogba na Samuel Eto'o?
Tunapozungumzia magwiji wa soka Africa huwa tunasimama dakika moja huku tukipiga saluti kwa Jay Jay Okocha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Etoo alikua Bora zaidi ya Drogba ila baadae Drogba alipambana akawa Bora Kama etoo na zaidi labda kwakua wakati Drogba anazidi kuzeeka alikua anazidi kuwa hatari huku etoo alikua anapungua ukali....ila Etoo ni Bora zaidi ya Drogba

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom